Suala la moto mlima KIlimanjaro

Namche Bazar

Senior Member
Apr 8, 2019
105
152
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri.

Ni zaidi ya wiki sasa moto unaendelea kuwaka katika mlima Kilimanjaro.
Na kinachoonekana ni kujaza watu mlimani ambao wanaitwa kikosi kazi bila kufanya kazi ya kuzima moto,wengi wao wameenda kula na kupiga picha tu (selfie) na kuwa kero hata kwa watalii wanaolala kwenye kambi kwa mfano kambi ya Mweka juzi 27/10/ kuna kundi kubwa la wazima moto walikuwa wanapiga kelele usiku kucha kwenye mahema yao yaliyokuwa sio mbali na mahema ya watalii wa kigeni hivyo kupelekea kuwa kero kubwa sana.

Pia suala la uchafuzi wa mazingira na kutupwa ovyo chupa na maji na mifuko ya mikate,kwanini mamlaka husika isikemee utupaji wa taka hovyo ili hata baada ya moto kuzimika mlima uendelee kuwa safi na kuokoa gharama ambazo zitatumika kulipa vibarua ili wakasafishe na kubeba hizo takataka.

Ushauri:

Waache kupeleka watu wanaoenda kupiga picha badala ya kuzima moto,watu ambao hata wao wenyewe kutembea ni shida eti anapewa kazi ya kuzima moto kwa kuwa tu ni mwajiriwa toka fire brigade,polisi,NCCA nk

Watangaze kazi kwa vijana porters(wagumu) na mountain guides hawa wanaujua mlima vizuri na wana nguvu na spidi ya kutembea na kuzima moto kwa haraka kuliko kupeleka watu useless.
Viongozi na misafara yao wamejaa getini Mweka wakiamini kazi ya uzimaji moto inaendelea vizuri huko juu,kumbe watu wamepumzika,kupiga stori na kula na kunywa maji ya chupa ya Kilimanjaro for free of charge huku wakiendelea kulipwa.
Leo hii 29/10/2022 moto umezuia wageni waliokuwa wanatoka Baranco kwenda Karanga,bado tatizo lipo.

Nayaandika haya sio kwa nia ya kumuaharibia mtu/watu ila ni kutaka kumaliza suala la moto na biashara ya utalii irejee kama zamani bila watu kupata adha ya Moshi,kelele nk wawapo mlimani.
Asanteni.
 
Tokea nikiwa mdogo huo moto huwa unawaaka.

Tena huwa una musimu wake.

Miaka ile wazee walikuwa wanapanda kuuzima.

Ni kama kulikuwa na mambo fulani ya kimila yalikuwa yanafanywa.

Yaani huo moto ni kama unalipuka tu from no where.

Yupo mmoja alivalishwa mgorore hebu muulizeni kama walimpa siri ya huo moto.
 
Suluhisho la yote ni vizima moto vya kisasa, kupeleka watu wakachimbe vimitaro na kufyeka ili moto usisambae ni kufanya kazi kama tupo zama za kale
 
Suluhisho la yote ni vizima moto vya kisasa, kupeleka watu wakachimbe vimitaro na kufyeka ili moto usisambae ni kufanya kazi kama tupo zama za kale
Hayo kwa Tz yetu yatakuja baada ya miaka labda 20,ikiwa Kilimanjaro ndio hifadhi inayoingiza pesa nyingi za kigeni kwa sasa na hawawezi vizima moto vya kisasa,tushauri wafanye kwa njia za kizamani lakini angalau zenye unafuu na ufanisi mkubwa.
 
Hayo kwa Tz yetu yatakuja baada ya miaka labda 20,ikiwa Kilimanjaro ndio hifadhi inayoingiza pesa nyingi za kigeni kwa sasa na hawawezi vizima moto vya kisasa,tushauri wafanye kwa njia za kizamani lakini angalau zenye unafuu na ufanisi mkubwa.
Namna ya kizamani ndiyo inayofanya uwepo wa watu wengi bila kazi kufanyika
 
Sasa utalii wa hapo pesa zinaingia iweje ulinzi wa vitu vya muhimu kama moto kusiwe na vifaa vyakuzimia moto? Wakati mwingine tukidharauliwa na mabeberu tusilalamike.
 
Hili swala limeshindikana moto unawaka kwa kasi
Aibu kwa nchi wameshindwa kukaa na wizara kukakodiwa hata vizima moto nje ya nchi hata kama tumechelewa, mficha maradhi kifo humuumbua kwa hali ya ukame uliopo na hali inayoendelea eneo kubwa ni dhahiri lishateketea usiku wa jana moto unaonekana vizuri unavyowaka, wizara ijitafakari na watendaji wake
 
Back
Top Bottom