Suala la miradi kusuasua, wote tubebe lawama maana tulipaswa kubeba jukumu kwanza

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,074
Miradi mikubwa kwa midogo inaposuasua utasikia;

Kiongozi ametupa lawama kwa mkandarasi/mzabuni

Mwananchi anamlaumu kiongozi

Mkandarasi anamlaumu serikali

Yaani ni vurugu tu kila mmoja anarusha lawama kwa kutokamilika kwa mradi. Japo lawama kwenda kwa mkandarasi/mzabuni ndiyo huwa kubwa zaidi 'Ooh kachukua tenda na kazi haiwezi, jinga kabisa'

Tulishasema kuwa haki huinua taifa. Je tumemtenda kwa haki huyu mkandarasi? Sikia:
1. Anapochukua tenda kuna vifungu vinambana kuajiri wazawa
2. Anapochukua tenda kuna vifungu vinambana kulindwa na wazawa kulinzi na usalama (haruhusiwi kuja na jeshi lake)

Makadirio na usanifu anaoufanya mkandarasi huwa hauhusiishi eti na mifuko ya simenti, nondo na mafuta dizeli na petroli kwa ajili ya wizi. Mwisho wa siku akiibiwa hesabu zaje zikafeli akashindwa kufanya kazi anaanza kusemwa ooooh anazingua.

Nisiongee sana lakini tunaweza kufanya kitu:
1. Suala la kuajiri wazawa libaki palepale.

2. Suala la ulinzi tuliangalie upya. Inabidi wakandarasi waruhusiwe kuwa na kijeshi chao kidogo kwa ulinzi wa watu na mali zao. Kikundi hicho kiwe na silaha za moto. Kiruhusiwe kuwapiga risasi za miguu wezi. Kiruhusiwe inapobidi kutumia kani iwezayo kuua ili kujilinda (lethal force). Rejea sheria za uvamizi (no tresspassing, tresspassers will be SHOT) kwa baadhi ya nchi ambapo mwenye nyumba anaruhusiwa kumpiga risasi yeyote anayeingia kwenye eneo lake bila ruhusa!

Tunaweza tu kujitahidi kupunguza uonevu kwa kutaka uthibitisho wa video kwamba mtu alikuwa anaiba kweli. Siku hizi kuna teknolojia za Cctv na drones hayo mambo yanawezekana kabisaa.

Mwananchi huyo mwizi akiona kuna marisasi sidhani kama ataendelea kuwakosea heshima kwa kuwaibia mbele ya macho yao. Ni risasi tu pambaf 😕.

Tumechoka miradi kukwamakwama kila siku aaargh! Hatutaki mtu atupiwe lawama. Kila mmoja awajibike kwa majukumu na matendo yake.

Mafuta, simenti, nondo n.k vikiibiwa kwenye miradi sio hasara ya mchina au mturuki au mzungu tu bali ni hasara yetu sote.

Mbona kwenye migodi hakuna wizi wa kijingajinga hivi.

Mfano tukiwapeleka mahakama za uwekezaji kuwadai fidia. Halafu wakasema mradi ulikwama kwa sababu ya upande mmoja wa mkataba kushindwa kutimiza jukumu la kudhibiti wizi hata tulivyouripoti unadhani tutachomoa? Kimsingi tutawalipa tena fidia kwa kuwasababishia hasara wao😳. E eeh endelea kushangaa!

Nimemaliza maoni.
 
Tuache kuanzisha miradi ya kisiasa
Miradi ya kisiasa, fafanua kidogo tafadhali .................

Maana ukiangalia makaratasi, miradi huwa ina tija ikienda kama makaratasi yalivyopangilia na kukamilika.

Reli, umeme, barabara majengo airports etc zoooote huwa zina faida kubwa na ndogo zote tu hata hizo za kisiasa mradi vikamilike kwanza.
 
Mkuu, serikali ya CCM na watendaji wake ndiyo wenye kustahili kubeba lawama. Kwa nini unataka kuwabebesha lawama wengine wasiostahili!?

Je! Ni nani aliyeshiriki toka hatua za awali ya uteuzi wa kandarasi kupitia ushindani katika tenda, uingiaji wa mikataba katika kandarasi husika, na hatimaye usimamizi wa miradi husika!?
 
Miradi ya kisiasa, fafanua kidogo tafadhali .................

Maana ukiangalia makaratasi, miradi huwa ina tija ikienda kama makaratasi yalivyopangilia na kukamilika.

Reli, umeme, barabara majengo airports etc zoooote huwa zina faida kubwa na ndogo zote tu hata hizo za kisiasa mradi vikamilike kwanza.
Swali Zuri sana, iko hivi, kuwa kwenye plan ni one thing na Lini ianze na ianzaje ni kitu kingine, Kuna mifano ningekupa ila wacha niishie Hapa
 
Wala rushwa wamejaa serikalini, mtu amekupa rushwa utamsimamiaje?
Serikali ni watu kumbuka watu ndio wanaamua kudili vipi na mkandarasi kiujumla. So jamii inavyoangalia wizi unafanyika ndivyo hivovivyo viongozi wanavyoangalia miradi inasuasua. Viongozi nao ni wananchi ambao yooote ni serikali.

Basi kuepusha hilo ndo tukabidhi miradi kwa sharti moja tu. Iwe mvua iwe jua tunataka mradi ukamilike juni 2023. Usituletee swagga za umeibiwa sijui umenyimwa hiki a aaah.

Ukiona kuna mwizi wako rekodi piga risasi muue, na mtu akija kukuletea siasa sijui 10% mrekodi tumtangaze TBC na kwingineko tumchukulie hatua.
 
Waziri au KM umeenda ofisini kwake utaweza kumrecord? shida ni wizi unaanzia juu kushuka chini, mradi wa 3B lakini hapo hapo mnataka mkandarasi awape 500M mbaya zaidi ni kabla hata ya kazi haijakamilika.
 
Wewe utasema wizi unaanzia juu kushuka chini.

Wao watasema wizi unaanzia chini kupanda juu.

Wengine watasema upo katikati yaani ni tafrani tupu.

Sasa dawa n nn?

Basi mie bado sijafikiria vizuri kuhusu huo wa juu (unakaribishwa kuleta suluhisho). Ila hapa chini kwa waogawaoga risasi na shoti za umeme zitatosha
 
Kama boss wako haibi wewe utaibaje? tenda anatoa PS au mhudumu wa ofisi? anayeidhinisha malipo ni nani? mikataba inasainiwa na madereva na walinzi? majangili ni hayo yanayobebwa na V8 na kulindwa na polisi badala ya kuwa gerezani yapo kwenye ofisi za umma.
 
Hata mie nnapenda sana kuwawajibisha whusika wote lakini nimechagua ninaowezana nao.

Tena hawa wa mtaani ndio wanaoonwa hata na watoto. Hizo 10% usikute labda nyingine ni nadharia njama kuchafuana tu.

Lakini wamtaani ndio wanawafundisha taifa la kesho mbinu mbovu wakija kushika uongozi.

Makosa mawili hayabadiliki kuwa sio kosa kwamba kiongozi kaiba ndo na mi nnaiba

Hii ya kutupia lawama ni dalili za kutotaka kubeba jukumu kutupiana mipira.

Ni kama mke na mume hawaongei halafu mume anajisemea 'simuongeleshi sababu ye haniongeleshi pia' na mke naye aseme 'simuongeleshisa sababu kaninunia' kutupiana mipira
 
Kwa hiyo hata report ya CAG ni nadharia sababu tunawaonea wivu? NHIF aibu tupu 40B hazijulikani, Wizara ya Afya magari 200 hayajulikani yamenunuliwa wala mzabuni na hayupo, hiyo ni mifano michache.
 
Back
Top Bottom