Suala la Maji kukosekana: Tusimlaumu mama Samia, yeye hakuleta ukame!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,333
24,227
Sasa hivi nchi nzima tuna ukame ambao haujakuwpo kwa miaka kama kumi hivi.
Ukame huu unaleta athari mbili kuu, ukosefu wa maji ya matumizi ya binadamu na hvile vile kukosekana kwa maji ya kutosha kusukuma mitambo ya kutengeneza umeme.

Sasa, ukame unatukosesha maji mijini na umeme kwa pamoja.

Kwa miaka mingi tabia nchi imekuwa ikibadilika kwenda na kuwa hali mbaya zaidi kila mwaka.

Wengine walikuwa watoto, lakini 1973/4 palikuwa na ukame wa kutisha, tulikula ugali wa "yanga", unga wa njano wa msaada.
Kabla ya hapo 1965 napo kulikuwa na ukame( karbia miaka 10 kabla).
Mwaka 1987-89 vile vile kulikuwa na ukme(10 years later)
Mwaka 1997/98 vile vile-miaka kumi baadaye
Tukaja 2011, kwa marudio hayo hayo ya miaka karibia kumi .

Leo 2022, tuna ukame, miaka 11 na ushee baada ya 2011.

Kwa mlio wasomi humu JF, check the mateorogical data kwa miaka hiyo.

Tatizo watanzania tunasahau kwa karibu.
Mbaya zaidi ni kwa wanasiasa wasioweza kutumia scientific data ku plan for the future.

Tukumbuke pia kuwa huko Ulaya, ukame mwaka huu umekuwa mbaya kuliko kipindi chochote kwa miaka 50 iiyopita..
Wenzetu watachukua changamoto hiyo kuplan for the future.

Kwa upande wetu bwawa ka Kidunda lilikuwa lijengwe zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Tusimlaumu Mama Samia kwa hili.
Sayansi ilitueleza kuwa ukame utakuja mwaka huu 2022.

Na kwa hii kujirudia rudia ukame, tutapata ukame mwingine miaka ya 2031-2033.
Kwa waliosoma masuala ya Hydrology, hiyo ipo katika Gumbels Return Year Predictions za mvua kubwa na ukame.
 
Yeye kama kiongozi anatakiwa awe na mikakati ya kuzuia hili kutojirudia, na chama chake kimekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 60 kinastahili lawama kwa kutoweka reservoir za maji kama mabwawa za kutosha
Hawa watu wapo madarakani tukiwalipa mabilioni ya shilingi kwenye posho, mishahara na ulinzi ili watatue matatizo yetu,

sio kutujibu kwa kiburi kama kike cha mwendazake
 
Israel, Saudi Arabia, Qatar, Kuwait na Oman ambazo ziko jangwani hazina shida ya maji??
Sasa hivi nchi nzima tuna ukame ambao haujakuwpo kwa miaka kama kumi hivi.
Ukame huu unaleta athari mbili kuu, ukosefu wa maji ya matumizi ya binadamu na hvile vile kukosekana kwa maji ya kutosha kusukuma mitambo ya kutengeneza umeme.

Sasa, ukame unatukosesha maji mijini na umeme kwa pamoja.

Kwa miaka mingi tabia nchi imekuwa ikibadilika kwenda na kuwa hali mbaya zaidi kila mwaka.

Wengine walikuwa watoto, lakini 1973/4 palikuwa na ukame wa kutisha, tulikula ugali wa "yanga", unga wa njano wa msaada.
Kabla ya hapo 1965 napo kulikuwa na ukame( karbia miaka 10 kabla).
Mwaka 1987-89 vile vile kulikuwa na ukme(10 years later)
Mwaka 1997/98 vile vile-miaka kumi baadaye
Tukaja 2011, kwa marudio hayo hayo ya miaka karibia kumi .

Leo 2022, tuna ukame, miaka 11 na ushee baada ya 2011.

Kwa mlio wasomi humu JF, check the mateorogical data kwa miaka hiyo.

Tatizo watanzania tunasahau kwa karibu.
Mbaya zaidi ni kwa wanasiasa wasioweza kutumia scientific data ku plan for the future.

Tukumbuke pia kuwa huko Ulaya, ukame mwaka huu umekuwa mbaya kuliko kipindi chochote kwa miaka 50 iiyopita..
Wenzetu watachukua changamoto hiyo kuplan for the future.

Kwa upande wetu bwawa ka Kidunda lilikuwa lijengwe zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Tusimlaumu Mama Samia kwa hili.
Satyansi ilitueleza kuwa ukame utakuja mwaka huu 2022.
 
Mama hana makosa. Waziri wake (Mzee wa Drama) anafanya nini pamoja na Boss wa DAWASA. Hata ratiba ya rationing inawashinda kusupervise? It will be nice if we have daily briefing on the status of the water rationing other than that ni kuonyesha kiburi kwa wateja/wananchi. Out of interest, palikuwa hamna indication ye yote kama tutafika hapa? Sidhani mliaamka siku moja ndiyo ikatokea hii shida.
 
Mleta mada anaweza kudhani ametumia akili nyingi kufikiri na kujenga hoja, kumbe hajui alisemalo. Hivi wewe km baba mtoto wako akifukuzwa shule kwa kukosa karo utamjibu kuwa sio kosa lako ila ni la Mwalimu aliemfukuza, au watoto wakilala njaa sababu ya kukosa unga utawajibu kuwa sio kosa lako ni la wakulima kushindwa kuzalisha chakula kwa wingi au ni kosa la Mangi kushindwa kufungua duka.

Mleta mada unajua maana ya uwajibikaji wa Mzazi kwa mtoto au kiongozi wa serikali kwa watu wake au mfanyakazi wa serikali ndani ya ofisi ya umma kwa wananchi anaotakiwa kuwahudumia?

Unadhani kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa niaba ya walio wengi ni kwenda kula kiyoyozi ofisini na kusema mimi nimeshapata hayo mengine hayanihusu watajijua wenyewe.

Unadhani kupewa dhamana ya kuongoza wengine ni sawa na kuongoza familia yako.

Watanzania sijui wana matatizo gani ya akili yasio pona. Serikali iliweka utaratibu wa Elimu bure ili kutibu kwa wingi ujinga lakini kumbe ndio bado unaongezeka.

Mambo yanayogusa maisha ya mwanadamu sio ya kufanyia siasa za maji taka km ulizoleta hapa. Mahaba yako kwa chama chako yasiwe fimbo ya kuadhibu wengine kwa hoja mfu km zako. Watu mnapenda kukalili vihoja na kudhani ni hoja. Kauli km zako aliwahi kuzisema mwendazake, na kushaabikiwa na waliokosa Elimu ya K.K.K (Kusoma, Kuhesabu, na Kuandika) km wewe.

Kumbe ndo maana ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wababa kama wewe hawajui au wana kwepa majukumu yao na kudhani ni ya mwanamke. Hatimae mwanamke anamchoka na kujiondokea maana atakuwa anahisi anaishi na mume bwege.
 
Mleta mada anaweza kudhani ametumia akili nyingi kufikiri na kujenga hoja, kumbe hajui alisemalo. Hivi wewe km baba mtoto wako akifukuzwa shule kwa kukosa karo utamjibu kuwa sio kosa lako ila ni la Mwalimu aliemfukuza, au watoto wakilala njaa sababu ya kukosa unga utawajibu kuwa sio kosa lako ni la wakulima kushindwa kuzalisha chakula kwa wingi au ni kosa la Mangi kushindwa kufungua duka.

Mleta mada unajua maana ya uwajibikaji wa Mzazi kwa mtoto au kiongozi wa serikali kwa watu wake au mfanyakazi wa serikali ndani ya ofisi ya umma kwa wananchi anaotakiwa kuwahudumia?

Unadhani kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa niaba ya walio wengi ni kwenda kula kiyoyozi ofisini na kusema mimi nimeshapata hayo mengine hayanihusu watajijua wenyewe.

Unadhani kupewa dhamana ya kuongoza wengine ni sawa na kuongoza familia yako.

Watanzania sijui wana matatizo gani ya akili yasio pona. Serikali iliweka utaratibu wa Elimu bure ili kutibu kwa wingi ujinga lakini kumbe ndio bado unaongezeka.

Mambo yanayogusa maisha ya mwanadamu sio ya kufanyia siasa za maji taka km ulizoleta hapa. Mahaba yako kwa chama chako yasiwe fimbo ya kuadhibu wengine kwa hoja mfu km zako. Watu mnapenda kukalili vihoja na kudhani ni hoja. Kauli km zako aliwahi kuzisema mwendazake, na kushaabikiwa na waliokosa Elimu ya K.K.K (Kusoma, Kuhesabu, na Kuandika) km wewe.

Kumbe ndo maana ndoa nyingi xinavinjika kwa sababu wababa kama wewe hawajui au wana keeps majukumu Yao na kudhani ni ya mwanamke. Hatimae mwanamke anamchoka na kujiondokea maana atakuwa anahisi anaishi na mume bwege.
Mkuu kuwa na akili nyingi au kutokuwa na akili kabisa hilo ni suala la uelewa wako.
Usinilaumu kama hukuelewa nilichoandika.
 
Mama hana makosa. Waziri wake (Mzee wa Drama) anafanya nini pamoja na Boss wa DAWASA. Hata ratiba ya rationing inawashinda kusupervise? It will be nice if we have daily briefing on the status of the water rationing other than that ni kuonyesha kiburi kwa wateja/wananchi. Out of interest, palikuwa hamna indication ye yote kama tutafika hapa? Sidhani mliaamka siku moja ndiyo ikatokea hii shida.
,Mkuu yani unamlaumu waziri halafu unasema aliyemteua hana makosa? Makosa ya Mama ni kuendelea kumuacha mteule wake mzembe ofisini.

Hebu fikiria tu Waziri tuseme hajaleta ukame ni sawa, ila hata kusimamia na kuhakikisha ratiba ya mgao wa maji kama ulivyotangazwa na Dawasa unaenda sawa hilo nalo limemshinda kama ulivyosema sasa mtu kama huyo unaendelea kukaa nae kwenye baraza? Si unabariki uzembe wake?
 
Out of interest, palikuwa hamna indication ye yote kama tutafika hapa?
Indication ilikuwepo hasa kutokana na ukame wa huko nyuma kama mtoa mada alivyoeleza. Kwa muktadha huo, waliplan kujenga bwawa la Kidunda ili liwe limekamilika kabla ya ukame wa mwaka huu. Aliyemfuatia JK aliupiga chini mradi huo na kuanzisha miradi yake ya Chato Airport, Kigongo Busisi na mingine. Sisemi kuwa miradi hii mibaya au haina maslahi kwa Taifa, hapana. Ila huenda ilipaswa kutanguliwa kwa umuhimu na ule wa Bwawa la Kidunda. Jambo jema, Samia ameufufua mradi huu na tatizo la kupungua kwa kina cha maji kwenye mto Ruvu litaisha (japo sina hakika kama tatizo la maji Dar litaisha).
 
Hata tukose maji hadi tufe,sitakaa nimkumbuke yule mwendawazimu,

unafikiri angekuwepo angefanya nini? Hakuwa na akili za kutatua crisis yoyote, zaidi ya kuagiza jeshi
Ha ha ha!
Kama suala la korosho, naona Jeshi lingeagizwa kuleta maji toka ziwa Victoria!!!🤣🤣
 
Kwa mfano katika hili yeye angefanya nini zaidi ya kuwaambia yeye hakuleta ukame!
Guys what is this.
Hivi mawazili wa Uingereza wanaojiuzulu kila kukicha sababu ya economic crisis wao ndo waliosababisha. Fikiria Liz Truss kakaa siku 45 tu kajiuzulu, tena bila shuruti, kwani yeye ndo alileta economic crisis inayowatafuna.

Kumbuka viongozi wa siasa huchaguliwa kutatua kero. Hizo kero unadhani ni zipi. Tuanzie hapo.

ELIMU ELIMU ELIMU
 
Mkuu Uingereza yenye demokrasia ya miaka karne na karne huwezi ifananisha na Tanzania ambayo ina viongozi wengine ambao hata uelewa wa Climatic na hydrological trends hawana idea nazo.
Kidunda ilikuwa ijengwe zaidi ya miaka kumi iliyopita.
 
Sawa tumlaumu mwendazake tu hamna shida!Kwake napo hamna maji kama sisi?
 
Back
Top Bottom