Unachokisema ni kweli kabisa, ila ndugu yangu wananchi walio wengi hicho unachokisema wala hawakijui kwani maisha kwao ni magumu tu siku zote. Wanaojua hiyo tofauti ni wale waliozoea kuiba pesa serekalini, kwenda kwenye vikao visivyo na semina zisizo na tija, lakini kwa mtanzania wa kawaida wa kijijini ambaye hakopeshiki benki, anakula mlo mmoja, hospitali iko mbali, nyumba yake inavuja hata hali iwe ngumu vipi yeye anajua ni kawaida. Sasa hao waliozoe kwenda sokoni na mavx ya serekali, kwenye semina na vidosho acha waipate fresh. Nawaomba sana wafadhili washikilie hivyohivyo kama miaka saba hivi ili tuheshimiane.