Suala la ESCROW, Ikulu yabanwa zaidi

Suala la ESCROW, Ikulu yabanwa zaidi

Hivi yule mjinga mkuya aliliambiaje bunge!

Hii tabia ya viongozi kuongea uongo , jeuri na dharau imeota mizizi.
Huyo anatakiwa awajibishwe bunge lijalo kwa kulidanganya bunge.
Mr dhaifu km ana akili hana budi kumuwajibisha na huyo.
 
Mwezi Jan Kafulila amkomalie kwa kulidanganya bunge na umma.

Hata Mr dhaifu naye anastahili kukomaliwa.
Alipotoka marekani kwenye matibabu ya tezi dume akatoa speech ndefu kutupotezea maboya. (Japo haikufua dafu) . halafu akadanganya eti ya escrow hayajui.
Hivi huyu ni Rais wa Nchi au wa timu ya mpira?
Wewe Rais Nchi imebaniwa fedha za MCC , huna taarifa?
Wewe Rais Nchi imebaniwa almost billion 500 na ushee, geti huna taarifa?
Mr. Dhaifu ni muongo sana.
 
Hii tabia ya viongozi kuongea uongo , jeuri na dharau imeota mizizi.
Huyo anatakiwa awajibishwe bunge lijalo kwa kulidanganya bunge.
Mr dhaifu km ana akili hana budi kumuwajibisha na huyo.
Lao lilikuwa moja. Dhaifu naye alishasema hatochukua hatua yoyote mpaka afanye uchunguzi, alikuwa na wasiwasi na taarifa za CAG na PCCB? Hii longolongo yake sasa ni baada ya mkwara wa mabwana, halafu hagusii uchunguzi wa PCCB maana na yeye au wanafamilia wake wanaguswa.
 
Hawa ni viongozi wetu and it's a fact!, to hell with MCC, if we have to!.
Pamoja na madhaifu yake yote, sometimes namkubali sana JK, he is a beggar president, ila pia ni masikini jeuri!, yes sisi ni masikini, tunawapigia magoti kuwaomba misaada yao watusaidie, ila sio lazima tuwabong'olee!.
Mimi binafsi nimeufurahia msimamo wa JK kunyamaza kimya.


Mkuu Nguruvi 3, hawa wafadhili wengine nao wana yao!, hiyo ya misaada ni gia tuu ya kuingilia!, kama unadhania wanatusaidia kwa sababu wanatupenda sana, hivyo wanatuhurumia!, you are wrong!, some of them are just the "Greeks!, we have to fear them especially when they bring gifts!".

Niliwahi kuhudumu kwa wazungu fulani, nikiwa kama mshauri wao wa siasa, walikasirishwa sana jinsi Tanzania tunavyo tapanya na ku misuse Donners funds kwa ufisadi na spending on luxuries, nikawashauri, "stop the funding!", so that we can learn the hard way!, walinigomea!, wakatoa sababu kuwa if they stop the funding, there will be no medicine and people will die!, hivyo wanatupenda sana na wanatuhurumia sana!, but the truth is not!, later I realized sababu ya wema wao!.


Wengine wameumbwa na aibu, wengine kuomba kwao ni pride!, hivyo wakati kwao JK ni aibu, kwetu sisi ombaomba JK ni pride of a nation, keshokutwa tutampa serikali za mitaa, na mwakani tunairudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

Pasco
Mkuu hakuna mahali niliposema wafadhili wanatuonea huruma. Nilichosema ni kuwa kuliko hicho wanacholeta kwa njia na dhamira yoyote kutufikia ni vema wasilete maana hata kidogo kinachopaswa kufika hakifiki.

Pili, ukishakuwa omba omba huna ujanja lazima utakuwa mtumwa na kubong'oa hakuna mjadala.
Hakuna suala la masikini jeuri, masikini ni masikini tu. Huu umasikini wetu si wa mungu ni wa kujitakia.

Rais anatumia miaka 7 kupitisha bakuli badala ya kukaa chini na kuangalia bakuli linavuja wapi. Leo tumpe credit kuwa ni masikini jeuri. Hakuna jeuri ni kukosa vision.

Pesa zinazopotoea kwa wizi na udanganyifu ni nyingi kuliko wanzoleta wafadhili. Leo useme ni masikini jeuri.
Masikini jeuri ni ytule anayetumia resource zake chache kujikimu. Hatumaini MCC wakae na kumwelekeza afabye nini.

Kuna jeuri gani wakati anabadilisha baraza la mawaziri ana haha kufikia kashfa ili wafadhili wasigome.

Hatuna sababu za kuomba omba miaka 50 ya kujitawala. Tatizo letu ni kuwa na viongozi wasio na vision.

Kama kiongozi hajui kwanini sisi ni masikini, atawezaje kujua namna ya kutkwamua achilia mbali dhamira za wafadhili.

Lazima tukubali kuwa uongozi wa nchi yetu ni felia ya kwanza na ndio umasikini unaotukabili.
Sisi si masikini, ni masikini wa watu wa kutusaidia tujikombe. Badala ya kutusaidia wanagawa pesa kama njugu.
 
Wanaukumbi.


[h=2]MCC Statement on Board of Directors’ Discussion of Tanzania at the December 2014 Meeting[/h] Washington, D.C.—The U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) issued the following statement after its Board of Directors (Board) held its annual country selection meeting on December 10, 2014:
“MCC takes seriously all of its country partners’ commitments to combat corruption. At today’s meeting, MCC’s Board expressed continued concern over corruption in Tanzania, including the implications of the recent case involving Independent Power Tanzania Limited (IPTL). The Board noted that Tanzania has experienced a significant decline over the past seven years on the key indicator measuring efforts to control corruption. While the Board voted to allow Tanzania to continue working to develop a compact proposal—given its passage on MCC’s policy scorecards and its strong previous performance as an MCC partner—the Board stated its expectation that the Government of Tanzania must take firm, concrete steps to combat corruption before a compact is approved. Further, the Board voted to continue MCC’s engagement with Tanzania with the understanding that, in accordance with the Tanzanian State House December 9 statement, the Tanzanian government would act promptly and decisively on the late November parliamentary resolutions regarding IPTL. The Board also reaffirmed more broadly that Tanzania must undertake a series of previously agreed upon structural reforms to improve the efficiency, effectiveness and transparency of the energy sector, and more generally to deal with wider corruption.”

MY TAKE........

Sijui kama atapona mtu hapa kwenye suala la Escrow waliohusika wote kwenye huu ufisadi lazima wachukuliwe hatua za kisheria.
Kazi kwake Profesa wa Uchina, aamue kusuka au kunyoa.

Aidha aamue kuwalinda wezi wa mabilioni ya Escrow, matokeo yake wafadhili toka nje wataendeleza kibano chao cha kuzuia misaada nchini, kwa hali hiyo uchumi wa Taifa letu utadorora sana jambo litakalofanya wananchi wakichukie sana chama cha CCM, hali ambayo itasababisha CCM imfie JK mikononi mwake, kabla hajatoka madarakani, mwakani!

Au aamue kuchukua uamuzi mgumu wa kuwatosa makada wake wa CCM waliotukwapulia mabilioni ya shilingi za Escrow, hali ambayo itarejesha imani ya wananchi kwa chama cha CCM, na kwa hali hiyo kukifanya angalau kwa sasa kupata ridhaa ya wananchi, kuendelea kuitawala nchi hii.
 
..................

Pili, ukishakuwa omba omba huna ujanja lazima utakuwa mtumwa na kubong'oa hakuna mjadala.
Hakuna suala la masikini jeuri, masikini ni masikini tu. Huu umasikini wetu si wa mungu ni wa kujitakia.

Rais anatumia miaka 7 kupitisha bakuli badala ya kukaa chini na kuangalia bakuli linavuja wapi. Leo tumpe credit kuwa ni masikini jeuri. Hakuna jeuri ni kukosa vision..........................

Lazima tukubali kuwa uongozi wa nchi yetu ni felia ya kwanza na ndio umasikini unaotukabili......

UMESEMA YALOKUWA MOYONI MWANGU ASANTE NGURUVI3....Kwa kuongezea tu ni kwamba Rais alipoona wanamkubali hawa mabeberu basi akadhani ni mwenzao kumbe hajui kuwa hawa wankubeba na kukupa sifa kemkem halafu wanakutema kama maganda.
 
IMG_7175.JPG




Na Ibrahim Yamola na Suzan Mwillo, Mwananchi

Posted Ijumaa,Decemba12 2014 saa 14:32 PM


Kwa ufupi
MCC ni taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea. Shughuli za MCC zinajengwa katika msingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi pale tu unapoimarisha utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na kuondoa umaskini.


Fedha ambazo Tanzania ilipaswa kupata kupitia mradi huo wa MCC awamu ya pili ni Dola 450 milioni ambazo ni sawa na Sh765 bilioni.



Dar es Salaam. Wakati Serikali ya Marekani ikisema haitatoa fedha za Changamoto za Milenia (MCC) hadi utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow wa Sh306 bilioni utakapofanyiwa kazi, Ikulu imesema, Rais Jakaya Kikwete hatatekeleza agizo hilo kwa shinikizo la msaada huo.



MCC ni taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea. Shughuli za MCC zinajengwa katika msingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi pale tu unapoimarisha utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na kuondoa umaskini.



Taarifa hiyo ilisema Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la MCC kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini ilisema, katika mkutano wa bodi hiyo uliokutana Desemba 10 mwaka huu nchini Marekani, ulielezea hofu na masikitiko kuhusu hali ya rushwa inavyoendelea Tanzania.



Fedha ambazo Tanzania ilipaswa kupata kupitia mradi huo wa MCC awamu ya pili ni Dola 450 milioni ambazo ni sawa na Sh765 bilioni.

“Japokuwa bodi ilipiga kura ya kuiruhusu Tanzania iendelee na maandalizi kwa ajili ya mkataba wa pili kwa dhati kabisa, inaihimiza serikali ya Tanzania kuchukua hatua thabiti na mahsusi za kukabiliana na rushwa kama sharti la msingi kwa bodi hiyo kufanya uamuzi wa mwisho wa kuidhinisha mkataba huo.



“Bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania hapo Desemba 9 mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa uamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL,” ilieleza taarifa hiyo.



Katika tamko hilo kwa umma, Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress alisema “Kupigwa hatua katika mapambano dhidi ya rushwa ni muhimu sana kwa mkataba mpya kati ya MCC na Tanzania na katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara Tanzania.”



Aliongeza: “Tunatoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka kuhusu suala hili hasa kutokana na uzito wake katika masuala muhimu kadhaa ya maendeleo,” ilisema taarifa hiyo.

Hali kadhalika, Bodi iligusia makubaliano kadhaa yaliyofanyika na Tanzania iliahidi kufanya mageuzi ya kisera, kimuundo na kitaasisi ili kuongeza ufanisi na uwazi katika taasisi zake na katika sekta ya nishati.



Balozi Childress aliendelea kusema, “Tunafurahi kwamba mchakato wa majadiliano ya maandalizi ya mkataba wa pili utaendelea kwa miezi kadhaa ijayo. Tunapenda kusisitiza kuwa ni lazima ahadi hizi zitekelezwe kabla Marekani haijafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mkataba wowote mpya na Tanzania.”



Katika mkutano huo, Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi 10 zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizi zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.

Iwapo mkataba huo utapitishwa, utakuwa wa pili wa MCC kwa Tanzania kati ya mwaka 2008 na 2013 ambao ulitekeleza mkataba wa uwekezaji wenye thamani ya Dola za milioni 698 sawa na Sh1.18 trilioni ambao uliowezesha utekelezaji wa miradi ya maji, barabara na nishati ya umeme nchini kote Tanzania.


Chini ya mkataba huo, mtandao wa nyaya za umeme wenye zaidi ya kilomita 3,000 ulijengwa, jumla ya kilomita 450 za barabara pia zilijengwa, kadhalika mitambo mikubwa miwili ya usafishaji maji na njia ya kurukia ndege katika kiwanja kimoja cha ndege ilijengwa.



Kauli ya Ikulu

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema hilo ni jambo la kawaida kwani ili uweze kupata msaada huo ni lazima uwe umetimiza masharti na vigezo ambavyo miongoni ni masuala ya utawala bora na rushwa.

“Kabla ya kutia saini wanaangalia masuala ya utawala bora na rushwa na kama walivyosema wanasubiri kuona utekelezaji wake ni jambo la kawaida duniani kutokea.”



Kuhusu Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua za haraka dhidi ya waliohusika na sakata hilo, Balozi Sefue alisema, “MCC ipo au haipo Rais (Kikwete) anachukulia suala hili kwa umakini na atachukua uamuzi kwa misingi ya ushahidi uliotolewa.”



EIL yakazia

Wakala wa Uchunguzi wa Mazingira (EIA) wameitaka MCC kutokubali kuidhinisha mkabata huo na Tanzania wa dola 450 milioni hadi Rais Kikwete atakapochukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vya rushwa viliyotawala kwenye sakata la ujangili na usafirishwaji wa pembe za ndovu kwenda nje ya nchi hususani China.



Taasisi hiyo inayojihusisha na masuala ya mazingira ilitoa wito huo jana kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry na Mwenyekiti ambaye pia ni Mkurugenzi wa MCC, Diana Hyde kwamba wasitishe hatua hiyo kwa Tanzania.

Kutokana na hilo, EIA imeomba MCC ambayo imekuwa ikifadhili miradi ya maendeleo nchini kusitisha hatua hiyo kwanza hadi Rais Kikwete atakapolivalia njuga suala hilo.



Novemba mwaka huu, EIA ilitoa ripoti ya utafiti wa ujangili uliyoanika madudu dhidi ya mauaji ya tembo na namna meno yanavyotoroshwa nchini.



Mvutano bungeni

Katiba Bunge la 16/17 lililomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi uliopita, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya walivutana kuhusu ufadhili huo wa MCC uliokwama kutokana na ufisadi wa akaunti ya Tegeta Escrow.


Wakati wabunge wakiomba kiti cha Spika kiruhusu kujadiliwa bungeni kwa ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu ufisadi wa akaunti ya Tegeta Escrow, Mnyika alisimama na kusema, “kama ripoti hii haitajadiliwa basi fedha zinazotolewa na MCC tutazikosa.”

Baada ya kauli hiyo, Mkuya alisimama na kusema, “Si kweli kwamba tutazikosa fedha hizo kwani taratibu zinaendelea vizuri na mkataba utasainiwa Desemba mwaka huu na fedha hizo zitatoka Desemba.”

Kafulila



Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila akizungumzia uamuzi huo wa bodi ya MCC alisema, “taarifa hiyo imekuja wakati mwafaka...imenivisha nguo baada ya kuwa nimevuliwa bungeni na kuitwa mimi mwongo.”

Alisema, “Nilisema bungeni kwamba hasara tunayoipata kutokana na ufisadi huo wa Escrow ni zaidi kwani misaada tuliyokuwa tunaisubiri ya Sh900 bilioni kutoka Ulaya, Marekani Dola milioni 700 na ukijumuisha Sh306 bilioni ni zaidi ya Sh2 trilioni.”



Kafulila alisema fedha hizo zilikuwa zitoke tangu Septemba mwaka huu kama ambavyo Ghana imezipata lakini kutokana na uzembe wa Serikali ya Tanzania, imepoteza kiasi hicho cha fedha.

“Waziri wa fedha (Saada Mkuya) na Profesa Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo) walikana bungeni kwamba ninasema uwongo sasa ukweli umejulikana nani ni mkweli na nani ni mwongo,” alisema Kafulila jana.

Chanzo Mwananchi
 
wasitishe misaada yote mpaka ccm warudishe pesa zetu za escrow
 
Nafikiri hii iliwachefua sana Wamarekani:

"Mheshimwa Spika, Kamati ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,mabox, magunia na lumbesa"

Mambo magumu kwetu,Hata kama Raisi akiwafuta kazi vigogo waliotajwa katika ripoti ya PAC,masharti mengine yataongezeka ndio mwisho wa misaaada TZ.Sharti jipya la utawala bora na trasparency ni gumu sana ,achilia mbali na lile linalotesa Serikali la Ufisadi.
 
Ahsante Mungu kwa kutunusuru watz. Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu adiyependa kulinganishwa na miungu. Viongozi wetu ni miungu wamewafanya watz wamwache Mungu wao wa kweli na kuwaabudu wao.
Laana ya mwalimu nyerere imemkamata ipasavyo jk. Nyerere alisema ukiona mtu anakimbilia Ikulu mwogopeni kama ukoma. Maneno ya baba wa Taifa yametimia. Jk hakwenda Ikulu kuwatumikia watz bali familia yake na ndugu zake. It is a shame! Mungu Ahsante kwa kumuaibisha maana mali za udhalimu anachuma yeye na familia yake hawatazila kamwe maana ni moto ushukao toka Mbinguni.

Misaada yote ikatwe na mikataba yote ya kinyonyaji (uwekezaji wa madini na gesi) ivunjwe watz tuanze kuijenga nchi upya. Watz tumwombe Mungu atupe viongozi kutoka kwake; wacha Mungu na wenye hofu. Ikiwezekana atuondolee kabisa kizazi cha awamu ya nne ya jk chenye laana ya kuliangamiza taifa. Mungu uinuliwe na kutukuzwa MILELE hata MILELE. Amen.
 
majizi makubwa haya yanaenda kukaa hoteli kubwaa za gharama kumbe yamatumia hela za escrow
 
msione watu hawachukuliwi hatua,ripoti ya PAC ilisema ikulu ili sain hela zitolewa .ndomaana wakina tumbili wamekoma hawataki kuachia ngazi wanaona wanaonewa .hawataki kumlindia heshima babao.hawa ni viongozi matumbo
 
wakina tumbiri wamemwaibisha mkulu.sasa mkulu kaamriwa asipowaengua hakuna kukwea pipa kwenda kwa docta wa tezi.mkulu mnavyomjua anavyopenda kukwea pipa.hawezi kukubali lazima awaengue
 
Ma V8 ya mawazir yote yameambiwa yarudishwe. Tamko rasmi jumatatu. :msela:
 
Masikini Tanzania as poor as we are, as beggars as we are, we can not be choosers!, tunasubiri kupangiwa!, hizi kelele za kulalamikia rushwa huku we don't do anything, hazitusaidii kabisa!, IPTL ni rushwa mwanzo mwisho!, Escrow sio rushwa bali ni utapeli tuu, sasa MCC wanasubiria utekelezaji wa maazimio ya Bunge!. Yaani kufuatia umasikini wetu, rais wetu sasa analazimishwa lazima afanye kitu ndipo MCC ipite!. Kiukweli mimi sijaipenda kabisa release hii, na hata kama JK alipanga to do something, he should have done before, lakini akifanya sasa itaonekana ni to bow down to pressure za mabeberu hawa na wakoloni mamboleo simply because we have to beg!.

If I ware him, I would have said, to hell with MCC, kama Escrow was a clean deal, it is clean!. If it is dirty, then it needs cleaning, but escrow ni matokeo tuu na sio chanzo, sijaona any efforts to deal na chanzo!.

We are real ignorants!.

Poor we!.

Pasco

You must be a beneficiary wa utapeli uliofanyika kwenye escrow kusema haya. Heshima ya Ikulu yetu imevunjwa kwa uzembe wa kutekeleza sheria tulizojitungia wenyewe. Unatarajia Ikulu hiyo inayoshiriki katika grand and institutionalized corruption iheshimiwe nje? Lazima uwe unajidanganya full stop. Ikulu zinazoshirikiana na kufuga matapeli wa kimataifa hazina heshima popote pale. Hata wachina wanaowapa fedha zao bila kudai accountability wana mtego wao, siku watakapodai fedha zao lazima zitutokee puani.

Hatuwezi kudai heshima kutoka kwa wengine wakati sisi wenyewe hatujiheshimu. Kuvunja sheria zetu wenyewe zinafanya hadhi yetu kama nchi inayojitegemea iwe mashakani - kwani wanaoshughulika na sisi wanajiuliza; hawa wasioheshimu sheria zao wenyewe, wataheshimu sheria za kimataifa? Tuwe wapole kwa hili. Ikulu yetu imejipaka kinyesi, lazima inuke na nzi waifuate. Ni nani yuko tayari kukumbatiana na aliyejipaka kinyesi?
 
Kazi kwake Profesa wa Uchina, aamue kusuka au kunyoa.

Aidha aamue kuwalinda wezi wa mabilioni ya Escrow, matokeo yake wafadhili toka nje wataendeleza kibano chao cha kuzuia misaada nchini, kwa hali hiyo uchumi wa Taifa letu utadorora sana jambo litakalofanya wananchi wakichukie sana chama cha CCM, hali ambayo itasababisha CCM imfie JK mikononi mwake, kabla hajatoka madarakani, mwakani!

Au aamue kuchukua uamuzi mgumu wa kuwatosa makada wake wa CCM waliotukwapulia mabilioni ya shilingi za Escrow, hali ambayo itarejesha imani ya wananchi kwa chama cha CCM, na kwa hali hiyo kukifanya angalau kwa sasa kupata ridhaa ya wananchi, kuendelea kuitawala nchi hii.

Hapa unasema kama vile yeye hakuhusika wala kuujua wizi huo!! Anasita kufanya chochote kwa sababu ndani yake nafsi inamsuta kwani hilo saga analijua mwanzo mwisho. Hata akiwatosa hao wenzie, bado watu wataendelea kumwangalia kwa macho mawili. Hili suala la IPTL alikuwa na uwezo wa kulimaliza kwenye utawala wake, badala yake ameligeuza kuwa uvundo atakaoondoka nao ikulu. Mmesahau kuwa Mkapa baada ya kuondoka ikulu alizomewa na watu kwa uvundo aliotoka nao ikulu? Huyu naye anajichafua mwenyewe, nadhani uwezo mdogo wa kutathmini hali ya mambo umefanya ajiingize kwenye uvundo wa IPTL. Kwa mtu mwenye maono, angefanya kitu ambacho watanzania wengekikumbuka. Badala yake anajichafua tu!!
 
msione watu hawachukuliwi hatua,ripoti ya PAC ilisema ikulu ili sain hela zitolewa .ndomaana wakina tumbili wamekoma hawataki kuachia ngazi wanaona wanaonewa .hawataki kumlindia heshima babao.hawa ni viongozi matumbo

Waliomlindia heshima kwenye EPA waliambulia nini? Waliomlindia heshima kwenye richmond waliambulia nini? ...... Yaliyotokea huko nyuma ndo yanawafanya wengine leo wakomaee, kwani mwenye zigo lake wanamjua na wanajua kuwa wakiachia kilaini, wamejiangamiza wao huku mwenyewe akiendelea kukenua na kupika mengine. Ni afadhali waendelee kukomaa kuonesha kwamba wao si tatizo. Hata waking'olewa, wawe tayari kuliambia taifa kwamba wao ni wasafi na waliamlishwa kutekeleza uchafu - Gavana wa benki kuu anasimama juu kwani juhudi zake za kuzuia uvundo zimeainishwa. Ila hao wengine watakuwa na wakati mgumu sana kujitetea...... wakati mwingine ukipewa amri ambayo si halali ni lazima usimamie uhalali wakati mwingine ikilazimu uwe tayari kuachia maslahi na ukuu kwa ajili ya kutetea ukweli. Kutekeleza amri chafu huku ukijua ni kushiriki uchafu ..... huna utetezi utakaokusafisha.
 
Back
Top Bottom