Suala la ardhi halimo kwenye Muungano, Zanzibar wapo makini kulinda ardhi yao lakini wametuzidi akili kuimiliki ardhi ya bara

Nitukane tu mkuu.
Kwangu mimi kutishiwa kutukanwa ni jambo baya zaidi kuliko kutukanwa kwenyewe.

Kama unadhani hili linajadiliwa vema kwa kutukana, karibu sana. Niko tayari.

Here are the options:
1. Unaweza kunitukana hapa au PM
2. Naweza kukupa email yangu unitukane huko ikikupendeza.
3. Unaweza kutumia akaunti zangu za mitandao ya kijamii kunitukana (nitakutajia).
4. Kama kunitukana kwa njia ya simu kutaleta ufanisi zaidi, nitakupa namba yangu.
5. Pia ninaweza kuja ulipo (ukipenda), unitukane ana kwa ana.

Jisikie huru mkuu: NITUKANE hadi pale nafsi yako itakapotosheka.

NB: Nilidhani hapa tunachangia hoja kwa mitazamo tofauti maana JF ni jukwaa la mijadala huru likijumuisha mawazo kinzani.
Nadhani sikua sahihi, hakika ninatakiwa kutukanwa.

Karibu sana kwa matukano ewe ndugu "mtukana wengine".
Thaconfession
 
Zanzibar ni koloni la tz bara
Inashangaza sana mnabunge leo,mahakama na rais wenu lakini kila kitu mnapangiwa kutoka bara ,ni kama vile rimot inavyocontrol tv

Tanzania bara haitambuliki kama nchi, sasa itakuwaje na koloni?
 
Tanzania bara haitambuliki kama nchi, sasa itakuwaje na koloni?
Ccm wamecheza kama pele kwenye huu muungano,walivyo wanasa wa visiwani hakuna kufurukuta.
Nikuwa control kama remote ,Zanzibar haina uwezo wa kujitawala ikiachwa huru mu Oman ataingia hapo bora tuwatawale tu.
 
Ccm wamecheza kama pele kwenye huu muungano,walivyo wanasa wa visiwani hakuna kufurukuta.
Nikuwa control kama remote ,Zanzibar haina uwezo wa kujitawala ikiachwa huru mu Oman ataingia hapo bora tuwatawale tu.
Sasa umeongea ukweli. Zanzibar ilivamiwa na Nyerere. Lakini unajidanganya ukifikiri Wazanzibari hawawezi kufurukuta. Kinachowazuia Wanzanzibari sasa hivi ni kutambulika kimataifa (international recognition) siyo CCM. Likitokea taifa kubwa lolote likiitambua Zanzibar kama nchi, CCM hawawezi kufanya lolote.
 
Siyo ardhi tu:
1. Wanalinda tamaduni zao kwa nguvu
2. Wanalinda dini yao " Zanzibar ni sehemu ya JMT" lakini ina dini kama nchi
3. Wana bunge lao
4. Serikali yao
5.
 
Kwa sheria za Zanzibar, Mzanzibari Mkaazi anapewa hati ya kumiliki ardhi('Title Deed') lakini Mtanzania(Mtanganyika) anapewa hati ya matumizi ya ardhi kwa muda maalum mfano miaka 33('Lease')
 
Tofauti na Zanzibar ambako hairusiwi Mtanganyika kisheria kumliki ardhi
Kule Zanzibar si Mzanzibari wala Mtanganyika anaweza kumiliki ardhi. Ardhi ni mali ya taifa. Wanaruhusiwa watu kutumia ardhi tu na sio kumiliki. Akitokea mtu akakwambia anamiliki ardhi jua huyo anakudanganya. Nimesema hili kuondoa upotoshaji wa kwamba Zanzibar watu wanamiliki ardhi na hasa kwa vile humu jamvini jambo limetrend sana.
 
Kwa sheria za Zanzibar, Mzanzibari Mkaazi anapewa hati ya kumiliki ardhi('Title Deed') lakini Mtanzania(Mtanganyika) anapewa hati ya matumizi ya ardhi kwa muda maalum mfano miaka 33('Lease')
Hii si sahihi. Zanzibar watu wote wanapewa hati ya matumizi ya ardhi tu na si vingine
 
Hao Wazanzibari wenyewe hawamiliki ardhi wanapewa hati ya matumizi ya ardhi tu. Serikali ikiitaka hiyo ardhi inaichukuwa tu bali unalipwa fidia ya mazao na majengo ikiwa hujaiendeleza inachukuliwa bila yakulipwa hata senti.
Wote huku bara tunapewa hati ya umiliki kwa muda fulani
Ila kwa Zanzibar mtu kutoka bara hapewi hiyo hati anafanya kukodishiwa kama mgeni mwingine yeyote Ultima mmarekani au mwingereza,
 
We we ndio unataka kupotosha kuna kitu kinaitwa certificate of occupancy ambayo inampa mtu rght of occupancy kwenye eneo fulani kwa muda wa kuanzia miaka 33,66,au 99.
Mgeni hapati hiyo, mzanzibar anapata certificate of occupancy huku bar a ila mbara hapatiwi certificate of occupancy kule Zanzibar anakuwa anakodishiwa kama mgeni mwingine yeyote tuu,
Kuna tofauti kubwa na nyingi kati ya mtu anayemiliki ardhi kwa kutumia certificate of occupancy na mtu anayekodishiwa th
Mfano mdogo ukiwa na certificate of occupancy unaweza kuitumia kupata mkopo au hata kumdhamini mtu mahakamani ila document ya kukodishiwa haikubaliki
 
Mkivunja muungano mtaishi nchi gani? Tanzania ni hiyo mmeichoka na Tanganyika haipo tena. Sasa nyie machogo wenye chuki na Zanzibar mtakuwa raia wa nchi gani?

Wewe utakuwa umevimbirwa na maurojo.
Nchi kimsingi ni kipande cha ardhi majina yanaweza kubadilika ila wananchi wake bado wapo.
Mwaka 1964 territory ya tanganyika inajulikana ilikuwaje
 

Weka namba yako hapa ili nikupigie kabisa, haiwrzekani ukashindwa kuwafikiria wajukuu wa wajukuu wako Kama watakuwa na ardhi, unawaza wewe TU kwamba Tanganyika tupo wachache...weweeeee!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…