Oohhh I thought "mali ya umma" ni empowerement kwa umma kama si hivyo basi nimekosea. Basi hiyo aliyotuletea nyerere nadhani ilikuwa ni ufisadi.
Zomba,
Inaelekea hulijui kabisa Azimio la Arusha. Pia lazima ujue Ujamaa kwa miaka ya 60 ilikuwa ndio siasa iliyokuwa inafuatwa na nchi zilizo nyingi, ikiwa ni matokeo ya ubaya wa ubepari wa miaka ya 50 pamoja na matatizo yaliyokuwa yametokana na ukoloni. Kama huna habari, Nyerere mwenyewe alikuwa muumini wa siasa za kimagharibi mpaka alipobadilika baada ya Tanganyika kupata uhuru.
Pia kama umebahatika kuishi Europe, nchi kama UK, Holland au Scandinavia, utagundua kwamba ni wajamaa kuliko Tanzania ya miaka ya 80. Upebari wa sasa wa Ulaya umechukua nusu ya sura ya ujamaa kwa maana ya kwamba raia kuwa access kwenye vitu muhimu katika maisha kama elimu, afya na chakula. Huhitaji kufanya kazi au pesa ili kupata huduma hizo.
Lakini pia siasa zao zimechukua misingi ya kibepari kwenye ownership kwa maana ya kwamba individual ownership inaongeza ufanisi kuliko government ownership. Pia naona unachanganya kati ya productivity na innovation. Angalia vizuri maana ya maneno hayo mawili na huenda yakasaidia kwenye mijadala yako.
80% ya innovation inakuja kutokana na kitu kinachoitwa continous improvement na labda hiyo 20% ndio mawazo mapya kabisa. Hii nafikiri ni ishara tosha kuonyesha kwamba katika kila system kuna mambo mengi tu mazuri, hivyo huui kabisa na badala yake una improve. Azimio la Arusha lilikuwa na mambo mengi mazuri kama alivyoandika Kichuguu. Kosa tulilolifanya sisi ni kuua Azimio la Arusha na kuanzisha kitu kingine kipya kabisa. Hakukuwa na learning ya aina yoyote na ndio maana tumeanguka vibaya mno na huo ubepari wetu.
Kumuita Nyerere fisadi ni kwenda too low, unaonyesha kwa kiasi gani hata unashindwa kuelewa hata maana ya neno fisadi. At least Nyerere alituletea uhuru Watanzania, je wewe umefanya nini cha maana mpaka umuite Nyerere fisadi?