Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Pana mtu nilimsaidia. Kutokana na kumsaidia, there appears kulikuwa na price I pay. Fair enough. Lakini baada ya hayo, it appears that alihusika in a scheme to frame me into a situation, I am not sure to what end. Nilisikitika sana kuona the circumstantial evidence inapoint uelekeo huo.

Wema Ujinga -- Maandishi Kwenye Daladala.

No Good Deed Ever Goes Unpunished.
 
Tupo wengi ila pole Sana
Kwanza niwatakie heri ya Krismasi kwa JF Members wote. Ninatumai wote ni wazima wa afya, leo nimejaribu kutafakari baadhi ya mambo na kuamini ule msemo wa mfadhili "MBUZI UTAMLA MCHUZI" binadamu atakuudhi.

Nitazungumzia xperience yangu kuhusu the so-called friends and relatives

1. Kanda ya Ziwa.
Nikiwa Meneja wa Mkoa taasisi fulani ya fedha, niliwahi fuatwa na vijana wawili ambao walikuwa ni wahudumu wa hoteli kuomba niwasaidie as kiukweli japo kwa hali ndogo nilokuwa nayo ila nilisaidia wengi hasa nikikumbuka safari yangu ilivokuwa. Nakumbuka niliwapa nafasi ya kuwa Sales Reps na kwa kuwa walikuwa wanaishi pale hotelini na wafanyakazi wenzao, kuwarahisishia na kuwapa mwanzo mzuri niliwachukulia chumba nikalipa 6months rent, nikanunua kitanda, godoro, jiko, pasi etc and of course walishukuru sana. I personally trained those guys, gave support and invested much on them, mwisho they became the best in my branch. Wakatoka katika kulipwa 90,000/= per month na kuweza kupata minimum 1mil per month, in other words not less than 200k per week as commission. Of course was proud, ila kilichokuja tokea Mungu ndo anajua na ikanibidi niombe transferna kuhama mkoa. Ikatengenezwa figisu na ikaundwa team with my admin, vijana wakapikwa kidogo nifukuzwe kazi [emoji848] mwisho malipo ni hapa hapa duniani wote walifukuzwa na nilipohama tawi na mkoa mauzo yakadrop. Jana nimekutana na mmoja wapo ni Mchungaji now baada ya kupata malipo matakatifu, kuvunjika mguu, kukoswa kufungwa na kampuni kwa wizi, etc. Kaniomba samahani sana, nimemjibu nilishamsamehe muda mrefu sana na awe na amani.

2. Kanda ya Ziwa
Nilifatwa na kijana ambaye alihitaji kazi Ila kwa elimu yake hakukidhi vigezo, and the guy was passing through hell. Dah, roho yangu hii nikamuonea huruma nikamchukua na kununua bodaboda
nikampa mkataba 1yr malipo 70per week, kijana akaanza vzr na pesa alikuwa anadeposit bank na kuniletea slip. Kilichokuja kutokea siwezi kuelezea, mpaka nikatengenezewa kesi ambayo ni Mungu tu aliniokoa.. Yakafuata matukio ya kishirikina mpaka nyumba yangu nilojenga na nilokuwa nakaa ikabidi nihame kuhofia uhai wangu.

3. Kanda ya Kaskazini
Way back 2010 nikiwa nimejiajiri na nimefungua kampuni ikijishugulisha na fumigation, stationary services and supplies, music studio production audio and video, electronic money transfer. Nikamchukua mtoto wa ma mdogo nikamtrain jinsi ya kuproduce music kuanzia beat, vocal mixing etc, at first dogo akawa mtiifu sana, nikamuacha nikiwa nasimamia kazi ili nami nijigawe mambo yaende, dah nakumbuka ni siku moja nimesafiri Dar kufata mzigo na kuonana na my co director ambaye ndo aliwekeza capital, niliporudi sikukuta kitu maana alisafisha studio, ofisi za stationary na items zote. Nilipigiwa xm ucku nikiwa Dar, nilirudi nikiwa siamini ila nilipofika na kuona empty shelves and office, nililia sana na mwisho co director mwenzangu alitaka kunifunga, thanks to God alileta njia. Dogo nilikutana nae Dar kachoka vby, na alinitafuta yeye ila nimemsamehe toka moyoni.

4. Makazini
Nimewahi fanyiwa fitina na wasaidizi wangu kisa wivu na chuki, nikahamisha vituo na wao kuwa promoted kushika nafasi yangu ila within first quarter wote waliprove failure na kufukuzwa kazi baada ya ukweli kuja kugundulika..

Kwa kifupi nimepitia mengi sana kwenye maisha yangu, achilia mbali ajali, kuwa broke from a person who was well off financially, kuzulumiwa pesa nyingi sana na mwisho kutengwa, ila niwatie moyo wote ambao mna wakati mgumu au mnapitia magumu kamwe msikate tamaa, God is always in control.

Nikikumbuka nilipotoka na hapa nilipo, japo sijafika bado ambapo nilikuwa before ila namshukuru Mungu sana.

Kwa yeyote pia ambaye alifanya mema na kulipwa mabaya pls share with us, ili wengine wajifunze pia

Niwatakie sikukuu njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku ambayo siikumbuki vizuri,nilikia simu inaita, number mpya. Nilipokea. Jamaa mmoja ambaye baadae alijitambulisha kuwa amemaliza DIT na number yangu amepata toka tovuti ya board ya wakandarasi. Mbali na kuomba kazi,alinieleza mengi ya maisha yake na kwakuwa naelewa maisha, nilimuonea huruma Sana kukaa hapa mjini huna ndugu halafu huna kazi inatesa Sana.

Nilimwambia kuwa kwa sasa mimi sina mradi, ila kuna ndugu yangu yeye ana miradi mingi nitajaribu kumuombea.(jamaa hakujua kuwa nitakayempa kazi ni mimi na ninayempangia mshahara ni mimi) Hazikupita siku nyingi nafasi ikapatikana nikamwita dogo,(nikamwambia bro amesema niongee na wewe kuna nafasi) nikamfanyia interview kidogo nikamwambia siku ya kuanza kazi.

Alikaa ofisini kama wiki mbili ikabidi tumleleke site akafanye kazi, hapo ndipo shughuli ilipoanza.
Jamaa alipofika tu siku ya kwanza akanipigia simu,ananiambia mbona watu wako siwaelewi, nikamwambia huwaelewi kivipi? Akasema wapo local Sana, hawafuati utaratibu.Anadharau kila mtu,maneno machafu, Nikamwambia ndio maana tumekupeleka ili ushirikiane nao tuweze kumalizia mradi. Jamaa akanijibu hawezi shauriana na mtu Jambo lolote ,ikabidi nicheke Tu na kukata simu.

Mimi nilijua kuwa dogo ana Moto wa kufanya kazi na ugeni wa kazi kwa kuwa ametoka chuo, kumbe nilijidanya aise, hakuna mtu mpumbav* kama dogo niliyekutana naye maishani mwangu. (Kiukweli dogo longolongo Yuko vizuri)alichokifanya ni kumshawishi brother kuwa Mimi nimeweka watu wangu site ambao ninaiba nao, dogo alimshawishi brother hadi Imani yote ikatoka kwangu. Akaaminika yeye, kila kitu anapewa,useme nini juu ya dogo ukasikilizwa, ila Mimi nilimshauri Tu brother kuwa awe makini na watu na ili nisigombane naye, nikaacha wakaendelea na mambo Yao.

Leo brother amenitafuta na kuniambia kuwa hamielewi dogo(nimemwambia aendelee kumsikiliza na kushauriwa naye). Maana amegundua dogo ni mwizi wa kiwango cha standard gauge. Ameniambia anataka nimalizane naye maana Mimi ndiye niliyemleta.

Sasa mimi ninataka nimfundishe dogo somo la maisha yake. Sasa hivi nikimtimua haitamuuma maana kuna hela wamepewa siku chache zilizopita. Nasubiri hela ikate ndio namtimulia mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😅😅😅! Pole sana mm huku hayupo!hahhaa! Mie aliniambia oh nisaidie mmangu ni fukara sana msaidie afuge bloila...mwananke nikaingia mkopo kumpa mazake😅! Alinifanyia mchezo wa ajabu sana!shenz typ

Ulimkopea BF??
Hahaahaaa pole sana

Dah yakwangu mimi sitaki hata kukumbuka yani

Ila kuna mzee mmoja nilimuheshimu sana akaja kuniomba msaada nimtafutie fundi nikamtafutia akaenda akafanya kazi kaondoka kasharudi Mwanza mzee anakuja kusema fundi niliyempeleka kaharibu hicho kifaa chake kwahiyo tumeshirikiana kufanya utapeli. Kaniletea TZR imejaa wajomba kibao. Akajua mie mwepesi

Nikamwambia twende nyumbani kwako nikaenda kuangalia hicho kifaa kilichoharibiwa nikaenda dukani nikanunua mpya 1.2 mil nikampelekea halaf nikasepa. Abaki navyo vyote viwili

Karibu kila wiki tunakutana anaomba msamaha anasingizi mkewake eti ndo alimjaza upepo. Namwambia mimi nishakusamehe mbona we furahia maisha tu
 
.duhpole sana!hakua bf !
 
[emoji28][emoji28][emoji28]! Pole sana mm huku hayupo!hahhaa! Mie aliniambia oh nisaidie mmangu ni fukara sana msaidie afuge bloila...mwananke nikaingia mkopo kumpa mazake[emoji28]! Alinifanyia mchezo wa ajabu sana!shenz typ

[emoji23][emoji23][emoji23]poyee
 
Mwaka huu wakati tukianza mwaka mpya kulikuwa na nafasi za kazi kwenye company yetu. Kama kawaida zilitakiwa zijazwe, niliamua kwa dhati kabisa kutafuta vijana wenye sifa kutoka humu jukwaani (JF).

Mchakato ulifanyika na hatimae nkaajiri vijana watatu kutoka humu humu ambao mmoja alikuwa na experience kidogo na wawili are straight from school wamemaliza pale UDSM 2018. Mmoja yule mwenye experience baada ya muda mchache aliamua kuacha kazi baada ya kuomba salary increment na mimi kukataa hilo ombi kwa sababu haikuwa hata na miezi 4 kazini, kilichoniudhi ni namna alivyoondoka, alidanganya kwamba anaenda kumuangalia mzazi wake mgonjwa, na pia alichukua baadhi ya vifaa vya ofisini. Tulitegemea angekaa na Sisi ila ndio hivyo.

Wa pili kati ya hawa watatu ni kijana mmoja anaetoka kanda ya ziwa. Much know kwa sana, he considers himself the most knowledgeable and best employee out of all we have. Alikuwa akim criticise supervisor wake kwenye staff meeting in front of all other staff. Sio mara moja sio mara mbili. Nidhamu yake ni mbaya sana, alifikia mpaka kumtongoza one of the manager (foreigner) from the same office. At first alikuwa akiniheshimu/kuniogopa mimi tu because he knew I was making the calls. I went out of my way in helping him establish his life, salary ikikata mnamo tarehe 20 I would give him loans or my personal money. Baada ya kurudi one of my trip around August this year supervisor wake akanieleza mashakil yake. Nikaanza kukata all favors alizokuwa akipata from me. Akaona I was no longer a friend to her, I was only a boss at work and nothing more. As long as he could do his job and not insult anyone, everything was okey for me. At last, he had to go, and he had to go himself, what happened mpaka akaondoka mwenyewe sitaki kusema hapa but yeah he had to leave kwa kejeli na dharau na shutma kubwa dhidi yangu. Shutma moja ni kwamba mimi nimemchawia na namfanyia uchawi, usiku akilala ananiona namkaba🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Sijui why hakumtafuta Mshana Jr hahaahahahahha

Huyu kijana wa tatu bado nipo nae, he is doing good and he is my friend, he loves talking to me about Manchester United and would joke to me about Arsenal. He thinks I am the best boss in the world and may be he is reading this hahahaahahahah.

Sijisifii lakini humu jukwaani nimeshawasaidia watu si chini ya 10 msaada wa maana sio hizi 10,000 au 15,000 ila sasa nimeacha.

Ndio maana the other time nkamwambia Cresida be careful.

cc: SweetieLee and Karma

daah binadamu sisi mwee
 
Siku ambayo siikumbuki vizuri,nilikia simu inaita, number mpya. Nilipokea. Jamaa mmoja ambaye baadae alijitambulisha kuwa amemaliza DIT na number yangu amepata toka tovuti ya board ya wakandarasi. Mbali na kuomba kazi,alinieleza mengi ya maisha yake na kwakuwa naelewa maisha, nilimuonea huruma Sana kukaa hapa mjini huna ndugu halafu huna kazi inatesa Sana.

Nilimwambia kuwa kwa sasa mimi sina mradi, ila kuna ndugu yangu yeye ana miradi mingi nitajaribu kumuombea.(jamaa hakujua kuwa nitakayempa kazi ni mimi na ninayempangia mshahara ni mimi) Hazikupita siku nyingi nafasi ikapatikana nikamwita dogo,(nikamwambia bro amesema niongee na wewe kuna nafasi) nikamfanyia interview kidogo nikamwambia siku ya kuanza kazi.

Alikaa ofisini kama wiki mbili ikabidi tumleleke site akafanye kazi, hapo ndipo shughuli ilipoanza.
Jamaa alipofika tu siku ya kwanza akanipigia simu,ananiambia mbona watu wako siwaelewi, nikamwambia huwaelewi kivipi? Akasema wapo local Sana, hawafuati utaratibu.Anadharau kila mtu,maneno machafu, Nikamwambia ndio maana tumekupeleka ili ushirikiane nao tuweze kumalizia mradi. Jamaa akanijibu hawezi shauriana na mtu Jambo lolote ,ikabidi nicheke Tu na kukata simu.

Mimi nilijua kuwa dogo ana Moto wa kufanya kazi na ugeni wa kazi kwa kuwa ametoka chuo, kumbe nilijidanya aise, hakuna mtu mpumbav* kama dogo niliyekutana naye maishani mwangu. (Kiukweli dogo longolongo Yuko vizuri)alichokifanya ni kumshawishi brother kuwa Mimi nimeweka watu wangu site ambao ninaiba nao, dogo alimshawishi brother hadi Imani yote ikatoka kwangu. Akaaminika yeye, kila kitu anapewa,useme nini juu ya dogo ukasikilizwa, ila Mimi nilimshauri Tu brother kuwa awe makini na watu na ili nisigombane naye, nikaacha wakaendelea na mambo Yao.

Leo brother amenitafuta na kuniambia kuwa hamielewi dogo(nimemwambia aendelee kumsikiliza na kushauriwa naye). Maana amegundua dogo ni mwizi wa kiwango cha standard gauge. Ameniambia anataka nimalizane naye maana Mimi ndiye niliyemleta.

Sasa mimi ninataka nimfundishe dogo somo la maisha yake. Sasa hivi nikimtimua haitamuuma maana kuna hela wamepewa siku chache zilizopita. Nasubiri hela ikate ndio namtimulia mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app

doooh
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]hakika pains change people
Mimi nilimpokea kijana ambaye tulisoma pamoja ila hakuwa rafiki yangu, kupitia rafiki yangu akapewa namba yangu akiripoti kazini anicheki, nikamsaidia na alipaswa kupangiwa kituo kibaya sana huko vijijini. Nilizuia na alipangiwa near Head Office. Alipozoea aliwatumia watu wote niliomtambulisha kunichafua na kuhakikisha anakaa yeye katika kitengo nilichonacho pale HQ. Alifanikiwa kwani nilisimamishwa kazi kwa kutafutiwa kosa, hakunichek ingawa alikuwa na contacts zangu.
Nilimchunguza nikagundua alikuwa snitch sana. Jamaa wakaniambia dogo kakuzunguka anakaa katika kiti chako. Niliumia sana ila nilimchana ila alijibu shit sana. Likaundwa zengwe nitakaporudishwa job niondolewe HQ na walifanikiwa ila niliapa kutoendelea na kazi iwapo HR angefanya hivyo mbele yake HR. HR alipuuza na waliponiandikia barua ckuripoti na kuamua kuondoka eneo la kazi.
Nilipofika mtaani ndugu walifanyia collable ya chuki na dharau hata nilipoumwa hawakunichek licha ya kuwakatia bima za afya ndugu hao nilipokuwa kazini.
Nashukuru Mungu kwa mengi yaliyopita sasa nimepata kazi na ninalipwa mara 2 ya kile nilikuwa nalipwa awali.
Yapo mengi ndugu zangu maana kuna mwanamke pia nilimsaidia kusoma nimuoe ila alipomaliza alinitukana. Kwasasa simuamini mtu, naishi kama Dictator na ndugu wameanza kuniogopa maana kazi nimepata ofisi kubwa ambayo wao hawakuamini na walijua miezi 6 baada ya kuianza licha ya kutokea hapo hapo home.
Walidai nimerogwa mpuuzi nisiye na maana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiambiwagaa uongoo huwaga mnajaa upepo sanaa.. Hakuna falaa anaefanya kazi wizarani akakupoa elfu 25 sema tu jamaa alikupiga fix ili akuopoe vizurii na kweli ukajaaa... Akala kipochi na pesa ukampa
Wanaume wa siku hizi sijui wakoje mimi kuna lijit humu lilinipiga 25,000 yangu hakyaMungu inaniuma sana yaani halafu linafanya wizara ya mambo ya ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I don't remember if I ever did any good to others, rather some people are always doing good to me!
I'm humbled!
I'm grateful!
I wish to be generous to others, May Almighty God grant me the same!

Much respect to all who are good at doing good to others. You have a space in heaven!
Always never count your good deeds to others instead keep on doing it as much as you can.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom