STORY FUPI: Ni mara ngapi tunakosa zawadi kwa sababu hazikufungwa vile tulivyotarajia?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Lazima usome... mwanamke mmoja aliyeolewa alikuwa akitarajia zawadi ya siku ya kuzaliwa kutoka kwa mumewe.

Kwa miezi mingi alikuwa amevutiwa na pete nzuri ya almasi kwenye chumba cha maonyesho, na akijua mume wake angeweza kumudu, alimwambia kwamba hiyo ndiyo tu alitaka. Siku yake ya kuzaliwa ilipokaribia, mwanamke huyu alisubiri ishara kwamba mumewe alikuwa amenunua pete hile ya almasi.

Hatimaye, asubuhi ya siku yake ya kuzaliwa, mume wake alimwita kwa bashasha na katika hali ya kumpa habari njema. Mume wake alimwambia jinsi alivyokuwa akijivunia kuwa na mke mzuri kama huyo, na akamwambia jinsi alivyompenda. Akamkabidhi sanduku zuri la zawadi lililofungwa. Akiwa na hamu ya kutaka kujua, mke alifungua sanduku na kukuta Biblia ya kupendeza, iliyofungwa kwa ngozi, na jina la mke likiwa limepambwa kwa dhahabu. Kwa hasira, alipaza sauti yake kwa mume wake na kusema, "Kwa pesa zako na utajiri wako wote, unanipa Biblia?" na kutoka nje ya nyumba kwa mbwembwe na jaziba akimuacha mumewe chumbani na kuondoka kabisa eneo hilo.

Miaka mingi ilipita na mwanamke huyo alifanikiwa sana katika biashara. Aliweza kukaa kwenye nyumba nzuri zaidi na familia nzuri, lakini aligundua kuwa mume wake wa zamani alikuwa mzee sana, na akafikiria labda angeenda kumtembelea na kumsalimia. Hakuwa amemwona kwa miaka mingi. Lakini kabla hajafanya mipango, alipokea Ujumbe uliomwambia kwamba mume wake wa zamani alikuwa ameaga dunia, na wosia ukitaka kuwa urithi wote apewe huyo mwanamke. Alishangaa sana na ikabidi afanye kila liwezekanalo aende nyumbani kwa huyo mume wake wa zamani. Alipofika nyumbani kwa mume wake wa zamani, huzuni na majuto ya ghafla yalijaa moyoni mwake. Alianza kupekua karatasi muhimu za mume wake wa zamani na kuona Biblia ambayo bado ikiwa mpya, kama vile alivyoiacha miaka kadhaa iliyopita. Kwa machozi, alifungua Biblia na kuanza kufungua kurasa moja baada ya nyingine. Mume wake wa zamani alikuwa amesisitiza kwa uangalifu kwa kupigia mstari kwa rangi kifungu cha maneno

Mathayo 7:11, "Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba".

Alipokuwa akisoma maneno hayo, kifurushi kidogo kilianguka kutoka nyuma ya Biblia. Ilikuwa na pete ya almasi, na jina lake limechorwa juu yake - pete ile ile ya almasi ambayo aliiona kwenye chumba cha maonyesho, kwenye lebo ilikuwa tarehe ya kuzaliwa kwake, na maneno... "nakupenda daima". Alibubujikwa na machozi ya majuto kwa kushindwa kujua thamani yake kwa mumewe.


Ujumbe: Ni mara ngapi tunakosa baraka za Mungu, kwa sababu hazijafungwa kama tulivyotarajia?
 
Back
Top Bottom