Na wewe mtoa mada hujiamini. Unabadilisha Id then unaandika story ambayo unaamini kabisa msomaji akiisoma atajua ni wewe, hapa sijajua lengo lako la kubadiri ID.
Inaonekana kuwa your so desperate na marriage, kila mtu anapenda kuoa/kuolewa lakini usije ukaona kama ni laana kuchelewa kumpata mwenza. Na kwa stori yako inaonekana ulimruhusu aje ajitambulishe kwako huku hata kumjua vizuri bado.
Vijana tuweni makini, tuweni na subira tunavotaka kuingia kwenye stage ya kuoa/kuolewa, na wengi wanafanya hivyo hasa wakitamani tu siku ya kuvaa shera, suti na kukata keki.
Ushawahi kufikiria huyo mme/mke mwenye kazi yake nzuri, pesa mingi, na maisha mazuri akiugua miaka mitano kitandani kama utavumilia? na ndio maana wengi wamekuwa na Relationship/marriage za maigizo. But naamini bado kuna wanaume na wanawake ambao ni husband/wife material.