Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,081
- 464,063
Unateseka na nini etihivi kwanini jf hakuna sehemu yakurekodi japo sauti jaman,nateseka mimi nayangu moyoni

Khaaaaanimekosa wakugonga nae
Shemeji, muite basi Bishop akuje pande hizi🤣🤣🤣 arosto itatuua😱😱😱Khaaaaa
Bishop fanya ukuje basiShemeji, muite basi Bishop akuje pande hiziarosto itatuua😱😱😱
Shemeji, muite basi Bishop akuje pande hiziarosto itatuua😱😱😱
Eti arostoyaani kila saa narefresh tu.....Bishop fanya ukuje basi
Nice story............Taxi - (107)
“Wala siyo hivyo, ukweli ni kwamba mimi siyo polisi. I'm just concerned as a close friend... Nataka nionane na mdogo wako kwa kuamini kama kweli ana jambo analijua basi ataniambia, I know how to deal with...” Tunu alisema na kuachia tabasamu pana.
“Sina sababu ya kutokukuamini, hata hivyo, nimefurahi sana kukuona tena after so many years. Nimefurahi japo imekuwa ni kipindi kigumu na cha mshtuko mkubwa. Sikutegemea kabisa kama...” Sammy alisema kwa huzuni lakini akasita baada ya watu watatu kufika.
Walikuwa wanawake wawili na mwanamume mmoja, jirani zao kule Tabata Chang’ombe, waliopita kumjulia hali Joyce.
* * * * *
Saa nne kamili asubuhi, katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, magurudumu ya ndege aina ya Bombardier DASH8 Q400 ya shirika la ndege la Tanzania yaligusa ardhi kwenye kiwanja hicho huku tayari abiria wakiwa wamejiandaa kwa tukio lile la kutua kwa ndege. Ndege hiyo ilikuwa inatokea jijini Tanga.
Muda mfupi baada ya ndege ile kusimama, milango ya ndege ilifunguliwa na hapo abiria wakaanza kushuka. Kati ya abiria hao walikuwepo abiria wawili mume na mke waliokuwa na sura zilizosawajika zikiwa na huzuni isiyoelezeka. Hawa walikuwa ni Rafael Jengo na Bi. Pamela Jengo, wazazi wa Joyce.
Rafael Jengo alikuwa mrefu mwenye sura ya ucheshi na umbo kubwa lililopendeza. Alikuwa amevaa suti nadhifu ya rangi ya kijivu na shati jeusi lililomkaa vyema na kumpendeza. Miguuni alikuwa amevaa viatu vyeusi vya ngozi na mkono wake wa kushoto alivaa saa nzuri ya mkononi. Umri wa Rafael Jengo wa miaka hamsini na nne bado ulikuwa haujatosha kabisa kuzipokonya nguvu zake mwilini.
Bi. Pamela alikuwa mnene wa wastani, hakuwa mfupi wala mrefu bali alikuwa na kimo cha wastani na alikuwa mweupe. Alikuwa na umri wa miaka arobaini na nane. Wakati wanashuka toka kwenye ndege Rafael Jengo alikuwa akimtazama mkewe Bi. Pamela akiwa na uso uliosawajika kidogo pasipo kusema neno lolote huku akionekana kuipa utulivu akili yake.
Mara waliposhuka kwenye ile ndege wakaingia kwenye jengo namba mbili la kiwanja kile cha ndege cha kimataifa lenye migahawa ya kisasa na ofisi mbalimbali za utawala. Kwa kuwa hawakuwa na mizigo yoyote mikubwa waliwatangulia abiria wengine wenye mizigo wakapenya haraka na kutoka nje ya jengo la kiwanja kile cha ndege cha kimataifa.
Dereva mmoja wa teksi mjanja akawawahi haraka kabla ya wenzake baada ya kuhisi hitaji lao. Dereva yule alikuwa mzee wa makamo, mrefu na mwembamba mwenye sura ya ucheshi akiwa amevaa kofia nyeusi ya kapelo, shati jeupe, suruali ya nyeusi na makubasi ya ngozi miguuni, aliwahi kuwapokea mizigo waliyokuja nayo na kuwafungulia mlango wa taxi yake hata kabla hawajaafikiana naye au kumweleza hitaji lao. Kwa ushawishi ule hawakuwa na pingamizi, hivyo wakaingia ndani ya gari.
Mara tu walipoingia ndani ya ile taxi yule dereva akawatazama kwa makini huku akiachia tabasamu la kirafiki. “Sijui niwapeleke wapi, ndugu zangu?” yule dereva taxi aliwauliza huku tabasamu la kindugu likiendelea kutawala usoni kwake.
“Tupeleke Amana,” Rafael Jengo alisema, na muda huo huo ile taxi ikaondoka na kuanza kuyaacha maegesho ya magari ya kile kiwanja cha ndege, kisha ikaingia katika barabara ya Nyerere na safari ya kuelekea Amana ikaanza.
* * * * *
Kwenye viunga vya maegesho vya hospitali ya Amana, Tunu alikuwa ameketi kwa utulivu ndani ya gari dogo la kifahari aina ya BMW X6 xDrive 50i jeusi alilokuja nalo. Gari lile lilikuwa haliungurumi. Alikuwa nyuma ya usukani wake akionekana kutafakari sana juu ya kazi iliyokuwa mbele yake. Alikuwa analitazama kwa makini gari la Sammy aina ya Cadillac DeVille.
Alikuwa na mambo kadhaa ya kuyashughulikia na hakujua angeanza na lipi, hata hivyo alikuwa amepata mahali pazuri pa kuanzia baada ya mazungumzo yake na Sammy, mwanamume aliyemwondolea utoto wake na kumwingiza katika dunia ya watu wazima.
Hakutegemea kabisa kukutana na Sammy katika mazingira yale ya utata. Alijihisi alikuwa na jukumu la kumsaidia Sammy kama njia ya kudumisha uhusiano wao uliopotea kwa takriban miaka kumi na moja. Siyo Sammy aliyekuwa ameathirika na kupotezana kwao, hata yeye pia alikuwa katika wakati mgumu, alishindwa kabisa kumtoa Sammy moyoni mwake.
Aliikumbuka vyema siku aliyokwenda nyumbani kwa Sammy, yale waliyoyafanya na ahadi walizopeana baada ya hapo, na wakati akiondoka hakujua kama wasingeonana tena kwani aliporudi nyumbani kwa shangazi yake huko Sinza alikuta taarifa za kifo cha baba yake aliyekuwa mwanasiasa maarufu mjini Tabora. Alitakiwa kusafiri kwenda Tabora asubuhi ya siku iliyofuata na hakuweza tena kuwasiliana na Sammy kwani hakuwa amechukua namba yake ya simu.
Tunu alikuwa amezaliwa mkoani Tabora akiwa mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne, yeye akiwa mtoto pekee wa kike. Baada ya mazishi hakurudi jijini Dar es Salaam, alibaki Tabora kumsaidia mama yake hadi matokeo ya mtihani wake wa kidato cha sita yalipotoka ambapo Tunu alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kitaifa, na hivyo kupata udhamini wa kusomeshwa bure chuo kikuu.
Siku alipofika jijini Dar es Salaam alimtafuta Sammy bila mafanikio, nyumba aliyokuwa akiishi alikuwa amehama na hakuna aliyejua alihamia wapi. Baada ya kuhangaika kumtafuta kila alikodhani angemwona hatimaye Tunu alikata tamaa ya kumpata, kwani pia alikuwa na muda mfupi sana wa kujiandaa kabla ya safari.
Muda ulipofika aliondoka kwenda masomoni nchini Marekani katika Taasisi ya Teknolojia ya Georgia (Georgia Tech). Huko Marekani Tunu alisoma kwa miaka minne akibobea na kuhitimu Shahada ya Kwanza katika Computer System Analysis.
Aliporudi nchini alichaguliwa kujiunga na programu maalumu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya vijana wasomi walioandaliwa kwenda kuchukua mafunzo ya awali ya ujasusi. Baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi Tunu alilitumikia jeshi kwa muda mfupi na kituo chake kilikuwa Lugalo jijini Dar es Salaam.
Inaendelea...
Taxi - (107)

Aliporudi nchini alichaguliwa kujiunga na programu maalumu ya Jeshi la Wananchi wae Tanzania kwa ajili ya vijana wasomi walioandaliwa kwenda kuchukua mafunzo ya awali ya ujasusi. Baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi Tunu alilitumikia jeshi kwa muda mfupi na kituo chake kilikuwa Lugalo jijini Dar es Salaam.
Inaendelea...

usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua hadi mwisho...