Natamani na kusubiri kuona siku ambayo tutapata viongozi wenye uchungu hasa na nchi yetu wakiwapanga foleni wahujumu wote wa uchumi wetu regardless wana umri gani, ikiwezekana na wanafamilia wao waliohusika, na kuwapiga risasi hadharani."Rais mla rushwa kamwe hawezi kupambana na rushwa" (- Mwl. JK Nyerere) Hebu tukumbushane ni nani aliyekuwa waziri wa nishati na madini mwaka 1994 wakati kina Chenge wakituingiza mkenge wa IPPTL? Kama nadharia hiyo ya Nyerere ni ya kweli basi tujue tumekwisha! Kelele zote kuhusu rushwa na ufisadi unaofanywa na Kikwete na wenzake leo ni za kisanii zisizo na hata chembe ya dhati kwani hata yeye katika ngazi za chini alihusika katika mikataba kama hii ya wenzake leo. Mkataba wa IPPTL uliojaa vipengelevya dhuluma na kuipora Tanzania mamilioni ya walalahoi ulisainiwa na mafisadi ambao ndiyo wakubwa wa serikali leo hii Kikwete akiwemo! Hapa nataka kupinga dhana ya "Kikwete himself has been misled into thinking that this project is too big and too costly, hence it would take too long to build the power plant. The president has now falsely given up hope of implementing this project during his ten-year rule."
Ndiyo tuseme si sahihi kusema Kikwete anapotoshwa au amepotoshwa na washauri wake wa karibu kwa vile hata yeye mwenyewe anaufahamu mchezo unavyofanyika. Ila iko siku yote yaliyofanywa na yanayofanywa gizani kulihujumu taifa letu tukufu yatawekwa hadharani na historia itawahukumu. Mungu ibariki Tanzania.
Natamani na kusubiri kuona siku ambayo tutapata viongozi wenye uchungu hasa na nchi yetu wakiwapanga foleni wahujumu wote wa uchumi wetu regardless wana umri gani, ikiwezekana na wanafamilia wao waliohusika, na kuwapiga risasi hadharani.
Nimekuwa nawafundisha wanangu kuwachukia mafisadi na wahujumu uchumi na ninataka kuwafundisha sasa kwamba ikitokea wakawa wakuu wa nchi hii wasisahau kuwapa adhabu za vifo watu hawa. Hili linawezekana na litakomesha mchezo huu. Ngoja niwatayarishe wanangu kuwa viongozi.
Walisema he was late for being briefed na balozi wetu maana hata baadhi ya watu kwenye msafara walianza kelele kwamba mbona imechukua muda.Chini watanzania waliokuja kumpongeza walikuwa wanalia tu na wachache walikuwa na maswali hao waliwaka kweli wakitaka aje waanze kusogoa ilishazidi muda.JK hakuwa na ratiba ya kuonana na Watanzania wale ila walijitokeza wenyewe baada ya kusikia
Nchi ya wasanii mpaka mabalozi wasanii. Si wanapeana hapa ubalozi kama zawadi au kama retirement benefit kwa walioshindwa chaguzi?"Raisi wetu JK anawasili leo saa 21:30 usiku kwaajili ya maadhimisho ya Siku ya maendeleo ya jumuiya za ulaya"...Watanzania Wote tumeombwa twende kuonana na Raisi hotelini kwake saa nne usiku.....! Hiyo ndo taarifa tuliyokua tumetangaziwa na balozi wetu.
Adui mkubwa wa maendeleo ya Afrika ni viongozi wetu. Nafikiri sasa inabidi tufike mahali tuanze kuandamana mitaani na mabango ya kulaani uhuni huu wa viongozi wetu pale unapokuwa umebainishwa. Tumechoka sasa na huu wizi na hujuma ya uchumi wetu na maendeleo ya watanzania kwa ujumla.
Kama sikosei mwaka jana Wachina walishatua TZ wakiwa full nondo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya mradi huo kwa gharama zao wakapigwa stop. Huwezi kuamini.
Ratiba ilisema kiongozi wa nchi atawasili hotelini saa nne kamili usiku, ataenda chumbani kwake then in 5 min atashuka chini kuongea na Watanzania...watu wakafika hotelini na kugandishwa hadi saa tano na nusu..alipofika yeye na mkewe akawap watu mikono na musala "Asante kwa kutukRibisha" then huyo shaaa chumbani, kwani... tulimuona tena??kuuliza tukaambiwa kasema hashuki chini tena...hayo si ni madharau?
Huyu ndo Raisi anejali Uzalendo kweli?
Nadhani pia alimiss mbaya trip za kiwanja ngoja utamsikia anatia tim US muda si mrefu. Gharama zake watanzania watabeba tu ni watu wa AMANI na UKARIMU ULIOTUKUKA.
It wounds my heart to find tanzanian behaving like non Tanzanian. Ill advising president for personal interest is not acceptable and if revealed those responsible should face a death penalt.
Kumbe tunateseka na joto lote hili na giza nene la mgao wa umeme kutokana na kazi ya mafisadi na viongozi wala rushwa? Wallahi nchi hii itakuwa masikini milele...
Come on... Wote tulimsikiliza huyo msanii jinsi alivyoonesha kuwa ni mradi ambao utatumia miaka mingi sana kukamilika. Sasa ukisoma hiyo habari ya This Day (sijui kama umeisoma kabla ya kuchangia?!) utagundua kwamba kumbe mradi unakuwa sabotaged tu na mafisadi. Otherwise ni mradi ambao ulipaswa kutekelezwa siku nyingi sana, na huu upuuzi wa mgao wa umeme ungeshakuwa historia -- kwamba hapo zamani za kale Tanzania kulikuwa na tatizo la umeme na watu wake walilazimika kukaa gizani kwa masaa mengi kutokana na ujinga na usanii wa viongozi wao.
Kikwete mbona kishaitangaza hiyo project kuwa ataianza hivi karibuni. Hizi habari zingine ni pumba tu.
Au hamkusikiliza hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la kumi?