Wapendwa ni aje...!! ujio huwa ni wa mawazo na kuwazua, kupimia upepo na kuchukua hatua stahiki, usiende kichwakichwa yakakufika ya kukufika ati,,, katika kupitiapitia jukwaani hapa nimebaini mambo mbalimbali kwa wanajamvi espeshale baada ya kuanza mwaka huu... , zifuatazo ni dondoo za mwelekeo wa wanajamvi kwa mwaka huu....
i. Mwaka huu kimsingi umeanza kwa kugubikwa na wingu baya la kusambaratika na kutetereka kwa mahusiano na ndoa za watu, tulivyoingia tu tukashuhudia
nitonye akimmimina
sweetlady kama maji machafu kisa eti bibie hatulii na amekuza kiwango ati anaweza akawamudu wachezaji idadi yoyote kwa wakati wowote, katika hili majina kama
Mr Rocky na
Vin Diesel yalisikika mara kwa mara.
ii. Tulishuhudia pia
Arushaone aki bip kwa
Mamzalendo kama kawaida yake katoka nduki kama alivyofanya kwa
Mamndenyi . Kampotezea
Mamzalendo kimyakimya ilhali nia alitangaza hadharani hapa, wakati huohuo tumeshuhudia kijana wa Jf Arusha wing
Filipo akipagawa ghafla kama katiwa ndimu baada ya safari ya Tanga, kinywani muda wote ni
Arabela jambo lililomfanya
zubedayo_michuzi anyong'onyee na kwa upande wa pili niseme tu ndoa ya
Filipo kwa
marejesho imeshikiliwa na uvumilivu na busara za
marejesho , otherwise....!!!
Mwaka huu umeshuhudia kuibuka kwa vijana machachari kama
Vin Diesel ambaye asione jinsia ya Eva mbele yake anatangaza ndoa bila kujali ni mke wa mtu, mchumba au under 18,,
Pia ttumeshuhudia kijana
Slave akijifunga pingu na
Evelyn Salt licha ya zengwe lililoanzishwa na
Globu.
Hali kadhalika jukwaa limeshuhudia kuadimika Cc kwa watu kama
Erickb52,
Dena Amsi,
Mtambuzi,
Ronn M na mkewe
jeneneke hivyo kuwa miss sana,
Mwenyekiti wa tume ameurahishwa na ndoa moja ya mfano na familia iliyotulia ya
watu8 na
measkron pamoja na watoto wao, hii ndoa imekuwa ya mfano.
Hali kadhalika tumeshuhudia ndoa kati ya
C6 na
charminglady ,
Chimbuvu na
Madame B na
Bishanga na
The secretary zikiwa katika dhoruba kali kiasi kwamba zinategemewa busara za mwenyekiti kuokoa jahazi.
Kubwa kuliko zote ilikuwa ni kuibuka kwa kundi la VIRUSI au masalia waliokuwa wanatumwa kuja kuchafua hali ya hewa hapa ndani na kuwasababishia members ban za mara kwa mara, hiyo ikapelekea kuumbuliwa kwa kaka
Marry Hunbig a.k.a
mzungu mndali ambaye alitumia jinsia ya bandia akataka kumuingiza mkenge
stevoh kabla hatujamstukia na kumuumbua, Kimsingi jukwaa linazidi kupendeza na kuwa na members wengi zaidi
Huku ndo chit chat hatuulizani dini, kabila, itikadi ya kisiasa wala elimu ya mtu.
Napenda kukaribisha maombi ya wote wanaotaka kurasmisha mahusiano yao walete mpango mkakati wao kwangu ili niweze kuufanyia upembuzi yakinifu kabla sijaruhusu kikosi kazi kuanza mchakato wa utekelezaji.
We miss you
Ruhazwe JR,
The Boss,
Judgement,
Ciello,
cacico,
BAK (mutu ya burudani),
pombekali ,
Mentor et al
CHIT CHAT MUCH FUN MUCH LOVE
Copy:
Asprin , kasi ya ukaguzi imepungua sana ndo maana tunasumbuliwa na watu kama
Marry Hunbig Mndali