Freeland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 14,481
- 10,233
Tenga amedumu miaka tisa kwenye uongozi, ulitaka akae miaka mingapi zaidi ndio atufikishe huko mbali?
MIAKA TISA kwenye uongozi, nini kikubwa alichokifanya cha kujivunia? Katika muda huo Taifa Stars ilishindwa kufuzu AFCON tano, 2006, 2008, 2010,2012, 2013.
Hakuna timu ya vijana iliyofuzu michuano ya Afrika ambayo tungesema ni mtaji wa badaae.
Muda wa miaka Tisa ulitosha kuandaa timu ya vijana ambayo tungekuwa tunaitarajia kufuzu AFCON kwa sasa.
Timu ya taifa iliweza angalau kuwa inapata ushindi katika kipindi cha Tenga.
Tenga amejenga nidhamu ya taasisi ya TFF ...Kumbuka enzi za FAT ya kina ndolanga...
Tenga ndiye aliyeanzisha ligi kuu inayoeleweka na kuweza kuvutia wadhamini wa kutosha kwenye ligi kuu....
Timu ilivyokua inaenda kwa kipindi cha paulsein na tenga ilianza kuwa timu inayoaminika...kwamba unaweza ukaiamini stars itashinda....
Chini ya huyu mtu hovyo kuwahi kutokea katika soka Jamal Malinzi kuna kipi kipya? au Jezi?
Last edited by a moderator: