Stars yatoka sare Swaziland

mwacheni77

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
763
209
Mwenye taarifa za mchezo tunaomba watujuze tujue chama letu limefanya nn leo
pelegrinius-rutahyuga_300_175.jpg

Mshauri wa masuala ya kiufundi wa Rais wa TFF, Jamali Malinzi, Pelegrinius Rutahyuga.

TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars jana ilitoka sare bao ya 1-1 dhidi ya wenyeji wao Swaziland katika mechi iliyochezwa mjini Mbabane. Mechi hiyo ilikuwa ya kimataifa ya kirafiki inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Kabla ya kwenda Mbabane, Stars ikiwa na wachezaji 20 iliweka kambi ya siku tatu Johannesburg, Afrika Kusini. Habari kutoka Mbabane zinasema mchezo ulikuwa mkali, lakini mwamuzi anadaiwa kuiuma Taifa Stars.

"Mchzeo ulikuwa mzuri, huku Swaziland hali ya hewa ilikuwa baridi kali sana, vijana walijitahidi sana, lakini kuna mambo mengine sio ya kulalamikia, waamuzi hawakuchezesha kwa haki hata kidogo, alitunyima penalti ya wazi kabisa na alitoa kadi za njano nyingi upande wetu bila mpangilio," alisema mshauri wa masuala ya kiufundi wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamali Malinzi, Pelegrinius Rutahyuga.

Rutahyuga alisema bao la Stars lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa anayecheza soka ya kulipwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Thomas Ulimwengu.

Rutahyuga alisema Stars inatarajiwa kurejea nchini leo kujiandaa na ratiba nyingine.

Wachezaji waliokwenda Mbabane chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij ni Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wanaocheza TP Mazembe, Mwinyi Kazimoto anayecheza soka ya kulipwa Qatar na Juma Lazio anayechezea Zesco ya Zambia.

Wengine ni nahodha Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Deogratius Munishi.

Aidha wengine ni Aishi Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Himid Mao, Emmanuel Simwanda, Salum Abubakari, Saidi Ndemla, Haruna Chanongo, Simon Msuva, Abubakar Mtiro, Hassan Isihaka, Erasto Nyoni na Salim Mbonde.

Chanzo:Habari Leo
 
Jamal Malinzi

Hivi huyu anaweza kweli kuliinuwa soka la Tanzania? I doubt.


cc Bishanga
Bishanga hana uwezo wowote wa kuinua soka letu...Ni mwanasiasa asiyejua lolote...I said tangu mwanzo kwa malinzi soka letu litazidi kudididimia.....

Tunahitaji watu wa Calliber ya Tenga...huyo jamaa angetufikisha mbali

Katika mambo ya kipuuzi zaidi kufanywa na malinzi ni kumtimua kocha Poulsein....Yule kocha alikuwa anaenda vizuri...alianza na timu ya vijana...ameonesha progress nzuri sana ya soka letu....Malinzi ni Janga la mpira Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Bishanga hana uwezo wowote wa kuinua soka letu...Ni mwanasiasa asiyejua lolote...I said tangu mwanzo kwa malinzi soka letu litazidi kudididimia.....

Tunahitaji watu wa Calliber ya Tenga...huyo jamaa angetufikisha mbali

Katika mambo ya kipuuzi zaidi kufanywa na malinzi ni kumtimua kocha Poulsein....Yule kocha alikuwa anaenda vizuri...alianza na timu ya vijana...ameonesha progress nzuri sana ya soka letu....Malinzi ni Janga la mpira Tanzania

Tenga amedumu miaka tisa kwenye uongozi, ulitaka akae miaka mingapi zaidi ndio atufikishe huko mbali?
MIAKA TISA kwenye uongozi, nini kikubwa alichokifanya cha kujivunia? Katika muda huo Taifa Stars ilishindwa kufuzu AFCON tano, 2006, 2008, 2010,2012, 2013.

Hakuna timu ya vijana iliyofuzu michuano ya Afrika ambayo tungesema ni mtaji wa badaae.

Muda wa miaka Tisa ulitosha kuandaa timu ya vijana ambayo tungekuwa tunaitarajia kufuzu AFCON kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom