Edo Kumwembe: Kwa Fei Toto wa Stars wote tumevuna tulichopanda

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
428
996
MECHI mbili zilizopita za Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alianzia benchi. Ilianzia pale Ismailia, Misri na Stars ilishinda na ikajirudia hapa Dar es Salaam, Stars iliondoka kichwa chini. Hakuna aliyeshangaa Fei kuwekwa benchi na Adel Amrouche, kocha mpya wa Stars.

Watanzania wa leo wana uelewa wa mpira. Wala hawajamlaumu kocha kumweka nje Fei katika mechi zote mbili. Wanajua Fei hayupo fiti. Alisimama kucheza ligi tangu mwaka jana na hizi mechi zimewakuta wachezaji wengi duniani wakitandaza soka katika ligi mbalimbali. Fei alikuwa amekaa zake Forodhani akila pweza.

Mazoezi ya kukimbia hapa na pale Zanzibar ni tofauti na kucheza mechi za kishindani. Hata kama tunaamini ligi yetu ina walakini lakini bado inamsaidia mchezaji kuwa fiti kama tulivyoona kwa wachezaji wa ligi yetu wakipambana na Uganda katika mechi mbili zilizopita.

Nilikuwepo kule Ismailia na kocha wa viungo wa Taifa Stars alilazimika kumpa mazoezi ya kipekee Fei ili aweze kuzikabili mechi mbili zilizokuwepo usoni mwake. Baadaye Fei alijikuta katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku akifanya mazoezi ya kipekee baada ya kugundulika yuko nyuma ya wenzake kwa suala la utimamu wa kimwili.

Ni mechi hizi mbili ambazo tulilazimika kucheza na viungo watatu ambao kiasili ni wachezaji tofauti na Fei. Mudathir Yahaya, Mzamiru Yassin na Himid Mao wote ni wazee wa kugongana. Wote sio mafundi sana katika kuunganisha timu eneo la mbele na ikiwezekana kufunga. Hii ilimwacha Fei akiwa kiungo wa kipekee kati yao.

Kama Fei angekuwa fiti basi mmoja kati yao angechomolewa na Fei angekwenda kucheza mbele kati ya wawili. Nani amesahau namna ambavyo Fei amefunga mabao akiwa na jezi ya Yanga miezi ya karibuni? Ni kwa sababu amefurahia kuicheza nafasi hiyo tangu kocha wake wa Yanga, Nasireddine Nabi amsogeze mbele. Zamani makocha walikuwa wanampotezea muda kumpanga eneo la nyuma.

Baada ya kukaa nje katika mechi mbili dhidi ya Uganda, Watanzania tumeanza kutazamana kwa aibu. Wakati ule sakata lake lilipoanza hatukujua kama kuna siku wote tungemhitaji Fei kwa pamoja. Tulidhani ni Yanga peke yao ambao wangemhitaji. Leo wote tumegundua ilikuwa hasara kwa Fei kukaa nje kwa muda mrefu kwa masilahi ya taifa zima.

Haishangazi kuona ndio maana FIFA wanataka mchezaji acheze soka uwanjani. Mchezaji anaweza kuwa na matatizo na klabu yake lakini FIFA wanamtaka acheze soka. Hasara ya Fei kukaa nje tumeiona katika mechi mbili zilizopita na sasa ni muda wa kutazamana usoni na kuulizana nani alisababisha hali hii na bahati mbaya zaidi hatujui itaendelea mpaka lini.

Upande wa kwanza kuna wale ambao inasemekana wako nyuma ya dili zima la Fei kuondoka Yanga. Sijui wamejisikiaje. Inawezekana wanamlipa mchezaji mshahara na katika masuala ya kipesa Fei akawa hana matatizo lakini tumeshuhudia hasara ambayo Taifa limepata kwa Fei kukaa nje katika mechi mbili zilizopita.

Kuna mashabiki wa timu nyingine ambao walikuwa wanashangilia Fei kuisusia Yanga. Kwa masilahi yao walikuwa sahihi lakini ghafla wamejikuta kuwa na wao ni Watanzania na walimhitaji Fei awe fiti katika mechi zote mbili hizi. Wamepigwa na butwaa kuona mchezaji hayupo fiti kuitumikia timu ya taifa.

Ni katika nyakati kama hizi za mechi za kimataifa ndio huwa tunaweka kando klabu zetu na kujikumbuka wote sisi ni Watanzania. Hiki ndicho ambacho kimewatokea mashabiki wa soka nchini ambao waliweka mbele masilahi ya klabu zao kuliko ya taifa.

Mechi hizi mbili zilizopita kuna mahala Watanzania waliungana. Kuna mashabiki wa Yanga walitaka Shomari Kapombe na Mohammed Hussein Tshabalala waitwe timu ya taifa. Na kuna mashabiki wa Simba walitaka Fei apewe mikoba yake. Tulisahau tofauti zetu. Hata hivyo, kwa suala la Fei ndipo tulipokumbuka tumejikwaa.

Lakini tatu suala zima limemkumbusha mchezaji mwenyewe umuhimu wa kucheza soka la kishindani kila wikiendi. Nadhani kwa kiasi fulani Fei atakuwa amefedheheka kwa kuanzia benchi katika mechi mbili zilizopita za Taifa Stars. Anajua kama angekuwa katika utimamu wa mwili basi hakuna kocha ambaye angemweka benchi pale Stars.

Kama ana uzalendo na nchi yake nadhani atakuwa amefadhaika kutotoa msaada ambao najua anajua angeweza kuutoa kwa timu. Kuna vitu vingi aliviona akiwa katika benchi lakini hakuna ambacho angeweza kufanya. Zaidi wachezaji mbalimbali mahiri duniani walikuwa viwanjani kuwakilisha mataifa yao.

Hii imenikumbusha msimamo wangu kuhusu sakata la Fei. Ninaamini katika vitu viwili. Naamini kwa mchezaji kuleta vurugu kama hizi za kimkataba mwisho wa msimu. Awe na haki au asiwe na haki sikuona umuhimu wa Fei kujaribu kukatisha mkataba wake katikati ya msimu. Alipaswa kusubiri mpaka mwisho wa msimu.

Sidhani kama hata Fifa wataafikiana na mchezaji wa aina yake hasa ukizingatia Yanga alikuwa anapangwa kila wikiendi na alikuwa analipwa stahiki zake zote. Kama haya yangekuwa hayafanyiki nadhani Fei angekuwa na wakati mzuri wa kushinda kesi yake. Kwa hali ilivyo sasa sidhani kama Fei atafanikiwa katika shauri lake.

Msimamo wangu wa pili ulikuwa ni kumtaka Fei atiririshe mkataba wake Yanga mpaka mwishoni mwa msimu ujao. Msimu wa soka una miezi michache. Wachezaji hucheza kwa miezi tisa tu.

Jaribu kuangalia, kuanzia pale Fei alipogoma mpaka leo tayari ligi imebakiza mwezi mmoja tu kumalizika. Msimu ujao angerudi Agosti mpaka Mei. Ni miezi michache tu mkataba unakuwa umeisha. Angekuwa mchezaji huru.

Ni hapo ndipo angepata pesa nyingi zaidi kwa sababu angeziingiza vitani klabu zote kubwa nchini kuwania saini yake. Hata klabu yake ingejikuta ikiingia katika vita kubwa ya kujaribu kumbakisha kwa kiwango kikubwa cha pesa.

Badala yake washauri wake au warubuni wake walimtaka aondoke katikati ya msimu kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kimegharimu maisha ya Taifa Stars kufuzu kwenda Afcon mwakani pale Ivory Coast.

Fei kama angeendelea kucheza Ligi au michuano ya Shirikisho nina uhakika angetusaidia. Fei kama angecheza mechi hizi sita za kombe la Shirikisho katika kundi ambalo Yanga walipangwa na TP Mazembe, Monastir na Real Bamako nina uhakika kwa kiasi kikubwa angetusaidia.

Ni mechi hizi ndizo ambazo zimesabababisha akina Enock Inonga, Clatous Chama, Fiston Mayele na Kennedy Musonda waitwe katika timu zao za taifa.

Kinachosikitisha ni kwamba hatujui Fei atakuwa nje mpaka lini. Wakati huu wenzake wameachana na timu zao za taifa na kurudi katika klabu zao hatujui Fei yuko wapi.

Jana alipaswa kucheza pambano lake la sita la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe lakini sasa hivi huenda yupo Zanzibar anapiga stori na washkaji zake.Ni jambo linalosikitisha.

Mwanaspoti
 
fei abadilishe wakala/manager, mambo ya kusema mama yangu ndo meneja wangu au mtu mjuaju juaji ila hana taaluma, yamepitwa na wakati, wachezaji wawe na team itayokuwa inashughulikia maslahi yao, wao wawe bize na mpira tu.
 
Eti huyu nae mwandishi wa habari daah nchi imechakaa sana
 
Una kisa nae si buree!!! Kwanini lakini umejaaliwa roho mbaya,,,punguza kaka si nzuri sana kiafya,,,Haswa afya ya akili na nafsi!!!!
sikatai hayo maoni yako kama ilivyo kwangu ni mtanzuko tu
 
Eti huyu nae mwandishi wa habari daah nchi imechakaa sana
acha roho ya korosho ndugu,alichokiandika ni lugha rahisi na imeeleweka, mambo ya marythm mtaambizana hukooo kny vikao vyenu vya waandishi,,,sie wakulima hatuhitaji misamiati....
 
Fei wa Taifa stars hata alipokuwa Yanga kikosini,hakuwa na maajabu Taifa stars.
 
Wechezaji wazawa wenye akili kama huyu ni wachache sana, mkataba unakaribia kufikia ukingoni Menejimenti ya mchezaji wamekaa mezani na Timu wamekubaliana na kuongeza mkataba na si kama yule Zuwena kukimbia kambi na kuanza kupiga kelele kama waimba taarab!

Similar Discussions

Back
Top Bottom