Taifa Stars yatua salama yapokelewa kwa shangwe na mashabiki

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) imetua salama alfajiri ya Septemba 9, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea nchini Algeria kwenye mchezo wa wa kufuzu mashindano ya AFCON 2023 yatakayochezwa mapema mwakani 2024 nchini Ivory Coast.

Katika mchezo huo uliochezwa Septemba 7, 2023, Tanzania na Algeria zilitoka zilitoka sare ya bila kufungana (0-0), matokeo ambayo yanazifanya timu hizo kufuzu michuano hiyo, huku Tanzania ikifuzu kwa mara ya tatu katika historia ya mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutua jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo kwa niaba ya Serikali, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maono yake kwenye sekta ya michezo, hamasa pamoja na kuunga mkono timu hiyo.

Aidha, amewashukuru Watanzania wote kwa sala, dua na maombi yao na kuiunga mkono timu yao ya Taifa na kusisitiza kutakuwa na utaratibu mzuri kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) hatua itakayowezesha mashabiki waende kwa wingi nchini Ivory Coast mwakani 2024 kwenye michuano hiyo ili kuendelea kupeperusha vyema bendera ya taifa.

"Wizara yetu ambayo inaongozwa na Waziri Mhe. Dkt Damas Ndumbaro itaendelea kuyaishi maono ya Mheshimiwa Rais katika kuiendeleza wa timu ya Taifa na sasa ufadhili na uangalizi utaongezeka zaidi ili Ivory Coast tukafanye vizuri zaidi" amesema Katibu Mkuu Bw. Yakubu.

View attachment 2743865View attachment 2743866View attachment 2743868View attachment 2743867

IMG-20230909-WA0007.jpg
 
Ila kuna watu wana muda wa mchezo. Yaani unatoka Kawe hadi Airport kuwashangilia hao kisha unarudi Kawe.
 
Sasa kuna watu wanaleta siasa kwenye michezo,

Watu wanafuatilia siasa huwa wanajiona kama wao ndo wana mchango mkuuuubwa kwenye maendeleo ya hii nchi 😂😂😂 kumbe hamna kitu aiseeeb

Btw, Pongezi nyingi sana kwa Taifa Stars, tuanze mipango ya AFCON sasa
 
Msiihusishe Timu yetu ya Taifa na mambo ya kisiasa yanayoendelea sasa hivi Nchini.

Taifa Stars umefuzu nimefurahi sana ushauri wangu ni wakifika wasiwe tena kichwa cha mwendawazimu.

Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki TANZANIA.
Kati yako na Mm, nan ameleta siasa
 
Tena kuna WanaCCM wengi ambao hawamtaki huyu Mama kwasababu "tu" wanasema She's too soft kwa Wapinzani wanataka Mtawala mwingine Authoritarian kama Magufuli ili aushughulikie Upinzani.

Sio kwamba hatusomi Magrupu yenu.

TAIFA STARZ haina Chama ni ya Wananchi.
 
Wakija kupigwa 9 huko kwenye fainali za AFCON mje tena hapa hapa muisifie CCM na huyo mwenyekiti wenu.
 
Back
Top Bottom