radiation
JF-Expert Member
- May 28, 2013
- 241
- 254
kutokana na kuamriwa na mamlaka ya mawasiliano TCRA star tv wameamua kurudi rasmi na kuendelea kurusha matangazo yao kupitia startimes.
====================
Ufafanuzi toka Star TV
====================
======================
Ufafanuzi toka Star Times
======================
====================
Ufafanuzi toka Star TV
====================
Mkuu,
Tunaonekana kwenye Star Times kutokana na makubaliano na mazungumzo yanayoendelea ili kuwa na maslahi kwa wote kibiashara na kwa ajili ya kutoa huduma ya habari na burudani kwa jamii, na si vinginevyo.
Asante.
Tunapenda kuwashauri wapenzi wa Star TV wenye ving'amuzi vya Star Times wa-"scan" upya ving'amuzi vyao ili waweze kupata matangazo yetu. Asanteni.
======================
Ufafanuzi toka Star Times
======================
Habari yenu wana jamii forum
tunapenda kuwajulisha wateja wetu kuwa kwa sasa Chanel ya Startv imerudi hewani na inapatikana bure kabisa kama ilivyokuwa awali, wateja wetu wataendelea kuiangalia chanel hii pamoja na zingine tano, (ITV, EATV, CLAUDS TV kwa dar, CHANEL TEN) Bure hata muda wao wa hewani utakapokuwa umemalizika
tunapenda kuwashukuru kwa uvumilivu wateja wetu wote na tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa kuna changamoto nyingi sana, lakini tunajitahidi sana kuweza kutatua matatizo madogo madogo kwa wateja wetu. Tunashauri kama mteja wetu atakuwa na tatizo lolote ni vema akatoa taarifa na sio kukaa kimya kwani kukaa na tatizo kisha kulalamika sio kutatua tatizo. Tuna timu ya mafundi 100 ambao wanazunguka mitaani kutoa misaada bure kabisa ya kiufundi.
tafadhari kama kuna yeyote mwenyetatizo anaweza kututumia namba yake ya simu katika inbox yetu
tunashukuru sana