asante sana kwa taarifa mkuu
Hongera kwa kusikiliza kilio cha wateja wenu!
StarTimes Tanzania hongereni kwa kumaliza tofauti baina yenu na Star TV kwa kuzingatia mahitaji ya walaji.<br />By majid musisi<br />
Hongera kwa kusikiliza kilio cha wateja wenu!
<br />
tunashukuru kwa uvumilivu wenu pia
Afadhali upo hapa leo mkuu!! Kuna kitu kinatuumiza sana tunapotumia huduma yenu, stuck,stuck,stuck!! Pili wateja wenu(nikiwemo)wanalalamikia kuuziwa channel ambazo ni free to air,kama KBC,UBC,CITIZEN nk,hamuoni kuwa soko lenu lipo mashakani kufuatia kuibuka kwa kampuni kama Digitech na continental ambazo zinajiainisha kuwa zinaonyesha channel hadi 60 bila malipo ya mwezi? Tatu, kulipia vingamuzi vyenu kwa njia ya Mpesa,tigopesa,na airtel money imekuwa shughuli ngumu kidogo,kila mara unaambiwa kuna tatizo la kiufundi!! Tatizo gani hilo lisilo tatulika? Haya ya Tv station kulalamikia malipo tuwaachie wenyewe,japo pia inatutia mashaka kama kesho tutazikuta channel tunazozipenda kwenye kingamuzi chenu!!wanaweza kujitoa wakati wowote kama hamtawawekea mazingira salama ya kuendelea kuaminika na kuwalindia matangazo waliyonayo pamoja na kuvutia matangazo mengine zaidi,ambayo ndiyo Uhai wa media yoyote duniani,siwezi kupeleka tangazo langu kwenye Tv ambayo mwonekano wake ni wa tabu,inaweza kusimama wakati wowote,na au inategemea untrusted network kurusha tangazo langu,mupo tayari kwa ushindani kweli?? Tuendelee kusubiria huduma nzuri kutoka kwenu? Au tutafute plan B??
Hii ya malipo ina matatizo zaidi kwenu kuliko LUKU,fanya utafiti binafsi na utaungana na wateja wako kutafuta solution.
Habari yako Tamar, kama nilivyoeleza katika post zangu zilizopita kustak kwa chanel hakusababishwi na mitambo yetu au uimara wa king'amuzi, la hasha, hili husababishwa na upokeaji hafifu wa mawimbi kwa mteja. unapopokea mawimbi hafifu inasababisha decoder kushindwa kusukuma picha na hivyo hupolekea picha kuganda au kuscratch. hivyo ukiona decoder yako inascratch ujua unapokea mawimbi hafifu ambayo husababishwa na antena yako kufungwa vibaya au kuwa katika uelekeo usio sahihi. ndio maana mara zote huwa tunawashauri wateja wetu kuhakikisha antena zao zimefungwa vizuri na katika uelekeo sahihi.
pili kuhusu chanel kama UBC, KBC au CITIZEN, nafikiri katika ving'amuzi hatuna UBC na KBC hii inatokana na sababu za kisheria ambapo kunabaadhi ya maudhui ya chanel hizi haturuhusiwi kurusha hapa tanzania, na ndio maana ilifika wakati hawa kipindi cha kombe la euro cup tulikuwa tunazima ubc isionyeshe mechi, hivyo ili kuondoa usumbufu huo kwa wateja wetu kuwa tunazima chanel hizo tukaona ni bora zikaondolewa kuruhusu kuingizwa chanel za ndani ambazo zilihitaji nafasi
kuhusu hayo makampuni ya bure, ninawasiwasi na huo usemi wao, lakini natumai hiyo ni marketing strategies tu, baadae wataainisha gharama zao za mwezi, hata sisi tulipoanza ilikuwa bure. wote tupo registered kama PAY TV,
Una wasiwasi!! Huna imani na TCRA?au huwa wanasajili kampuni ambayo hawajui kwa hakika inatoa huduma gani?
Kuhusu malipo kupitia Mpesa au tigo pesa, kawaida inategemea na system toka pande zote mbili na ndio maana leo ukinunua umeme kupitia tigo pesa na mpesa utakuwa muda wa kupata token unatofautiana. kwa hiyo kwa upande wetu tunajitahidi sana ingawa system zetu na voda zimekaa vizuri sna na zipo haraka, tigo kwa kuwa ni ndio huduma tumeanza hivi karibuni bado tunaendelea kufanyamarekebisho katika system zetu kutatua changamoto kadhaa
Hii ya malipo ina matatizo zaidi kwenu kuliko LUKU,fanya utafiti binafsi na utaungana na wateja wako kutafuta solution.
habari yenu wana jamii forum
tunapenda kuwajulisha wateja wetu kuwa kwa sasa chanel ya startv imerudi hewani na inapatikana bure kabisa kama ilivyokuwa awali, wateja wetu wataendelea kuiangalia chanel hii pamoja na zingine tano, (itv, eatv, clauds tv kwa dar, chanel ten) bure hata muda wao wa hewani utakapokuwa umemalizika
tunapenda kuwashukuru kwa uvumilivu wateja wetu wote na tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa kuna changamoto nyingi sana, lakini tunajitahidi sana kuweza kutatua matatizo madogo madogo kwa wateja wetu. Tunashauri kama mteja wetu atakuwa na tatizo lolote ni vema akatoa taarifa na sio kukaa kimya kwani kukaa na tatizo kisha kulalamika sio kutatua tatizo. Tuna timu ya mafundi 100 ambao wanazunguka mitaani kutoa misaada bure kabisa ya kiufundi.
Tafadhari kama kuna yeyote mwenyetatizo anaweza kututumia namba yake ya simu katika inbox yetu
tunashukuru sana
Habari yenu wana jamii forum
tunapenda kuwajulisha wateja wetu kuwa kwa sasa Chanel ya Startv imerudi hewani na inapatikana bure kabisa kama ilivyokuwa awali, wateja wetu wataendelea kuiangalia chanel hii pamoja na zingine tano, (ITV, EATV, CLAUDS TV kwa dar, CHANEL TEN) Bure hata muda wao wa hewani utakapokuwa umemalizika
tunapenda kuwashukuru kwa uvumilivu wateja wetu wote na tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa kuna changamoto nyingi sana, lakini tunajitahidi sana kuweza kutatua matatizo madogo madogo kwa wateja wetu. Tunashauri kama mteja wetu atakuwa na tatizo lolote ni vema akatoa taarifa na sio kukaa kimya kwani kukaa na tatizo kisha kulalamika sio kutatua tatizo. Tuna timu ya mafundi 100 ambao wanazunguka mitaani kutoa misaada bure kabisa ya kiufundi.
tafadhari kama kuna yeyote mwenyetatizo anaweza kututumia namba yake ya simu katika inbox yetu
tunashukuru sana
StarTimes
Tanzania hongereni kwa kumaliza tofauti baina yenu na
Star TV kwa kuzingatia mahitaji ya
walaji.
Nimekuelewa mkuu, tutajitahidi kutatua tatizo hilo