Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,697
- 2,559
Bado changamoto nyingi tulizonazo zinasababishwa na watawala na serikali zetu za kiafrika. Kwa Akili ya kawaida na viongozi wenye Akili timamu hawawezi kulazimisha kila Bus dogo linaloenda kwa Mattias, kongowe au mlandizi kupitia Loliondo.
Miundombinu ya kuingia njia hiyo ndio shida ilipo, kwanza Kona Kali ya kuchepukia katika high way ya morogoro hili tumemwachia mwenyezi ila siku yeyote pale wanapasuka watu ila hatuombei itokee.
Kikitokea chochote asitafutwe mchawi. pili barabara yenyewe ni mbovu na inaharibu magari na kupoteza muda kwa watu wanaokwenda mbali. Tatu stand yenyewe ni aibu kwa serikali ya Jamhuri ya muungano na mkoa wa pwani.
Ni kweli Pwani wanakaa waswahili lakini waswahili wapenda vitu vizuri sio huu ujinga wa Loliondo. Nne mie kwa hesabu yangu ya ngumbalu ni Zaidi ya Bus 100 ziko katika njia hii na stand haifai hata kwa gari 10 kuitumia kwa wakati na kubwa kuliko ni Geshi la Polisi ndio wamegeuza dambwe la kuchukulia rushwa, njia mbaya na lazima kupita madereva wakichepuka wanakutana na wala rushwa.
Kunaulazima gani wanaokwenda Mlandizi kupitia Loliondo, kwanini tusichague wenyewe tokea mbezi tupunguze jam na usumbufu kama hakuna anayeshuka tuokoe muda. Kwanini iwe lazima wakati miundombinu haiko tayari kuhudumia watu wengi.