Staa wa mieleka,John Cena afunguka kuwa anahitaji mtoto kwani anapata fedheha.

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
268,184
1,095,288
Licha ya kupitia kwenye mahusiano na wanawake lukuki, Mwanamieleka maarufu duniani, John Cena ameonekana nafsi yake kufedheheka kwa kukosa mtoto. John Cena (41) ambaye ameshapitia kwenye maisha ya ndoa kwa miaka minne na aliyekuwa mke wake wa ndoa Elizabeth Huberdeau, hajabahatika kupata mtoto jambo ambalo amekiri linamnyima raha. “nimepitia kwenye mahusiano tofauti tofauti, lakini sijabahatika kupata mtoto. mwanzoni nilikuwa naangalia mwanamke nitakaye jenga naye familia lakini kwa sasa natamani zaidi kupata mtoto hata kwa njia ya upasuaji ikiwezekana,“ameeleza John Cena kwenye mahojiano yake na kipindi cha Today cha NBC. Mwanzoni mwa mwaka huu John Cena alimvisha pete ya uchumba mcheza mieleka mwenzie Nikki Bella lakini miezi miwili baadae wakamwagana. Katika maisha yake yote, John Cena hajawahi kupata mtoto na alishawahi kutamka wazi miaka ya nyuma kwamba hapendi watoto.
43778655_2187298988214225_1664841366493427447_n.jpg
 
Asisikitike amshukuru tu Mungu, ukute anakutana na wanawake waaminifu, huku kwetu wangekuwa wamemzalia watoto kibao. Mtoto wa kwanza anaweza kuwa kweli wako lkn huko mbele anaanza kumix, inabidi ulee tu ss utafanyaje, hata km mtoto humwelewi hata km ujauzito tarehe zinaonyesha ulikuwa safari, we uchune tu.
 
Back
Top Bottom