Spika Tulia unamharibia Rais Samia nchi, mambo mabaya yameharibikia mikononi mwako

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Nimebaini kuwa adui mkubwa wa Taifa la Tanzania kwa sasa ni Dk.Tulia Ackson ambaye mambo yote machafu yamefia mikononi mwake na taifa likiwa halijua linatokaje kwenye mkwamo huu. Mfano wa mambo yaliyofia mikononi mwa Tulia na Bunge lake.

1. Mkataba wa Bandari Serikali iliupeleka Bungeni tangu mwezi wa Februari 2023 Spika amekaa nao kwa miezi mitano hadi Juni 2023 ndiyo anauleta Bungeni tena kwa dharura na kujadiliwa siku moja na kupitishwa na kusababisha balaa linaloendelea sasa.

2. Ripoti ya CAG amepelekewa tangu mwezi Machi huku ikionyesha ufisadi mkubwa wa matrilioni ya fedha yeye ameikalia anasema hadi Novemba ndiyo itajadiliwa wakati mwenzake Spika Makinda alipopelekewa ripoti ya CAG na kuonyesha ufisadi wa Escrow aliitisha bunge la dharura kujadili hoja ya Escrow hakusubiri bunge la Novemba.

3. Kuna Mbunge aliomba indwe tume kuchunguza suala la bei ya Mafuta tangu Mwaka jana Juni 2022 ili ukweli ufahamike kuhusu biashara nzima ya mafuta, Spika akakataa ushauri huo wa kuunda tume kwa kuwalinda hao wahusika leo nchi inalia kila kona tatizo la mafuta

Ni dhahiri anayeshabikia na kusababisha Serikali kuchafuliwa na kutukanwa kwa kiwango hiki na wananchi wengi kupoteza imani na Serikali yao ni huyu Spika wa Bunge ambaye mambo yote yanayohitaji uamuzi ameyakalia ofisini kwake kwa manufaa binafsi.

Kila jambo Rais analiwahisha Bungeni kwa ajili ya hatua lakini Spika akifika yeye anazunguka na mambo hayo kwa faida anazojua yeye.
 
Naunga mkono hoja, mambo yote yameharibikia kwake Tulia ndiyo maana suala la bandari analiongea yeye peke yake tena kwa kupaniki kweli kweli na nina wasiwasi sana hata kwenye vikao vyao vya ndani huenda anawapotosha wabunge na mh Rais kwenye mambo mengi kwa kisingizio kwamba ana PHD ya Sheria.
 
Nimebaini kuwa adui mkubwa wa Taifa la Tanzania kwa sasa ni Dk.Tulia Ackson ambaye mambo yote machafu yamefia mikononi mwake na taifa likiwa halijua linatokaje kwenye mkwamo huu...
Hata wana ccm wenzake Mbeya wanajua Spika anajikomba komba tu na Yuko tayari kushawishi Bunge na kuishawishi Serikali iuze hata viwanja vya ndege vyote, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro, Serengeti na raslimali zozote za nchi ikiwa tu Mh Rais Atamhakikishia ubunge wake na Uspika 2025
 
Nilisoma makala BBC kipindi Tulia amechaguliwa na chama chake kuwa spika. Walisema hana 'spine', ukiachana na akili za darasani huku kwingine ana akili za kushikiwa. Ni mtu wa kunyenyekea mamlaka.

Hatuna bunge, hatuna spika. Kwakifupi nchi iko kwenye autopilot. Tunaelekea wapi ni Mungu tu ndio anajua.

Itachukua miaka 100 kwa wanawake kuja kuaminiwa tena kwenye nafasi nyeti kama rais na makamu wa rais.
 
Nilisoma makala BBC kipindi Tulia amechaguliwa na chama chake kuwa spika. Walisema hana 'spine', ukiachana na akili xa darasani huku kwingine ana akili za kushikiwa. Ni mtu wa kunyenyekea mamlaka.

Hatuna bunge, hatuna spika. Kwakifupi nchi iko kwenye autopilot. Tunaelekea wapi ni Mungu tu ndio anajua.

Itachukua miaka 100 kwa wanawake kuja kuaminiwa tena kwenye nafasi nyeti kama rais na makamu wa rais.
Chukua maua yako
 
Nimebaini kuwa adui mkubwa wa Taifa la Tanzania kwa sasa ni Dk.Tulia Ackson ambaye mambo yote machafu yamefia mikononi mwake na taifa likiwa halijua...
Hayo yote bunge letu kamwe haliwez yasimamia ✔️Rais laiti angekua na team inayoendananae angeweza san kupeleka mamb vzr, but kazungukwa na crews ambazo haziendan nae.
 
Nimebaini kuwa adui mkubwa wa Taifa la Tanzania kwa sasa ni Dk.Tulia Ackson ambaye mambo yote machafu yamefia mikononi mwake na taifa likiwa halijua linatokaje...
Wahenga walinena kitambo, "kikulacho kinguoni mwako.." Spika wa Binge amechangia kuchafua Kwa maamuzi yake ya kiti. Muda utahukumu!
 
Nimebaini kuwa adui mkubwa wa Taifa la Tanzania kwa sasa ni Dk.Tulia Ackson ambaye mambo yote machafu yamefia mikononi mwake na taifa likiwa halijua...
Yeye anadhani Ndio Rais Samia atamkubali ili ampe sapoti kupita bila kupingwa 2025
 
Ye hapendi kuishi?
Mnapenda kuyachukulia mambo juu juu
Hebu mkue basi.
Wewe ndie unamfanya aishi? Kipi bora kwako..utumikie ushauri haramu ili uishi kwa majuto badae au utumikie kusudi la aliyekuumba upate thawabu ya milele..
 
Back
Top Bottom