MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,221
- 22,295
Leo natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusu ishu ya wabunge 19 wa viti maalum kutoka CHADEMA ambao walifutwa uanachama hivi karibuni. Na haya maoni ninayoyatoa nikiwa nimejiridhisha kabisa na ukweli kuhusu hili sakata. Ni suala zito linalohitaji kufikiria kwa makini.
Mengi yameshasemwa ila leo ninampongeza Spika kijana Tulia Akson kwa kuweza kusimama kidete hadi leo kaa kuhakikisha haki ya kina mama 19 yinapatikana. Spika kijana Tulia kwa hakika alishaona nia ya vigogo wa CHADEMA kwenye hili suala ilikuwa kuwaondoa kina Mdee na kuwaingiza watu wao ambao hawana historia yoyote ndani ya CHADEMA. Spika kalinda maslahi mapana ya taifa. Kuwang'oa wabunge waliokipigania chama kama Mdee na kuwaweka wasiojulikana ni hujuma kwa taifa.
Pia CHADEMA kutomfikisha mahakamani mtu aliyefoji barua ni sawa na kumlinda mhusika na kutetea uovu. Ilibidi na aliyefoji sahihi na mhuri wa chama afukuzwe pia uanachama pamoja na kufikishwa mahakamani. Kauli ya Mbowe kwamba alimwambia Mdee aachie ubunge ili akafanye kazi ya mshahara wa mamilioni nje ya nchi ni sababu nyingine inayoongeza ulazima wa hawa kina mama shupavu 19 kutetewa. Haiwezekani kipaji kikubwa cha siasa kama cha Halima tukizike kwa mshahara wa kazi fulani nje ya nchi.
Nampongeza sana Spika kijana Tulia kwa kazi nzuri. Kwa sababu ya umri mdogo namwombea aje kuwa Rais wa nchi hii miaka ijayo.