Spika Sitta - Iko wapi ripoti ya uchawi bungeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta - Iko wapi ripoti ya uchawi bungeni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mgaya, Jul 3, 2008.

 1. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zinakwenda sasa na hakuna chochote kinachosemwa kuhusu suala la mbunge wa ccm na kiongozi mnene kabisa wa ccm ambaye pia anaita mapesa ya wizi vijisenti kufanya vitendo vya uchawi bungeni.

  Mheshimiwa Sitta uliahidi kufanyia uchunguzi jambo hili, je umefikia wapi? Kama mnataka kufunika aibu katika hili basi ujue kuwa litajadiliwa hapa JF kwa vile ni jambo muhimu sana kwa maendeleo ya siasa za Tanzania. Wahenga walisema kuwa mficha kidonda harufu itamuumbua. Nakuomba Mheshimiwa Sitta ulete report ya uchawi bungeni na wahusika wachukuliwe hatua haraka sana iwezekanavyo.
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mwenye kutakiwa kutoa ripoti hapa sio Spika kwani yeye tayari alishawasilisha nyaraka na vielelezo kwa vyombo vya dola , sasa hapa adaiwe Mkemia mkuu ,na polisi pamoja na idara ya usalama wa taifa .
   
 3. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wewe Mgaya wenzako wanaficha aibu waliyoipata baada ya vyombo vya habari vya Kenya na Uganda kuanza kuifuatilia hii habari na wewe unataka kuifufua. Yataanza maswali ya magari yanayokwenda bagamoyo kila mwisho wa wiki na mengine mengi ambayo wakulu hawataki kuyaongolea.

  hii ndio imetoka hivyo na hakuna report wala nini.
   
 4. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe lakini pia uchawi ulifanyika bungeni na spika ndiye mkuu wa kaya ya bunge kwa hiyo si vibaya akiulizwa kuhusu hili.

  Asante kwa maelezo na ufafanuzi
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Ripoti ya uchawi bungeni ni muhimu ikatoka kwani kuna wabunge wengine huko bungeni ambao kwa kusema kweli kauli zao zinatia shaka.
   
 6. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naisubiria kwa hamu kubwa sana ili ukweli ujulikane na utendaji kazi wa mafisadi wa ccm uwe wazi zaidi
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Tena si ya kuisubiria kwa hamu...Bali waitoe kabla hata ya kuanza mjadala wa TAIFA!
  Kwani si walisema huo "UNGA UNGA" Uko kwa mkemia mkuu?
  Sasa kama kuna mbunge wetu ambaye alipata madhara na wabunge wetu ndio watunga sheria...Then inakuwa vipi waathirike ama KUTISHIWA MAISHA YAO halafu mjadala uendelee bila ya kutoa taarifa kamili za UCHUNGUZI?
  Tuambiwe huo unga unga ilikuwa ni nini na huyo aliyouweka alikuwa na maana gani?
   
 8. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiih Hey watch out usije kupigwa kipapai na wewe kwa kufunua mambo ya juju la waheshimiwa ambalo nahisi spika ameitia kapuni kiaina....Sasa unakumbushia tena? Unaweza kusikia jogoo analia tumboni mwako humo..Teh! teh!tehteh!!
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Kwa hali ilivyo kipapai kinaweza kuwa tayari kwani wabunge wenyewe wanalala tu huko bungeni!
   
 10. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwi kwi kwi,

  Mimi hawaniwezi, uchawi wao utaishia huko huko bagamoyo na idodomya lakini sio hapa mtandaoni.
   
 11. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa mushi, ukiona jinsi wanavyolala huku mafisadi wakipeta tu basi utaamini kuwa vipapai vimewazidia nguvu. Unakumbuka Dr Slaa alivyokumbusha wabunge kusema kila kinachoandikwa hadi Mkullo akabidi kubadili maandishi kwenye bajeti yake?

  Waache uchawi na kufanya kazi, inatisha sasa.
   
 12. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama watu wameanza kuchinja akina mama wanatafuta makoo itakuwa hii ya unga kwenye bunge, wakubali wasikubali uchawi upo, wangetoa taarifa tu ili guessing game iishe.
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Ukiacha wale waliolazwa hospitali...Kuna wale wanaoongea kama wamechanganyikiwa...Na wale wenye kunyamaza...Wanayafanya haya!
  RIPOTI ITOKE MARA MOJA!

  [​IMG]
   
 14. M

  Mgaya JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 520
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wao wanajua watanzania ni wepesi wa kusahau kwa hiyo wanavuta muda ili yasahaulike na mzee wa vijisenti aendelee "kutafuta kiti cha kukaa usiku wakati taa zimezimwa na kamera za usalama zimewekwa off"
   
 15. D

  DIKTETA Member

  #15
  Jul 4, 2008
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Spika Anaficha Kwakuwa Akitoa Mkanda Na Ripoti Hio Ni Yeye Ndio Atakuwa Ni Mzushi Na Muongo...chenge Kasema Wazi Kuwa Mkanda Uchezwe,yeye Anauficha Kwa Manufaa Ya Nani?mh Sita Hana Uwezo Wa Kutosha Ni Bingwa Wa Kuruka Maamuzi Yake..alipata Kusema Ra Aje Ajieleze Bungeni Na Alipoona Maelezo Yanamuumbua Akayaweka Kapuni
   
 16. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inamaana Mkemi Mkuu nae ni mganga? Maana ninavyofahamu mimi kama sio mganga basi jibu litakalo kuja tutaambiwa sio Uganga ni VUMBI TUU MAANA SIUNAJUA DODOMA KUNA VUMBI SANA
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  wangesha tangaza matokeo au ndo mambo yaleyale ya kutotoa matokeo ya uchunguzi au tume? Ila mimi nadhani kuna katatizo hapo ndiyo maana inawachukua muda mrefu.
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Vumbi lipelekwe kwa mkemia mkuu?Mkemia mkuu yeye mwenyewe hawezi kuujua uchawi labda kama na yeye ni mchawi!
  Sisi tunachotaka ni ripoti!
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Jamani Salva kesha waambia waandishi wasiandike habari za "NDUMBA" maana wawekezaji watafyatuka mbio, mnadhani agizo hilo alilotumwa Salva kulitoa linaishia kwa waandishi pekee? hata Kwa Spika habari ndio hiyo. Ala!
   
 20. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwani Bungeni kulikua na uchawi nyie vipi?Si mshaambiwa mheshimiwa alikua anatafuta kiti chake?Sasa mnataka ripoti gani kama sio umbea usio na mpango!!!
  Watu wanatafuta viti vyao nyie mnalalia uchawi!! Tehe tehe...... mshapigwa changa na changa lenyewe limemwagiwa maji limegeuka tope.Ukipigwa tope jichoni unafikiri utalitoa hivi hivi??

  Shauri zenu
   
Loading...