Spika: Sasa Lissu akiongea tutamjibu

Spika: Sasa Lissu akiongea tutamjibu

Sehemu ya Bunge kuanzia kujiimaarisha kwa kuruhusu hoja binafsi au kuunda kamati teule ya kuchunguza mauji ya kibiti, kigoma, njombe (wototo) na mengineyo ya mtu mmoja mmjoja anayesadikiwa amekufa kifo tatanishi.

Ikiwezekana kwa upande wa pili, iundwe tume huru ya majaji nao wafanye uchunguzi vifo hivi na matokeo ya uchunguzi yawekwe wazi.

Lengo lake likibeba sura ya kuleta maridhiano kwa makundi mbalimbali katika jamii ambao kwa sasa wanalazimika kusungumzia chini ya meza ambacho ni kitendo hatari kuliko kilipuzi cha nuclear.

Waachwe wa pumue, wasipopumuwa watavimbiwa, chumba hakitakalika kwa kuenea kwa harufu mbaya. Vyoo vitakuwa vimejaa, matundu yatakuwa machache, na itawalazimu watu kukidhi haja zao mahala popote watakapoona inafaa.
 
Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kwasasa kama Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akisema anapaswa kujibiwa kwakuwa inaonekana amepata nafuu/amepona.

Spika Ndugai amesema kuwa mwanzoni ilionekana si vyema kujibizana na aliyekuwa kitandani akijiuguza. Swali langu binafsi ni kuwa kumjibu Lissu hakutamfanya Lissu kusema zaidi na kuendeleza malumbano?
Lissu anasema kwenye international madia mzee wa rungu ananunua tbc, tanzanite nk
 
Lissu hata wewe hauwezi kumsaidia! ila angekuwa professor J angesaidiwa

unatukana watu wanaopaswa kukusaidia?

mkuu hawakupitia procedures za kawaida na waligoma, ananyooshwa na nobody cares mkuu

mwanzoni, tukubali kabisa kuwa CDM walilibeba kama lao, waka ignore utaratibu wa kawaida kabisa. halafu leo ndio inakuwa fimbo. hakuna anayejali, hakuna anayetetemeka kwa lolote

Kutibiwa kwa Pesa za Watanzania kupitia Mwamvuli wa Bunge ile ni Haki yake ,ni moja ya Stahiki zake zilizo kisheria na sio Msaada kama unavyo yaka kupotosha hapa.Halafu Serikali inapo ambiwa Ukweli sio Matusi/sio kutukanwa pia tujifunze kuwa Sheria ni kwa Watu wote wana paswa kuzifuata.

Nje ya hapo inayupasa sisi kama Binadamu (wenye mapungufu) ,tunspaswa kuweka Utu wetu mbele zaidi ya Vyeo vyetu .
 
Malizeni tu kuropoka lakini hamuwezi kufuta ukweli anaosema Lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona "ukwel anaosema Lissu" wengine tumekubaliana aendelee ila inatakiwa tuendelee na shughuli zingine kama hatumsikii vile mana spika akimtaka amjibu kila kitu itakuwa ni kupoteza muda kubishana na mtu mwenye sumu moyoni ya kuumizwa ingawa kwel ya waliomuumiza wote hatuijui

So elewa kwa kitendo alichofanyiwa mh. Lissu hata mimi sikubalian nacho hata kidogo na walaaniwe waliomfanya vile ingawa kwel ya yote hatuijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani Ndugai hajui anachokifanya, anakubali kufanya kile anachoambiwa kukifanya na yulee...

Kuna mambo ya kujadili hapa.
Kwanza sio kweli kuwa bunge halijawahi kumjibu Lissu, toka aliposhambuliwa limekuwa likimjibu, lakini majibu ya bunge yamekuwa yakipwaya sana. Labda Ndugai atuambie sasa, kama bunge limebadilisha style, litakuwa linamjibu Lissu papo kwa hapo. Na kama ndio hivyo maana yake Ndugai ametangaza vita dhidi ya Lissu, je ataweza?

Jambo la pili ni kuwa, maswali ya Lissu yapo wazi mnoo, lakini majibu ni msumari wa moto. Kauli yoyote ya Bunge kumjibu Lissu itakuwa ni kuleta mchanganyiko zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwa mfano, Ndugai ameanza kumjibu Lissu jana, ndani ya masaa 24 tu, spika yeye mwenyewe amekuja tena kujikanusha.

Lissu anasema toka apigwe risasi, bunge halijatoa hata senti tano kumtibia. Na ni kweli halijatoa. Ndugai atajibu nini?

Lissu anasema alipigwa risasi ndani ya mazingira ya makazi rasmi ya wabunge mchana kweupe ambayo yanalindwa masaa 24 na askari tele wenye silaha, wahusika walifanya tukio hilo na kuondoka salama salimini, hakuna aliyewakamata, aliyewakimbiza wala aliyewasaka mpaka sasa. Ndugai utajibu nini?

Lissu anasema eneo alilopigwa risasi linaangazwa na kamera za CCTV masaa 24, na siku ya tukio kamera hizo zilikuwepo On, lakini baada ya tukio lile hizo kamera zikaondolewa. Ndugai atajibu nini?

Lissu anasema tukio la yeye kupigwa risasi analihusisha moja kwa moja na mwelekeo wake wa kisiasa, huku akivihusisha vyombo vya dola na serikali ya awamu ya tano kutokana na mtitiriko wa matukio kabla ya tukio hilo. Sasa Ndugai anahusika vipi na hilo mpaka aje kulijibu?

Lissu kwa sasa anaongea na dunia nzima kupitia mahojiano yake ya vyombo vya habari na mikutano mbalimbali ya makundi ya kimataifa. Ndugai yuko Dodoma, akipambana na bundi bungeni, halafu anasema atamjibu Lissu!! Naye atoke, aombe Coverage na idhaa ya kiswahili ya BBC, Ujerumani, America nk ili wamuhoji na kuja na majibu.

Binafsi bado namuona Ndugai hatoshei hata kwenye kijiko kuweza kumjibu Lissu kwa hoja.
Tena pesa anazodai ndugai wamemlipa lissu ni mshahara na Posho za mbunge, awe anaumwa au haumwi, hizo 203 ml ni mshahara na posho kabla ya kodi. Lakini pesa za matibabu na ambayo ni haki yake hajalipwa. Na wao walitegemea atakufa lakini Mungu sio John, Leo Lissu ni mzima na wanajijanyaga tu [emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai Figo bado zinauma. Anaumuka sura kama bumunda
si vema kujenga utamaduni wa matusi namna hii, kwa nini tusilumbane kwa hoja? Yaani JF ndiyo mpo hivi? Yaani unategemea spika ajenge nchi kwa kumtukana? Nadhani ni muhimu kumheshimu Mh spika na bunge maana hao ndiyo watunga sheria wetu kwa sasa including wabunge wetu wa upinzani. Tuache kejeli na matusi
 
"Tutamjibu kila kitu" halafu jibu lako la kwanza unakuwa uongo mkubwa ambao baada ya masaa machache unakanusha kuwa wamekunukuu vibaya? Labda useme video recorder's zimekurekodi tofauti maana zipo.
Utawala huu utakapo toka na yote kuwekwa hadharani tutashangaa sana na kukasirika

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana hawataki kutoka
 
Chadema kazi sana kuwaelewa,kuna muda wanasema Lissu ajibiwe hoja zake kwa maana hoja hujibiwa kwa hoja,Spika anataka kujibu wanasema tena eti ndio ataharibu kabisa,sasa nini mnataka nyie watu?

Bomba Mvua
 
..hayo yalitokea baadae.

..Ndugai alitakiwa a take control of the situation kabla TL hajapelekwa Nairobi.

..He should have insisted that TL akatibiwe kule ambako familia imependekeza, which was Nairobi, na serekali isaidie kufanikisha maombi ya familia.

..Ni suala la UTU na BUSARA tu. Msimamo kuwa huyu ni TL basi tumsusie ili apate shida ndiyo yaliyotufikisha hapa.
Chadema walihijack process kwa interest ya kisiasa. Wskawa wanaoishana na kutanua tu kwenye five star hotels Nairobi. Kina Lema na Msigwa na genge lao wakanona na kunawiri. Lissu akaitukana serikali. Sasa hapo busara IPI itumike?
 
Chadema walihijack process kwa interest ya kisiasa. Wskawa wanaoishana na kutanua tu kwenye five star hotels Nairobi. Kina Lema na Msigwa na genge lao wakanona na kunawiri. Lissu akaitukana serikali. Sasa hapo busara IPI itumike?

..hayo yote yasingetokea kama SPIKA ange-take control of the situation na KABLA mgonjwa hajapelekwa NAIROBI.

..Hivi mtu yuko ktk hatari ya KUKATA ROHO halafu Spika anaanza mabishano ya taratibu na baada ya hapo anamsusa mgonjwa?!
 
..hayo yote yasingetokea kama SPIKA ange-take control of the situation na KABLA mgonjwa hajapelekwa NAIROBI.

..Hivi mtu yuko ktk hatari ya KUKATA ROHO halafu Spika anaanza mabishano ya taratibu na baada ya hapo anamsusa mgonjwa?!
Kwa nini unataka speaker peke yake awe na busara na siyo hao wengine?
 
..Spika ameli complicate suala la TL bila sababu yoyote.

..alitakiwa apambane kumpatia matibabu TL kwa utaratibu wa bunge, au nje ya utaratibu.

..pia alitakiwa awe mstari wa mbele kulishinikiza jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini wahusika.

..It is in our best interest waliomshambulia TL kukamatwa. Wasipokamatwa wanaweza kufanya ugaidi wao kwa Mtanzania mwingine.

..Binafsi naamini SPIKA angetumia UTU na BUSARA suala hili lisingeharibika kiasi hiki. Na TL angekuwa hana sababu ya kuzunguka nje ya nchi akilaumu Bunge na Serekali.
Anashinikiza vipi uchunguz wakati mhanga wa tukio kakimbia na dereva?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Aende akamjibu huko HARDTALK na dochovele kama anaweza , Ndugai lugha yenyewe haipandi ,anajibia bungeni lissu aliyaongea hayo bungeni ?
 
Aende akamjibu huko HARDTALK na dochovele kama anaweza , Ndugai lugha yenyewe haipandi ,anajibia bungeni lissu aliyaongea hayo bungeni ?
 
Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kwasasa kama Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akisema anapaswa kujibiwa kwakuwa inaonekana amepata nafuu/amepona.

Spika Ndugai amesema kuwa mwanzoni ilionekana si vyema kujibizana na aliyekuwa kitandani akijiuguza. Swali langu binafsi ni kuwa kumjibu Lissu hakutamfanya Lissu kusema zaidi na kuendeleza malumbano?
Namuunga mkono Spika kuwa akiongea Tundu Lissu na yeye anatakiwa kumjibu kwa kuwa ndy Bosi wake,
Hoja inajibiwa kwa hoja mfano Tundu Lissu amedai kuwa hajawahi kulipwa na Spika anaweka hadharani kuwa Taasisi yake imeshamlipa kiasi cha 250,M.
Madai mengine yajibiwe na serikali na sisi raia tutajua nani mkweli kati ya hoja zinazotolewa na pia kujibiwa ina maana hata huko anakoenda wanakuwa wana baadhi ya majibu kutoka serikalini na kwenye Bunge
 
Anashinikiza vipi uchunguz wakati mhanga wa tukio kakimbia na dereva?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.

..tuwe wakweli ndugu zangu.

..kama Polisi wangekuwa na nia ya kweli ya kumpata dereva wa TL basi wangewasiliana na wenzao wa Kenya au Ubelgiji ili dereva huyo ahojiwe au arejeshwe nchini.

..msifikiri suala hili lina maslahi kwa TL peke yake.

..hivi tuna uhakika gani kama waliomshambulia TL hawawezi kumshambulia mtu mwingine?

Cc Nguruvi3
 
Tuanze na procedures kwanza inasemaje?

1.spika was abused


usichekeshe watu

..Procedure wakati TL alikuwa ktk hatihati ya kukata roho?

..I dont think wewe ungekuwa ndiyo Spika ungemfanyia vile mbunge mwenzako ambaye maisha yake yapo hatarini.

..Inahitaji uwe na ROHO NGUMU kwelikweli kufanya kama Spika Ndugai.

..Na ukumbuke Spika amekuwa akilipiwa matibabu na bunge kwa muda mrefu. Vipi mtu wa namna hiyo akose HURUMA na UPENDO kwa mbunge wake.
 
..tuwe wakweli ndugu zangu.

..kama Polisi wangekuwa na nia ya kweli ya kumpata dereva wa TL basi wangewasiliana na wenzao wa Kenya au Ubelgiji ili dereva huyo ahojiwe au arejeshwe nchini.

..msifikiri suala hili lina maslahi kwa TL peke yake.

..hivi tuna uhakika gani kama waliomshambulia TL hawawezi kumshambulia mtu mwingine?

Cc Nguruvi3
Serikali kupitia polisi haiitaji kutumia nguvu hata kdg ilhali mhanga mwenyewe anaweka kauzibe. Dereva kaondoka hapa kwa kutoroshwa na akina Lema, Kwanini?Yuko huko Belgium bila hati zozote za kusafiria toka Tanzania,nani alimfanyia mpango aende huko wakati anajua huyo dereva anatakiwa awe nyumbani kusaidia polisi?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Ndugai Figo bado zinauma. Anaumuka sura kama bumunda

Hoja hujibiwa kwa hoja na sio kujibu kwa viroja kama ufanyavyo wewe.
Kila mtu ni mgonjwa na mwenyezi Mungu humponya kadri ya uweza wake.
 
Back
Top Bottom