Spika: Sasa Lissu akiongea tutamjibu

Spika: Sasa Lissu akiongea tutamjibu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
Spika wa Bunge Ndugu Job Ndugai amesema kuwa kwasasa kama Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akisema anapaswa kujibiwa kwakuwa inaonekana amepata nafuu/amepona.

Spika Ndugai amesema kuwa mwanzoni ilionekana si vyema kujibizana na aliyekuwa kitandani akijiuguza. Swali langu binafsi ni kuwa kumjibu Lissu hakutamfanya Lissu kusema zaidi na kuendeleza malumbano?
 
Lissu akijibiwa hatimizi lengo lake

..Spika ameli complicate suala la TL bila sababu yoyote.

..alitakiwa apambane kumpatia matibabu TL kwa utaratibu wa bunge, au nje ya utaratibu.

..pia alitakiwa awe mstari wa mbele kulishinikiza jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini wahusika.

..It is in our best interest waliomshambulia TL kukamatwa. Wasipokamatwa wanaweza kufanya ugaidi wao kwa Mtanzania mwingine.

..Binafsi naamini SPIKA angetumia UTU na BUSARA suala hili lisingeharibika kiasi hiki. Na TL angekuwa hana sababu ya kuzunguka nje ya nchi akilaumu Bunge na Serekali.
 
Nasikia kuna jamaa raia walikua wanataka kumbeba kuashiria wanavyomkubali, askari wakapiga sana watu kuzuia wasimbebe yule jamaa.

Nyerere akaingilia akasema kama mtu anataka kubebwa na wa kumbeba wapo acheni abebwe.

Wabebaji wote wakayeya.

Tangu mwanzo hakuna aliyetakiwa kujibiwa wala kuzuiwa kufanya anachotaka maana hatima yake ni kuchoka tu.
 
..Spika ameli complicate suala la TL bila sababu yoyote.

..alitakiwa apambane kumpatia matibabu TL kwa utaratibu wa bunge, au nje ya utaratibu.

..pia alitakiwa awe mstari wa mbele kulishinikiza jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini wahusika.

..It is in our best interest waliomshambulia TL kukamatwa. Wasipokamatwa wanaweza kufanya ugaidi wao kwa Mtanzania mwingine.

..Binafsi naamini SPIKA angetumia UTU na BUSARA suala hili lisingeharibika kiasi hiki. Na TL angekuwa hana sababu ya kuzunguka nje ya nchi akilaumu Bunge na Serekali.

Lissu hata wewe hauwezi kumsaidia! ila angekuwa professor J angesaidiwa

unatukana watu wanaopaswa kukusaidia?

mkuu hawakupitia procedures za kawaida na waligoma, ananyooshwa na nobody cares mkuu

mwanzoni, tukubali kabisa kuwa CDM walilibeba kama lao, waka ignore utaratibu wa kawaida kabisa. halafu leo ndio inakuwa fimbo. hakuna anayejali, hakuna anayetetemeka kwa lolote
 
Ndugu JokaKuu,

Kauli ya Ndugai (kama kweli kaitoa) kuwa kila akisema watajibu si yake huyu, imetoka huko Magogoni....

Na nikuambie, "kujibiwa huku", it's goes beyond your imagination!!

Na hebu jaribu kufikiri kidogo. Wajibu nini hasa ambacho kimekosa majibu tangu mwaka juzi Sept 7, 2017?

Kwa upande wake yeye kajaribu kujibu leo kwa njia ya mdomo wake, ndiyo kaharibu kabisa kuliko hata angenyamaza kimya....!!

Na ni kama anawafanya Watanzania wote ni wajinga wa viwango vyao kwamba hatuelewi ni nini hasa madai ya Tundu Lissu!!

Truly speaking, this is too sad....

Haieleweki tunakwenda wapi kama nchi iwapo hawa ndiyo viongozi wetu wanaotuongoza eti kuelekea nchi ya viwanda!!
 
Lissu hata wewe hauwezi kumsaidia! ila angekuwa professor J angesaidiwa

unatukana watu wanaopaswa kukusaidia?

mkuu hawakupitia procedures za kawaida na waligoma, ananyooshwa na nobody cares mkuu

mwanzoni, tukubali kabisa kuwa CDM walilibeba kama lao, waka ignore utaratibu wa kawaida kabisa. halafu leo ndio inakuwa fimbo. hakuna anayejali, hakuna anayetetemeka kwa lolote

..hayo yalitokea baadae.

..Ndugai alitakiwa a take control of the situation kabla TL hajapelekwa Nairobi.

..He should have insisted that TL akatibiwe kule ambako familia imependekeza, which was Nairobi, na serekali isaidie kufanikisha maombi ya familia.

..Ni suala la UTU na BUSARA tu. Msimamo kuwa huyu ni TL basi tumsusie ili apate shida ndiyo yaliyotufikisha hapa.
 
..Spika ameli complicate suala la TL bila sababu yoyote.

..alitakiwa apambane kumpatia matibabu TL kwa utaratibu wa bunge, au nje ya utaratibu.

..pia alitakiwa awe mstari wa mbele kulishinikiza jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini wahusika.

..It is in our best interest waliomshambulia TL kukamatwa. Wasipokamatwa wanaweza kufanya ugaidi wao kwa Mtanzania mwingine.

..Binafsi naamini SPIKA angetumia UTU na BUSARA suala hili lisingeharibika kiasi hiki. Na TL angekuwa hana sababu ya kuzunguka nje ya nchi akilaumu Bunge na Serekali.
Nia yake ni kumchokonoa ili aingie kwenye 18 ya sheria yao mpya walioitunga, hasa hapo atakaporudi
 
..hayo yalitokea baadae.

..Ndugai alitakiwa a take control of the situation kabla TL hajapelekwa Nairobi.

..He should have insisted that TL akatibiwe kule ambako familia imependekeza, which was Nairobi, na serekali isaidie kufanikisha maombi ya familia.

..Ni suala la UTU na BUSARA tu. Msimamo kuwa huyu ni TL basi tumsusie ili apate shida ndiyo yaliyotufikisha hapa.
No waliichukulia kisiasa zaidi, walitegemea atakufa ili shutuma zote ziende kwa wale waliochukua maamuzi ya awali katika kuokoa uhai wake
 
Nadhani Ndugai hajui anachokifanya, anakubali kufanya kile anachoambiwa kukifanya na yulee...

Kuna mambo ya kujadili hapa.
Kwanza sio kweli kuwa bunge halijawahi kumjibu Lissu, toka aliposhambuliwa limekuwa likimjibu, lakini majibu ya bunge yamekuwa yakipwaya sana. Labda Ndugai atuambie sasa, kama bunge limebadilisha style, litakuwa linamjibu Lissu papo kwa hapo. Na kama ndio hivyo maana yake Ndugai ametangaza vita dhidi ya Lissu, je ataweza?

Jambo la pili ni kuwa, maswali ya Lissu yapo wazi mnoo, lakini majibu ni msumari wa moto. Kauli yoyote ya Bunge kumjibu Lissu itakuwa ni kuleta mchanganyiko zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwa mfano, Ndugai ameanza kumjibu Lissu jana, ndani ya masaa 24 tu, spika yeye mwenyewe amekuja tena kujikanusha.

Lissu anasema toka apigwe risasi, bunge halijatoa hata senti tano kumtibia. Na ni kweli halijatoa. Ndugai atajibu nini?

Lissu anasema alipigwa risasi ndani ya mazingira ya makazi rasmi ya wabunge mchana kweupe ambayo yanalindwa masaa 24 na askari tele wenye silaha, wahusika walifanya tukio hilo na kuondoka salama salimini, hakuna aliyewakamata, aliyewakimbiza wala aliyewasaka mpaka sasa. Ndugai utajibu nini?

Lissu anasema eneo alilopigwa risasi linaangazwa na kamera za CCTV masaa 24, na siku ya tukio kamera hizo zilikuwepo On, lakini baada ya tukio lile hizo kamera zikaondolewa. Ndugai atajibu nini?

Lissu anasema tukio la yeye kupigwa risasi analihusisha moja kwa moja na mwelekeo wake wa kisiasa, huku akivihusisha vyombo vya dola na serikali ya awamu ya tano kutokana na mtitiriko wa matukio kabla ya tukio hilo. Sasa Ndugai anahusika vipi na hilo mpaka aje kulijibu?

Lissu kwa sasa anaongea na dunia nzima kupitia mahojiano yake ya vyombo vya habari na mikutano mbalimbali ya makundi ya kimataifa. Ndugai yuko Dodoma, akipambana na bundi bungeni, halafu anasema atamjibu Lissu!! Naye atoke, aombe Coverage na idhaa ya kiswahili ya BBC, Ujerumani, America nk ili wamuhoji na kuja na majibu.

Binafsi bado namuona Ndugai hatoshei hata kwenye kijiko kuweza kumjibu Lissu kwa hoja.
 
kuna watu wakikaa kimya unaweza tamani ukawaombe ushauri ila wakizungumza ndo unafahamu wazo lako kuomba ushauri kwao lilikuwa batili sana

Kuna Mzee mmoja alishika nyadhifa kubwa kubwa na kuheshimika nchini. Alipochukuwa fomu ya urais sikushangaa. Miaka zaidi ya Kimi baadaye Keira unsteady aliyepewa Klein kwenye Bodi moja nilikutana maybe kwenye kikao. Baada ys kumsikiliza sikuamini masikio yangu. Sikuona kabisa ile busara niliyotarajia. Kibaya zaidi katika kuropoka kwake alipotosha kikao na ikabidi aelezwe point blank!
 
ni vyema akajibiwa ili rekodi ikawekwa sawa hasa pale dhamira ya maneno yake anayotoa sasa ikiwa haieleweki
 
Back
Top Bottom