Spika Ndugai: Sheria ya kutaifisha ng'ombe wanaoingia hifadhini ni dhuluma. Ilipita tukiwa tumelala?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,167
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Sheria ya Serikali kutaifisha Ng'ombe wanaoingia maeneo ya Hifadhi ni tatizo, akiita kuwa Sheria yenye dhuluma.

Amesema, "Hii Sheria sijui ilipita wapi, tulikuwa tumelala au ilikuaje. Ile kwamba Ng'ombe wakiingia kwenye Hifadhi wanataifishwa wote, hapana! Kama ni ya miaka ya karibuni sijui nilikuwa nimesafiri nimeenda wapi".

Ameeleza, Tembo kutoka Hifadhini wanazurura na kula mazao ya watu akisema kuwepo usawa kwenye suala hilo na kuitaka Serikali kuliangalia.
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
1,336
2,000
Ndugai anatakiwa ajiulize kama umeweka sheria ya kutaifisha na bado watu wanaingiza mifugo, ukiitoa hiyo sheria je?

20210527_213348.jpg
 
Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
2,206
2,000
Watu takribani 400 wanapokaa na kufanya maamuzi ta hovyo hovyo. Kujua ng'ombe na mbusi ni sawa na nyumbu na swala wanao walinda kwenye hizo hifadhi imewawia vigumu. Ubaguzi wa kimaumbile wa wanyama.

Sheria hii itenguliwe maramoja wafugaji wspewe elimu ya jinsi ya kutunza mazingira. Wajue faida zake na umuhimu wa kufanya hivyo. Ziwepo faini za kumfundisha na wala si kumkomoa atakaye shindwa kutii.
 
mkaruka ataja rinu

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,541
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Sheria ya Serikali kutaifisha Ng'ombe wanaoingia maeneo ya Hifadhi ni tatizo, akiita kuwa Sheria yenye dhuluma.

Amesema, "Hii Sheria sijui ilipita wapi, tulikuwa tumelala au ilikuaje. Ile kwamba Ng'ombe wakiingia kwenye Hifadhi wanataifishwa wote, hapana! Kama ni ya miaka ya karibuni sijui nilikuwa nimesafiri nimeenda wapi".

Ameeleza, Tembo kutoka Hifadhini wanazurura na kula mazao ya watu akisema kuwepo usawa kwenye suala hilo na kuitaka Serikali kuliangalia.
Sijawahi kuona Spika mnafiki kama Ndugai tangu tupate Uhuru.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,038
2,000
Ni kweli kama anavyosema mwenyewe Ndugai kua walikua wamelala na sasa pengine ndio wanakurupuka kutoka usingizini!

Zipo sheria nyingi za hovyo na zakushangaza kama ile ya mtu akikutwa na hatia ya kusafirisha kilo 50 za mirungi anahukumiwa kifungo cha MAISHA jela! Kisa mirungi imewekwa kwenye kundi la dawa za kulevya.

Jambazi wa kutumia silaha au mbakaji wao ni miaka 30 tu jela. Lazima mtu uhoji utimamu wa afya ya akili ya waliotunga hizo sheria
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,752
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Sheria ya Serikali kutaifisha Ng'ombe wanaoingia maeneo ya Hifadhi ni tatizo, akiita kuwa Sheria yenye dhuluma.

Amesema, "Hii Sheria sijui ilipita wapi, tulikuwa tumelala au ilikuaje. Ile kwamba Ng'ombe wakiingia kwenye Hifadhi wanataifishwa wote, hapana! Kama ni ya miaka ya karibuni sijui nilikuwa nimesafiri nimeenda wapi".

Ameeleza, Tembo kutoka Hifadhini wanazurura na kula mazao ya watu akisema kuwepo usawa kwenye suala hilo na kuitaka Serikali kuliangalia.
This is a proof that the speaker is never serious!
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,322
2,000
Wazee wa kukurupuka kwa midundo na mapambio... utawala ukibadilika na wao wanabadilika tabia!!!
Tukirudi kwenye mada: Na wanyamapori wakiingia kijijini wataifishwe na kijiji au wenye mashamba kufidia uharibifu uliofanyika na uvamizi huo ".... au nasema uongo ndugu zangu?"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom