Spika Ndugai, Baadhi ya wanawake wakipewa cheo kazi yao inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani

Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Novemba 10, 2021 katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge wanawake.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi.

Spika amesema Taifa linaloongozwa na mwanamke linakuwa tulivu , amani na salama.

"Lakini kauli za baadhi zinaharibu taswira nzima, wengine mavazi yenu yanakuwa ya hovyo, ukipewa cheo kazi yako inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani jambo linaloharibu taswira ya viongozi wakuu wa nchi," amesema Ndugai.

Amewaagiza wabunge wanawake kujifunza kwa bidii mafunzo hayo kwani ushahidi unaonyesha waliojifunza walibadilika na kuwa viongozi mahiri.

Naye, Mwakilishi wa balozi wa Norway, Karen-Emilie Asla amesema mafunzo hayo ni kichocheo cha kumfanya mwanamke asijisikie mnyonge bali kila mtu anaweza kupewa nafasi.

Mwananchi
Yeye Ndugai anayo akili timamu? Anatishia watu na hana adabu.
 
Chifu hangaya hatoshi 😀😁
 
Bila kuwafokea Wadanganyika hawafanyi kazi!! Huoni sasa siku hizi ukienda maofisini yamerudi mambo yale yale ya zamanii ya kulembua macho ofisini badala ya kuwahudumua wananchi; wanajua hakuna lolote litakalowafaya wawajibike!!
Katiba mpya ni muhimu sana kuliko kufokeana
 
Back
Top Bottom