Spika Ndugai, Baadhi ya wanawake wakipewa cheo kazi yao inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Novemba 10, 2021 katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge wanawake.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi.

Spika amesema Taifa linaloongozwa na mwanamke linakuwa tulivu , amani na salama.

"Lakini kauli za baadhi zinaharibu taswira nzima, wengine mavazi yenu yanakuwa ya hovyo, ukipewa cheo kazi yako inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani jambo linaloharibu taswira ya viongozi wakuu wa nchi," amesema Ndugai.

Amewaagiza wabunge wanawake kujifunza kwa bidii mafunzo hayo kwani ushahidi unaonyesha waliojifunza walibadilika na kuwa viongozi mahiri.

Naye, Mwakilishi wa balozi wa Norway, Karen-Emilie Asla amesema mafunzo hayo ni kichocheo cha kumfanya mwanamke asijisikie mnyonge bali kila mtu anaweza kupewa nafasi.

Mwananchi
 
Binadamu ni binadamu tu,awe Me au Me.Uongozi bora na utawala bora hauna jinsia,ni hulka ya MTU tu kuwa na hayo aliyosema.

Hivi huwa wanatumia vigezo vipi kumwalika huyu mtu awe anawaasa watu wakati matendo yake hayaishi.
"Popote alipo akamatwe aletwe bungeni akiwa na pingu"
"Atake asitake titan hinge sea muda"
"Hawawezi kuniletea vipeperushi"
 
Kwa hiyo Ndugai ameamua kumvua nguo chifu Hangaya?

Maana hizo ndio sifa zinazomgusa moja kwa moja mama maushungi.
Naona unajaribu kuleta uchochezi Mkuu,ni wapi Job amemvua nguo Hangaya?ni wapi Hangaya amefokafoka wakati kauli zake ni kuwa yeye hafoki anatumia kalamu tu..

Nadhani huo ni mtazamo wako tu wala Mh Rais hayuko hivyo unavyotaka kutuaminisha.

Serikali ya kufoka foka ilikoma tarehe 17 march tulipotangaziwa ukuu wa alie juu,ambapo kila kiongozi alijaribu kufoka kadri ya uwezo wake kumfurahisha aliempa kazi.

Muache Mama achape kazi.
 
Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Novemba 10, 2021 katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge
Anayaona leo hayo mapungufu ya viongozi wateule?

Mbona hakuwahi kumkemea Bashite kipindi yupo anatesa watu ?
 
Back
Top Bottom