Spika Ndugai, Baadhi ya wanawake wakipewa cheo kazi yao inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani

Nzwangendaba

JF-Expert Member
Nov 9, 2019
306
500
Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.
...elimu
 

blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
5,726
2,000
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Huyu nafikiri anakula ugoro siku hizi..

Naona unamfaa aendelee nao.

Maana naona kama kataja tabia zake.
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,546
2,000
Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Novemba 10, 2021 katika ukumbi wa Pius Msekwa bungeni alipokuwa akizindua mafunzo ya uongozi kwa wabunge wanawake.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi.

Spika amesema Taifa linaloongozwa na mwanamke linakuwa tulivu , amani na salama.

"Lakini kauli za baadhi zinaharibu taswira nzima, wengine mavazi yenu yanakuwa ya hovyo, ukipewa cheo kazi yako inakuwa ni kufoka na kuweka watu ndani jambo linaloharibu taswira ya viongozi wakuu wa nchi," amesema Ndugai.

Amewaagiza wabunge wanawake kujifunza kwa bidii mafunzo hayo kwani ushahidi unaonyesha waliojifunza walibadilika na kuwa viongozi mahiri.

Naye, Mwakilishi wa balozi wa Norway, Karen-Emilie Asla amesema mafunzo hayo ni kichocheo cha kumfanya mwanamke asijisikie mnyonge bali kila mtu anaweza kupewa nafasi.

Mwananchi
Shughuli imeanza!! Hivi jiwe nae alivyokuwa akifoka na kufukuza watu...
Aaah niishie hapo siihoji jinsia.
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,371
2,000
Naona unajaribu kuleta uchochezi Mkuu,ni wapi Job amemvua nguo Hangaya?ni wapi Hangaya amefokafoka wakati kauli zake ni kuwa yeye hafoki anatumia kalamu tu..

Nadhani huo ni mtazamo wako tu wala Mh Rais hayuko hivyo unavyotaka kutuaminisha.

Serikali ya kufoka foka ilikoma tarehe 17 march tulipotangaziwa ukuu wa alie juu,ambapo kila kiongozi alijaribu kufoka kadri ya uwezo wake kumfurahisha aliempa kazi.

Muache Mama achape kazi.
Kwa mtizamo wako Job Ndugai alimaanisha/alimlenga nan??
 

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,316
2,000
Aliwalenga wote wenye tabia kama hizo alizozisema ila hakumaanisha wala kumsema Mh Rais wetu sababu yeye hana tabia hizo.
Aliyemuhukumu mbowe na kuiaminisha Dunia kuwa mbowe Ni Gaidi na ushahidi wanao wa kutosha Ni nani?

Anayepelekea kupindishwa kwa sheria katika kesi hiyo Ni nani?

Aliyetoa hongo ya madaraka baada ya kuona hyo kesi inakaribia kupigwa chini Ni nani?

Kifupi Hangaya ndiye anayelazimisha kumfunga Mbowe! Acha maCCM mtafunane , ila ukwel uko wazi kwa Kila mwenye akili!

Huyo Hangaya msimtetee, yeye ndiye anayewapa viburi wanawake wengine aliowapa mamlaka!
 

Kanyawela

Member
Aug 22, 2015
98
125
Dodoma. Spika wa bunge, Job Ndugai amewataka wanawake wenye mamlaka kutotumia vyeo vyao vibaya.

Spika Ndugai amesema mtu akipewa mamlaka halafu akaanza kuvimba na kushurutisha kwa kuwaweka watu ndani kwani kunawaondolea sifa ya kuwa viongozi.
Nyani haoni kundule๐Ÿ˜€
 

Afrikasana

JF-Expert Member
Oct 27, 2021
209
250
Ndugai mwenyewe mbona anatumia mamlaka yake kutoa watu ndani ya bunge?
Asiwaseme wanawake tena atulie maana huyo amegeuka kiroporopo kila hoja lazima achangie hasa za kuwaponda wapinzani
Ndugai Spika wa kuburuzwa. Anapitisha sheria leo mwezi ujao kaisahau
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom