Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Wangechapana tu bana! Kwanini watu kulazimishiwa mambo yaliyochakachuliwa kwa sababu ya wingi wa wabunge wa chama fulani.
Wabunge wa chadema sasa inawalazimu kununua viatu vyenye kisigino cha chuma. Kiwe na uzito ili kikirushwa kutoka nyuma kimfikie speaker maana anaendekeza u-ccm bungeni.
.
 
Anne Makinda hawezi kuongo bunge la kizazi hiki kwa kuonesha kuwa yeye yupo pale kwa masilahi ya chama cha mapinduzi. Sitta alikuwa muafaka kabisa kwani si tu kuwa anakubalika na wapinzani bungeni bali anaheshimika na watanzania wote kuwa ni spika wa kwanza kuruhusu michango yenye tija kwa wananchi. Anne alijua wazi kuwa kumfukuza Wenje bungeni kungeongeza hasira za wananchi dhidi ya CCM na hivyo hatua hiyo haikuwa na masilahi kwa CCM anayoiwakilisha.
 
Hii ni dalili muhimu kwamba spika Makinda hawezi kulimudu Bunge la kumi.Kuchapana bungeni ni dalili nzuri ya kuonyesha seriousness kwenye maswala ya msingi hasa unapodeal na wabunge wanafiki kama wa CCM.Jana wamepitisha kibabe muswaada wa SEZ na EPZ kwa kura huku wakipuuza mapendekezo ya msingi ya Mnyika kuhusu kuwashirikisha wawekezaji wadogo na wa kati.Mambo kama haya yanapopelekea wabunge kuchapana ni afya kwa bunge lenye wanafiki wengi ambao kazi yao bungeni ni kuropoka ndiyoooooooooooo!...bila kujua ndiyo athari yake ni nini!.
 
Tunataka liwe kama bunge la Kenya

Watanzania wamechoswa na Bunge la kuburuzwa na CCM. Nilitamani makonde yatembee ili kumaliza ubishi.
Mambo mengi yanayofanyika Bungeni chini ya uongozi wa CCM ni uhuni na ubabaishaji mtupu.
 
Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 13th April 2011

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, leo amepata wakati mgumu kuongoza kikao cha uchaguzi wa wajumbe kwenye taasisi mbalimbali za kibunge kwa kuwa wabunge walikuwa wanajibishana na kusababisha vurugu bungeni.

"Msitumie wingi wenu kutuburuza, mmezoea kutuburuza, tufunge mlango tupigane" walisema wabunge na kusababisha vurugu bungeni kwa takribani dakika kumi.

Mabishano hayo yalisababisha Spika akasirike na kuwaeleza wabunge kuwa walikuwa wanafanya mambo ya kijinga.

Vurugu hizo zilianza baada ya Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), kusema bungeni kuwa, mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi hizo ulifanywa kwenye dark market.

Wabunge wanaoaminika kuwa ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walishinikiza Mbunge huyo afute kauli yake, Makinda akamtaka Wenje afute kauli yake.

Wenje alisimama lakini hakufuta kauli yake, baadhi ya wabunge wakawa wanapiga kelele kushinikiza afukuzwe wakitumia maneno ‘out out out, atoke nje .

Wabunge hao walimtaka Mbunge huyo atoke, akanywe kikombe cha Babu, Loliondo.

Mara kwa mara Spika alilazimika kuwatuliza wabunge kwa kuwataka wamsikilize Mbunge aliyekuwa anazungumza.

Makinda aliwaeleza wabunge kuwa wanapaswa kutambua kuwa wananchi wamewachagua, na walikuwa wanawaangalia.

"Kwa nini mnafanya fujo isiyokuwa na akili… waheshimiwa wabunge tunafanya mambo ya kijinga" alisema Makinda lakini wabunge waliendelea kurushiana maneno.

Kwa mara nyingine Spika alimtaka Wenje afute kauli yake kwa kumweleza kuwa alikuwa amemtukana yeye Makinda na wajumbe wote wa Kamati ya Uongozi ya Bunge.

Alimweleza Wenje kuwa wao wote ni watu wazima na ni jambo la kawaida kwa Mbunge kufuta kauli bungeni.

Alimuuliza Wenje kwamba ingemgharimu shilingi ngapi kufuta kauli yake, na akamuuliza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kama Mbunge huyo angefanya hivyo, ingemgharimu kiasi gani.

Baadhi ya wabunge waliendelea kushinikiza Wenje afukuzwe, na kelele hizo zilizidi baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, kumweleza Spika kuwa ulikuwa wakati mwafaka kwake kumuamuru Wenje atoke nje ya Bunge.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alisema ni kweli Kamati ya Uongozi ya Bunge ilikutana kuzungumzia suala hilo, lakini hazikutolewa fomu ili wagombea wajaze.

Zitto alisema, kamati hiyo si dark market lakini haikuwa sahihi kuitafsiri visivyo kauli ya Wenje, wao (wabunge) wote ni wanasiasa, wawe na ngozi ngumu.

Baadhi ya wabunge waliendelea kusisitiza kuwa Wenje atoke, Zitto akawajibu kuwa hatoki, na wabunge wengine wakasema "hatoki mtu, tutatoka wote"

Makinda alimpa Wenje fursa nyingine ya kufuta kauli yake, Mbunge huyo akasema, hakusema Kamati ya Uongozi ni dark market, ila alimaanisha mchakato uliotumika, ma mwishoni akasema, anafuta maneno dark market, anaweka white market.
Hii ndio aina ya wabunge tulionao kwenye Bunge letu wanaowakilisha wananchi kazi kweli kweli
 
Makinda ana gamba gumu lisilovulika? Tutaona deadline ya siku 90 walotoa waoem
 
Naam waache wachapane tu, na kama CDM wanataka msaada basi kuchapana huko kutaendelea mpaka uraiani. Watanzania tumechoshwa na Bunge la usanii linalotetea upuuzi miaka nenda miaka rudi.

Mkuu umenifurahisha kwa kuonyesha hisia zako, ni kweli umefika wakati wananchi tuanze kuchukua hatua....
 
Makinda ana gamba gumu lisilovulika? Tutaona deadline ya siku 90 walotoa waoem

Ni bora wangepigana kaka maana Makinda haeleweki ni mtetezi wa chama kimoja badala ya kutetea vyama vyote Bungeni
 
Ni bora wangepigana tu maana maneno yamekuwa hayatoshi kueleza ukweli
 
There are currently 190 users browsing this thread. (71 members and 119 guests)
Yaan huku bunge linaendelea Zitto yuko JF, Je kweli tuna wabunge?
natamani sana Zitto awe mbunge wangu,mimi mbunge wangu sijui hata kama anaijua internet hajui kitu kinachoendelea duniani anajua kusoma tu magazeti nina huo uhakika. Na zitto kuwa hapa online inawezekana aliacha computer yake au simu yake ikiwa online, so sio shida kabisa na wala hakuna tatizo lolote , nyie watu wa ccm mnataka muerevuke nyie tu ili meundelee kutuibia sio
 
Back
Top Bottom