Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Dopas na Mwera hapo hamjasema kitu chochote cha maana. Mnashindwa kutuambia hoja Wenje ilikuwa nini. Wenje alizungumzia kanuni kukiukwa na kamati ya uongozi ambapo haina mamlaka ya kufanya hivyo. Alichokosea Wenje ni kutumia neno 'dark market' na ndicho alichofuta na badala yake akaweka 'white market'

Hivyo hoja yake ya kuwa kanuni imekiukwa kwa utashi wa wajumbe wa kamati ya uongozi bila kuwa na uwezo huo lilibaki hadi kanuni ilipotenguliwa kwanza na uchaguzi ukafanyika.

Kwa hiyo Dopas na Mwera mmetuletea ushabiki badala ya kujadili hoja ya Wenje na msimamo wenu juu ya hoja hiyo kwa kuzingatia kanuni za bunge. Hivyo nawataka mwufute kauli zenu za kipotoshaji.
 
Hapana Mkuu Dopas, hiyo ndiyo siasa iliyokomaa. Kutoa tamko bungeni na kuthdraw inapolazimu ni turufu kubwa ya kisiasa inayotumika kwenye bunge nyingi duniani na ina maana pana zaidi ya unavyotaka kuwasilisha hapa. Alichofanikisha Mhe. Wenje ni kwamba pamoja na kuombwa kufuta kauli yake hiyo lakini ukweli ni kwamba ujumbe umefika au kwa king'eng'e message sent ! Zaidi ya hapo tukio hili limezidi kutufumbua macho jinsi wabunge wa CCM wasivyo wavumilivu na wastahimilivu mjadala unapokuwa mkali. Hakukuwa na haja ya kupiga kelele kama wahuni kwa kumtaka mbunge mwenzo, Mh. Wenje, atolewe bungeni - hilo linawezekana tu hapa kwetu kwa sababu bunge linaendeshwa ki CCM zaidi.
 
wengine mara eti tupigane, wengine hao wapinzani, wengine hao ccm!! ahahahahah, mi nimeipenda sana hii.

Mara wengine CCM mnatuburuzaaaa!!!!!, mara wingi wenu ndo unatunya mtuburuzeeee!!!!! VERY INTERESTING SCRIPT KWA KWELIII!!!!................ila Kwa mtazamo wangu naona kama Spika BUNGE limeanza kumshindaaaa!!!!!! HAYO NO MAWAZO YANGU LAKINI....
 
elimu ya spika ni ya kuchakachua nini? dark means our skin....alivyosikia white market kafurahi so spika anapenda kuwa mzungu sio?
 
Tena hafai Makinda Kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kuna watu ana wa defend Saaaaaaaana

Kama kuna siku kama mbili kwa walioona bunge wiki ilipite kam tetea saaaaaana Ngeleja huku alikwa anajibu visivyo

tena atokeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
sijaona bunge lakijinga kama hili, watu hawaongelei maslai ya taifa wamekalia upumbavu wa kimabavu wa upinzani wao wa kivyama
upuuzi mtupu, sio ccm wala cdm
 
mtu anashindwa kumwandikia Rais Hotuma Ya Maana, wizara au chama ndo ataweza kuongoza? Kipindi "Mwezi-Wa-Kwanza" ma-ropes anamwandikia JK hotuma, hotuba za mkuu wa Kaya zilikuwa hovyo kweli... iweje leo mtu aseme ana uwezo wa kuwa waziri au katibu wa chama? Wana Bumbulii-taa, mmeliwa.... habari ndo hiyo
 
Nimependa Bunge hili ni ushindani jinsi ulivyo juu! Nilicheka zaidi mmoja alisema kwenye mic eti spika funga mlango tupigane humuhumu! Hahahahahhaaahahahahahaahahha!! Wabungeee teh
 
Mtaniwia radhi waungwana kwa lugha nitakayotumia juu ya huyu mpuuzi aitwae Werema maana nina hasira kali. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muunganowa Tanzania, MWanasheria mkuu ni mshauri mkuu wa serikali kwa mambo yanayohusikana na sheria (rules, regulations, and lws/legislation) ili kuisaidia kufanya maamuzi yaliyo na faida kwa watanzania (national interests). Cha kushangaza ni kwamba huyu punguani amekuwa bega kwa bega kuwasaidia mafisadi katika kampeni yao ya kuwadidimiza mafisadi kila leo.

Kwanza kabisa huyu mbumbumbu alikuwa fisadi wa kwanza kabisa kuropoka hadharani kuwa lazima DOWANS ilipwe maana hakuna jinsi. Akadai ameisoma hukumu kwa kirefu na kukuta hakuna jinsi zaidi ya DOWANS kulipwa. Ukweli ni kwamba hata rais wake ambaye ndio FISADI namba moja Tanzania amepiga breki kwenye hilo maana anajua watanzania japo ni vipofu wameibiwa vya kutosha mpaka wameanza kuuona huo wizi wenye ilhali hawana macho (refer to Chinua Achebe's Man of the People).

Kinachoniuzdhi zaidi ni kwamba majuzi pale bungeni huyu mpumbavu alijifanya kudai kuwa amevumilia vya kutosha sasa anaamuru askari wa bunge (Sajent of Arms) amtie nguvuni Mheshimiwa Wenje eti amekiuka kanuni za bunge kwa kudai kanuni zifwate na wabunge uhario wa CCM. Hivi huyu mbwa anajua hata sheria zikoje? Amesoma sheria kweli? Hivi anajua kwamba kanuni za bunge (standing orders) hazitakiwi kukiukwa mpaka zisimamishwe na bunge lenyewe? Najiuliza kama anatetea kuvunja kwa kanuni wakati alitakiwa ahakikishe kanuni zinatekelezwa na serikali kazi yake ninini? Nasema wazi na nasisitiza, huyu mbwa hafai kuwa mwanasheria mkuu Tanzania. Nipandikizi lililowekwa kutetea mafisadi. There I have said it! Temea mate chini!!!!
 
Jamani kuna siri gani? kwa nini wabunge wa CCM kwenye kikao cha jana cha bunge wakati wanataka Ezekiel Wenje wa CHADEMA atolewe na Zito Kabwe akawa anamtetea, wakatumia maneno haya:

" Zito TUNAKUHESHIMU, atoke".

Hapa sipaelewi kabisa! Zito anaheshimiwa lakini Wenje atoke, au Zito tunafahamiana wewe mtu wetu acha huyo asiye wetu atoke. Au kuna heshima gani hapo? Na kusema hivyo ilikuwa ni kumtishia Zito kwa lipi? kwamba atoke, "or else!"??????

Mods mnaweza kuiamisha lakini niliona niiweke hivi nisaidiwe mawazo hapa, hapa imenichanganya sana hii.
 
Huyu jamaa ni bure na ndipo utakapoona kuwa mahakama zetu zimejaa aina hii ya majaji - kuteuliwa kwa ushikaji bila kujali uwezo na credentials.
 
alipata kiti cha bumbuli? au "mshua" ali cheza karata zake kwenye kura za maoni?
 
Jamani kuna siri gani? kwa nini wabunge wa CCM kwenye kikao cha jana cha bunge wakati wanataka Ezekiel Wenje wa CHADEMA atolewe na Zito Kabwe akawa anamtetea, wakatumia maneno haya:

" Zito TUNAKUHESHIMU, atoke".

Hapa sipaelewi kabisa! Zito anaheshimiwa lakini Wenje atoke, au Zito tunafahamiana wewe mtu wetu acha huyo asiye wetu atoke. Au kuna heshima gani hapo? Na kusema hivyo ilikuwa ni kumtishia Zito kwa lipi? kwamba atoke, "or else!"??????

Mods mnaweza kuiamisha lakini niliona niiweke hivi nisaidiwe mawazo hapa, hapa imenichanganya sana hii.

Kionambele, Zitto amejijengea heshima ya kuwa miongoni mwa wabunge wachache ambao wako over and above partisan politics kwa ku focus on national interest. Ni mkweli daima, natumaini unakijua kinachowafika watu wakweli daima. Tafuta kitabu cha 'An Enemy of The People' ukisome, ndipo utamwelewa Zitto, amesimama wapi na anasimamia nini.

Jana alimtetea Wenje kwa kuwataka wabunge wawe waelewa zaidi.
 
"Tatizo jingine ninyi wa Chadema ni kwamba huwa mmejipanga kwamba huyu akazungumze hiki na huyu akazungumze kile kwa hiyo mnakurupuka sana wakati mwingine." ni baadhi ya maneno aliyotoa spika Makinda bungeni,hata kama mimi sio mfuasi wa chadema,naona bunge lisitumike kwa maslahi ya kundi fulani hii inaonyesha huyu mama hayuko makini,ushauri wangu wa bure huyu mama ajivue gamba mapema kabla bunge halijazidi kuharibika
 
Back
Top Bottom