Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Ushabiki wa wabunge usio angalia masilahi ya wengi huleta sononeko baadaye kwa wao wenyewe watakapojua ukweli na kwa wanachi kwa ujumla. Sasa hivi naona kinachofanyika ni mzaha tu.
 
In English, there is no such thing as "Dark Market". So much ado about nothing.

Hebu tuache mbwembwe. Tuongeze bidii, hii ni Dunia ya elektronik kila siku kuna mapya. Usinga'ang'aniye Webster's Dictionary.

[snip] .... Sometimes the term dark market is used to describe secretive, unregulated (though often technically legal) trading in commodity futures, notably crude oil in 2008.[3] This can be considered a third type of "grey market" since it is legal, yet unregulated, and probably not intended or explicitly authorized by oil producers. .........[snip]

Ref.
Grey market - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Kwa wenye access ya TV, watch TBC live, Spika Mama Makinda anachezea kibano kuhusu kanuni!
Sio siri, Spika Mama Makinda, Bunge linamshinda!

Bibi yaga yamemshinda
 
Waendelee na upuuzi wao huohuo, hizo si zilikuwa njama za CCM kumtoa Sitta? Sasa huyo Mama Makinda ya ndege atakoma kulinga mwaka huu,! Itabainika tu, alidhani wabunge mavuvuzera? Ngoja wampeleke peleke kwanza!
 
Mh. Wenje pamoja na kukosea kwa kusema black market (soko la magendo) spika hatuna. Ilibidi atoe ufafanuzi wa uhalali wa mkiti na mweziwe kuteua. Poor tanzania bunge hatuna kwa staili hii sheria kutunga na kuisimamia s.kali. I wish .....
 
Watabana, watabana, wataachia. Treni ya ukombozi wa Mtanzania ilishaondoka kwenye kituo.
 
Ujue huyu mama pamoja na kuwa ana miaka 35 bungeni bado nasema kuwa hata ile kauli ya wanawake wakiwezeshwa wanaweza haijamsaidia niseme ili tufikie kwenye malengo watanzania tusijaribu kucheza na maisha yetu..huyu mama anajaribu sio kwamba yuko kazini kama wanaume tunapikuwa kazini na katika nyazifa hizo.
 
kwa mtaji huo kuna siku watapigana kama wale wa kenya tena siku si nyingi
 
wana jamvini mnamzunguziaje? Ezekieli wakati ana changia hoja bungeni pale aliposema process ya kuwachagua wenye viti ilikuwa kama Dark market enzi za mwinyi? Na je maamuzi ya spika yakumtaka afute kauli yalikua sahihi?
 
[video]http://dullonet.com/2011/04/13/tbc-kipindi-cha-harakati-13-04-2011/[/video]

Wadau sikilizeni hiki kipindi Spika alipoonja Joto ya jiwe baada ya kuzani kuwa wabunge wa sasa ni kama wale wa akina ndio mzee!
 
wengine mara eti tupigane, wengine hao wapinzani, wengine hao ccm!! ahahahahah, mi nimeipenda sana hii.
 
Alilofanya Mheshimiwa Wenje jana limetupatia tafakari kubwa....

Kwa maoni yangu amekukurupuka..... Ataweza kuvaa vizuri 'viatu' ya dhamira ya Chadema chama makini?

Wabunge wana nafasi ya kutosha kuandaa hoja, au michango na maswali, hakuna anayekimbizwa.

Kwanini alitoa hoja asiyokuwa na uhakika nayo? Kama alikuwa na uhakika nayo kwanini ali-withdraw?

Kwani kutolewa nje ya Bunge kutamgharimu nini ikiwa anachosema ndiyo kilicho sahihi?

Kama alichosema sicho kilicho sahihi kwanini alisema? Kwani ni lazima kusema kuchangia kama hana mchango? Anamfurahisha nani? Bado maswali ni mengi...

Chadema ni chama makini inayohitaji watu makini, sio wa kukurupuka... kwa mtindo huo nina mashaka na safari ya kuwakilisha wana Nyamagana.

Kama aliteleza labda atajirekebisha kwa faida ya wapiga kura wake, chama chake na watanzania kwa ujumla
 
Hana lolote wenje mropokaji namsema hovyo tu amezoea mambo ya vijiweni,hata huo ushindi alioupata nikwasababu yakura za chuki watu walizopiga dhidi ya masha hata wana ccm hawakumpa kura masha walitaka aanguke,nakupa 100% wenje hapati tena kura nyamagana amini usiamini,amalize mdawake watu watafte anaewafaa.
 
Back
Top Bottom