Spika Job Ndugai: Matatizo yetu na Prof. Mussa Assad ni kutuita dhaifu, alitakiwa ajiuzulu. Hatuna tatizo na ripoti yake, tutaifanyia kazi

Nimeshangaa sana Spika kumtaka CAG ajiuzulu,
SIO kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake, Ila na kwa kuwa tu amekosoa mwenendo wa konokono wa Bunge katika kuisimamia Serikali dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za Umma.!

Kweli aliyemloga Ndungai kafwaa!
 
Proving his naivity, it's better to let us think he is an Idiot than to open his mouth and prove it, he is empty headed
 
pale job anaporopoka bila kushirikisha kichwa cha juu,,dr wa coral show
lakini pia amesema neno likitamkwa kwa kiingereza au kwa kiswahili linaleta uzito tofauti.
amesema wao hawalitaki hilo neno, kama CAG analipeeenda sana basi ajiite yeye Prof. Dhaifu, bunge wamekataa hilo jina la kejeli.
Lakini pia amezungumzia kasumba ya wasomi wa kibongo kujiita prof, Dr, NK kila sehemu kuwa ni ushamba, pia kujiona wewe mjuaji saana kwakua tu ni profesa huo ni undezi.
(nadhani dakta JPM pia aache kuitwaitwa Dr, ni ulimbukeni)
busara ni CAG kuwaomba radhi wabunge kwa kuwakwaza kisha maisha yaendelee.
 
Boss Ghazwat Yaani neno "Dhaifu" linabebewa Bango hivi???!!!
Kiongozi anaombwa ajiudhuru uongozi kwa sababu la neno dhaifu???!!!
Ilitakiwa wampe Onyo au Adhabu na sio ajiudhuru.
Mimi nafikiri kuna kitu nyuma ya pazia aisee,
Au anataka kutu distraction wananchi, labda wanataka tusijadili Report,
Tujadili Spika Vs Prof Assad,
Inaonyesha Prof Assad kaishika sana Dini aisee.



Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Aprili 14 atazungumza na waandishi wa habari jambo muhimu kuhusu bunge.

Mazungumzo hayo yatafanyika katika ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es salaam majira ya saa sita na nusu mchana.


=====

UPDATES:

View attachment 1071319

=> Spika Ndugai: CAG anaposema mbele ya umma kuwa ataendelea kutuita 'dhaifu' wakati ni jina ambalo hatulipendi na tumelikataa, tunashindwa kumuelewa kama analipenda sana ajiite yeye. Sasa kusema unaendelea kutumia endelea na nitakuita tena na safari hii itakuwa mbaya zaidi"

=> Spika Ndugai: "Namwambia ndugu yangu Prof. Assad hilo neno aliache, sisi taarifa tumeipata na tutaifanyia kazi. Msisitizo wetu ni mmoja, kwakuwa bunge lilishapitisha uamuzi wa kutofanya kazi na Prof. Assad ni uamuzi halali"


=> Spika Ndugai: "Sina chuki binafsi na Prof. Assad, yule ni ndugu yangu na ni mtanzania mwenzangu tatizo ni lugha anayoitumia na nisinhependa itufikishe hapa kama taifa."

=> Spika Ndugai: "Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au laaa!. Maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai: Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake,

=> Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amewahakikishia watanzania kuwa bunge linaendelea vizuri na kazi yake ya kutunga sheria, uwakilishi, kuisimamia Serikali pamoja na mipango ya nchi ikiwemo suala la bajeti ambalo linaendelea bungeni.

=> Spika Ndugai:“Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza

=> Spika Ndugai:Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai:Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai:Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo inayotajwa kuwa ya kihasibu.

=> Spika Ndugai: “Hata katika maisha ya kawaida, we unamuita mtu jina flani, anakwambia bwana tafadhali jina hili silipendi, lakini unaendelea kumuita na kuahidi utaendelea kulitumia, ni ustaarabu duniani?”

=> Spika Ndugai: “Katika kutekeleza majukumu yake #CAG hakupaswa na hapaswi kulitukana #Bunge kwa lugha zile za rejareja. Bunge huangalia taratibu zake na kuendesha mambo yake kufuatana na kanuni za Bunge…lile Bunge lenyewe hawezi kulikagua”

=> Spika Ndugai: Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai: “Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza”

"Nilipokuwa sipo kuna mambo mengi yamezungumzwa, na mengine yameandikwa kuhusu Ripoti ya CAG. Nitakapokuwa Dodoma nitaagiza ripoti ipelekwe kwenye kamati za PAC na LAC"




Zaidi soma.....

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akamwone Rais John Magufuli ili mzozo wake na Bunge uishe.

Kauli ya Spika inakuja wakati tayari Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad bali ofisi ya CAG.

Spika Ndugai aliyekuwa ziarani nchini Sweden wiki iliyopita ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 14, 2019 akieleza kusikitishwa na hatua ya Profesa Assad kurudia neno udhaifu kwa Bunge alipotoa taarifa yake hivi karibuni.

"Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake," alisema Ndugai.

Ameongeza kuwa hata bajeti inayojadiliwa na Bunge lazima ipitishwe na Rais. Amesema kwa kuwa Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad alitakiwa ajiuzulu.

"Kwa kuwa Bunge likishaaamua kuwa halifanyi kazi na mtu, ni uamuzi halali. Katika nchi zote Bunge likishakosa imani na wewe unajiuzulu," amesema.

Ameongeza, "Sasa hatumfundishi kazi Mussa Assad, anampa wakati mgumu Rais tu. Tutafanya kazi na ofisi ya wananchi."

Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.

Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.
 
Stupid comment. Kwetu sisi ni spika wa Binge la JMT. We hold and judge him at that capacity. Otherwise, let him resign and remain a member of Parliament from Kongwa constituency.
isingekuwa wananchi wa kongwa angepataje cheo cha speaker..
 
Wachamungu wote wa dini zote na wa makabila yote na wa vyama vyote wamesimama na Mtu wa Mungu Prof.Assad mteule wa Rais anayelindwa na Katiba.

Nadhani hata Rais amekua Mara kwa Mara akisema tumuombee ili atende kwa kumtanguliza Mungu.
Prof.Assad Anatenda kwa kumtanguliza Mungu.
Ndugai anatanguliza kujipatia sifa na Heshima kwa kuwalinda Madisadi kupitia bunge



Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe Assad angekuwa na hofu yaMungu biashara hii ya kungangania kuwaita wenzake madhaifu angeshaifutilia mbali kule.wenzaki hawapendi hilo neno linawadhalilisha, tena wengi wale wabunge, yeye mmoja tu , kwanini roho wa Mungu asingemuongoza na busara kutawala na aamue kushit hilo neno na kujirudi..whyyyy...ni kiburi cha nini, hicho, ndio cha uprofesa au.. hana hofu ya Mungu huyu mtu...
 
Nimesoma taarifa inayohusu spika kumfananisha CAG Assad na mbwa anayemtukana mtu anayemlisha kwa mkono wake.Hapa spika ameonyesha udhaifu wake kwa kumjia juu CAG na kumtolea maneno ya kashfa moja kwa moja. Huu ni udhaifu na kweli ameshindwa kabisa kuelewa taaluma ya uhasibu inasema nini katika strengh na weakness ya kiukaguzi. Spika hafai anafanyakazi kwa maelekezo toka mahala fulani sasa baada ya kuona kikatiba amemshindwa anatoka povu na kutamka bayana kuwa lengo la bunge ni kutaka CAG Assad ajiuzulu. Shame on speaker. Anashindwa kulisimamia bunge na anafanyakazi kwa amri toka mahala fulani kiasi kwamba hataki ukaguzi wa matumizi ya pesa ya umma. NASEMA KAMA KUJIUZULU BASI SPIKA AJIUZULU KWA KUHUJUMU PESA ZA UMMA KWA POSHO ALIYOPATA AKIWA INDIA NA KUSHINDWA KUONGOZA BUNGE KIKATIBA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss Ghazwat Yaani neno "Dhaifu" linabebewa Bango hivi???!!!
Kiongozi anaombwa ajiudhuru uongozi kwa sababu la neno dhaifu???!!!
Ilitakiwa wampe Onyo au Adhabu na sio ajiudhuru.
Mimi nafikiri kuna kitu nyuma ya pazia aisee,
Au anataka kutu distraction wananchi, labda wanataka tusijadili Report,
Tujadili Spika Vs Prof Assad,
Inaonyesha Prof Assad kaishika sana Dini aisee.
dini ndio inamuongoza Assad kuwaita wenzake dhaifu...?walahi hata ningekuwa mimi nisingekubali..hata wewe...tunashangaa mtu mzima amengangania neno utafikiri linampa maisha hapa duniani...Waswahili wanasema.wengi wape..hana hata busara ya kutafuta solution ya hii kitu..maajabu sana
 
Mkutano wa ndugai na wanahabari na ukichunguza aliyoyasema ni dhahiri ametumwa na mtu akayaseme hayo. Kosa kubwa la CAG ni.kungusa mtu ambaye anataka aonekane malaika kumbe ni mpigaji mzuri. Mtu huyo hapendi kukosolewa wala kushauriwa na yuko tayari hata kutoa uhai wa wakosoaji wake.
Wizi wa 1.5 mpaka 2.4 tln inaonekana umegusa mahali pake na sasa kinatafutwa njia za kumuondoa CAG ili waweke mtu wao atakayeficha uhalifu wao. Wenye akili wataelewa ila wale walevi wa bangi na gongo watapinga
 
Leo ndio nimejua CAG ni mtanzania pekee nchi hii asiyetakiwa kutoa maoni yake.
Uhuru uko wapi?... Vipi angesema bunge linafanya kazi vizuri, napo angeitwa kuhojiwa??!!
Ccm Mungu sio demu wenu eti hamna hofu nae ... Endeleeni na ujinga wenu... MTALIPWA ONE DAY
 
Boss Ghazwat Yaani neno "Dhaifu" linabebewa Bango hivi???!!!
Kiongozi anaombwa ajiudhuru uongozi kwa sababu la neno dhaifu???!!!
Ilitakiwa wampe Onyo au Adhabu na sio ajiudhuru.
Mimi nafikiri kuna kitu nyuma ya pazia aisee,
Au anataka kutu distraction wananchi, labda wanataka tusijadili Report,
Tujadili Spika Vs Prof Assad,
Inaonyesha Prof Assad kaishika sana Dini aisee.
dini ndio inamuongoza Assad kuwaita wenzake dhaifu...?walahi hata ningekuwa mimi nisingekubali..hata wewe...tunashangaa mtu mzima amengangania neno utafikiri linampa maisha hapa duniani...Waswahili wanasema.wengi wape..hana hata busara ya kutafuta solution ya hii kitu..maajabu sana
 
Back
Top Bottom