Spika Job Ndugai: Matatizo yetu na Prof. Mussa Assad ni kutuita dhaifu, alitakiwa ajiuzulu. Hatuna tatizo na ripoti yake, tutaifanyia kazi

Kwanza audit queries huwa zinawasilishwaga kwa mara ya kwanza ktk exit meeting hapo mnajibuuu wakaguzi wakiridhika na majibu yenu wanaziondoa queries walizoridhika na majibu yake. Zile ambazo hawajaridhika nazo labda kwasababu ya kukosa ushahidi wanaenda kuziandika rasmi na kuwaletea tena ktk maandishi ili mjibu rasmi na kuweka vithibitisho. Hapa wakaguzi hutoa muda wa kutosha kwa Taasisi husika kujibu hoja.

Baada ya Taasisi kujibu hoja za wakaguzi na kutoa vielelezo au vithibitisho, hoja zote zilizotolewa majibu na vielelezo vya kutosha hufutwa. Lakini, hoja ambazo hamjatoa majibu ya maana au vithibitisho zinasonga mbele, yaani maana yake mmeshindwa kuzijibu, hivyo zinasonga mbele, ndo hizo zinazoenda ktk ripoti ya CAG. Kwahiyo kuziita queries kirahisi rahisi tu sio sawa, ingawa ni kweli zipo zinazoweza kwenda kupata majibu zikiwa ktk ngazi ya Bunge, lakini asi simplify hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sote ni shahidi juu ya mtanange unaoendelea kati ya bunge letu na CAG, hv wana JF km msimamo huu ungewekezwa zaid katika kuhakikisha wanaisimamia serikali (ambayo ndio kazi ya bunge) tungekua wapi hadi leo.

hv malumbano hayo ya spika juu ya CAG yanatij gani kwa taifa. Ingependeza leo tungesikia namana anavyoitaka serikal ijibu hoja za CAG na si kung'ng'ania lisiitwe bunge dhaifu tuu.

MiM
 
Basi sawa,Assad ataamua kuchuja kati ya maoni yangu na yako yepi sahihi,sisi kwa maana ya mimi na wewe tumetimiza wajibu wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani nimesikiliza spika nikachoka kabisa.. Mtu kama huyu Nani alimpa mamlaka ya kuongoza muhimili muhimu kama bunge? Eti ajiongeze ajiuzulu.. Kwa nini yeye Ndugai asijiuzulu kwa kushindwa kuongoza bunge anataka CAG ndio ajiuzulu? Sisi wananchi tulio wengi tuna Imani na CAG Prof Assad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliposema zile ni 'audit query' tu,ndipo nilipojua Prof. Assad hawezi hata kumjibu tena maana anapoteza muda wake tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah.....Queries hujibiwa na kuwa resolved during the audit process wakati zile zinazotolewa reports ni audit findings.

Kwamba polisi wamelipa 16b kwa manunuzi ya sare ambazo hakuna ushahidi wa kuwepo order ya manunuzi wala delivery siyo audit query, hiyo ni audit finding....and fingers can correctly be pointed kwa walioidhinisha malipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Stupid comment. Kwetu sisi ni spika wa Binge la JMT. We hold and judge him at that capacity. Otherwise, let him resign and remain a member of Parliament from Kongwa constituency.
 
Naona huyu speaker ana-ramble anachoongea hakileti sense. Kama hataki kufanya kazi na CAG mbona ripoti yake bunge inaifanyia kazi, sasa kwanini ajiuzulu? Ushauri wangu ni wafanye kazi na CAG Prof. Assad hadi atakapostaafu kwa sababu sioni impact yoyote CAG Assad akiwepo....Watafanyia kazi tu hiyo report maana CAG akipeleka ripoti IKULU, kutoka kule anapeleka mtu mwingine, sasa kuna shida gani hapo?
Watanzania wengi waliopo nje wanahitaji uraia pacha kwa faida ya nchi yetu....Siyo kweli hayo anayoyasema kuhusu uraia pacha (Dual Citizenship), wameuomba tangu enzi za Kikwete lakini serikali ya Tanzania imekuwa ikiwadharau, wana-diaspora wana faida kubwa hasa kwenye money remittance, ni vyema wakawapa uraia pacha kuliko kuvamia Bureau De Change na kunyang'anya pesa huko. Watanzania wote waliopo nje wanahitaji uraia pacha ili wawe na uhakika na miradi na mali watakayowekeza nchini...Wamechoka kukataliwa na kutishiwa kuambiwa kuwa HAWANA HAKI YA KUMILIKI ARDHI, Wenzetu Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanaruhusu uraia wa pacha...sisi tunakataa kwa sababu ambazo hazina maana...Waacheni watanzania wafurahie nchi yao, LUKUVI anawaita waliojiripua kumbe hata knowledge ya watu kukaa nje hana. KWANI WATANZANIA WANAOISHI NJE WAKIKUBALIWA URAIA PACHA TUTAPOTEZA NINI? Ndugai acha nia ovu.
 
Asikubali kabisa kabisa hata kama Spika anatumiwa na mafisadi na wezi wa Mali za umma.

Bunge kama lilishindwa kumwadhibu mkosaji mwenye makosa ya kijinai ya vyeti feki Leo linataka kumwadhibu mtu mwadilifu anayelinda fedha za walipa Kodi kwa sababu mafisadi wanataka kuivuruga serikali kwa mgongo wa bunge kwa kumtumia Jobman.

Rais atapambana vipi na ufisadi bila kuweka MTU mwadilifu aliyejitoa muhanga kulinda rasilimali za umma kwa uaminifu?

CCM ijitafakari vizuri 2020 ,Ndugai asipewe tena nafasi apumzike amwachie yule kada mwenzake aliyejaribu kumuua kwa kumpiga gongo mpaka akapoteza fahamu.
Kama CCM kingekua ni chama kinachojali utu na uhai wa binadam ile ilikua ni sababu tosha ya kumwengua Ndugai na hata kumnyima uspika.
Ni Tanzania tu watu wanaotumia silaha za marungu kuwazupiga wanasiasa wenzao ndani ya chama kimoja wanapewa nafasi ya kugombea na hata kuongoza muhimili mkubwa unaotegemewa kutunga sheria za haki za binadam na utawala bora.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hii issue bunge lipo at mercy ya CAG,speaker analialia tuu aache kutuita hivyo😃😃 hawana cha kumfanya.
 
Anatumiwa na mafisadi na wezi wa Mali za umma na pesa sa walipa kodi.
Kuna watu wamezoea kupiga sana pesa za umma kwa miradi feki.
Walizoea kuwahonga Walachizi lakini kwa Prof. Assad amegonga mwamba kwa uadilifu wake ,sasa wameamua kumtumia Spika na bunge lake ili wamdhibiti CAG na kuwatisha waadilifu wote ili waamini kuwa uadilifu wao hauna manufaa kwao binafsi.

Mbona yeye amemtukana CAG kwa kumfananisha na mbwa?
Nduu gay hajui hata Lipi lenye manufaa kwa umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…