Spika Job Ndugai: Matatizo yetu na Prof. Mussa Assad ni kutuita dhaifu, alitakiwa ajiuzulu. Hatuna tatizo na ripoti yake, tutaifanyia kazi

Kwanza audit queries huwa zinawasilishwaga kwa mara ya kwanza ktk exit meeting hapo mnajibuuu wakaguzi wakiridhika na majibu yenu wanaziondoa queries walizoridhika na majibu yake. Zile ambazo hawajaridhika nazo labda kwasababu ya kukosa ushahidi wanaenda kuziandika rasmi na kuwaletea tena ktk maandishi ili mjibu rasmi na kuweka vithibitisho. Hapa wakaguzi hutoa muda wa kutosha kwa Taasisi husika kujibu hoja.

Baada ya Taasisi kujibu hoja za wakaguzi na kutoa vielelezo au vithibitisho, hoja zote zilizotolewa majibu na vielelezo vya kutosha hufutwa. Lakini, hoja ambazo hamjatoa majibu ya maana au vithibitisho zinasonga mbele, yaani maana yake mmeshindwa kuzijibu, hivyo zinasonga mbele, ndo hizo zinazoenda ktk ripoti ya CAG. Kwahiyo kuziita queries kirahisi rahisi tu sio sawa, ingawa ni kweli zipo zinazoweza kwenda kupata majibu zikiwa ktk ngazi ya Bunge, lakini asi simplify hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sote ni shahidi juu ya mtanange unaoendelea kati ya bunge letu na CAG, hv wana JF km msimamo huu ungewekezwa zaid katika kuhakikisha wanaisimamia serikali (ambayo ndio kazi ya bunge) tungekua wapi hadi leo.

hv malumbano hayo ya spika juu ya CAG yanatij gani kwa taifa. Ingependeza leo tungesikia namana anavyoitaka serikal ijibu hoja za CAG na si kung'ng'ania lisiitwe bunge dhaifu tuu.

MiM
 
Uislamu ni dini ya salama na amani lakini ina kanuni na taratibu zake.Kwanza dini hii hairuhusu kumnyenyekea au kumpigia mtu magoti kwa kuhofia uheshimiwa wake.Pia muislamu anatakiwa kusimamia haki hata kama atabaki peke yake.Sasa Profesa Assad bila shaka anajua haya,hakuna kuomba radhi kwa kuwa tu ukweli umewauma waheshimiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi sawa,Assad ataamua kuchuja kati ya maoni yangu na yako yepi sahihi,sisi kwa maana ya mimi na wewe tumetimiza wajibu wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani nimesikiliza spika nikachoka kabisa.. Mtu kama huyu Nani alimpa mamlaka ya kuongoza muhimili muhimu kama bunge? Eti ajiongeze ajiuzulu.. Kwa nini yeye Ndugai asijiuzulu kwa kushindwa kuongoza bunge anataka CAG ndio ajiuzulu? Sisi wananchi tulio wengi tuna Imani na CAG Prof Assad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliposema zile ni 'audit query' tu,ndipo nilipojua Prof. Assad hawezi hata kumjibu tena maana anapoteza muda wake tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah.....Queries hujibiwa na kuwa resolved during the audit process wakati zile zinazotolewa reports ni audit findings.

Kwamba polisi wamelipa 16b kwa manunuzi ya sare ambazo hakuna ushahidi wa kuwepo order ya manunuzi wala delivery siyo audit query, hiyo ni audit finding....and fingers can correctly be pointed kwa walioidhinisha malipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nadhan ndio unastahili yote uliyoyasema..yanakufaa wewe kwasababu nadhan ni muathirika wa utumbuaji...hasira zako unataka umbebeshe Speaker..unachekesha kweli...wananchi wake waliomchagua ndio wanajua umuhimu wake wewe huwezi jua...kwa sababu unaposema matusi yako ni sawa na kuwatusi wananchi wake wa jimbo la Kongwa...una akili wewe kweli..i doubt..!

Stupid comment. Kwetu sisi ni spika wa Binge la JMT. We hold and judge him at that capacity. Otherwise, let him resign and remain a member of Parliament from Kongwa constituency.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Aprili 14 atazungumza na waandishi wa habari jambo muhimu kuhusu bunge.

Mazungumzo hayo yatafanyika katika ofisi ndogo ya bunge jijini Dar es salaam majira ya saa sita na nusu mchana.


=====

UPDATES:

View attachment 1071319

=> Spika Ndugai: CAG anaposema mbele ya umma kuwa ataendelea kutuita 'dhaifu' wakati ni jina ambalo hatulipendi na tumelikataa, tunashindwa kumuelewa kama analipenda sana ajiite yeye. Sasa kusema unaendelea kutumia endelea na nitakuita tena na safari hii itakuwa mbaya zaidi"

=> Spika Ndugai: "Namwambia ndugu yangu Prof. Assad hilo neno aliache, sisi taarifa tumeipata na tutaifanyia kazi. Msisitizo wetu ni mmoja, kwakuwa bunge lilishapitisha uamuzi wa kutofanya kazi na Prof. Assad ni uamuzi halali"


=> Spika Ndugai: "Sina chuki binafsi na Prof. Assad, yule ni ndugu yangu na ni mtanzania mwenzangu tatizo ni lugha anayoitumia na nisinhependa itufikishe hapa kama taifa."

=> Spika Ndugai: "Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au laaa!. Maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai: Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake,

=> Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amewahakikishia watanzania kuwa bunge linaendelea vizuri na kazi yake ya kutunga sheria, uwakilishi, kuisimamia Serikali pamoja na mipango ya nchi ikiwemo suala la bajeti ambalo linaendelea bungeni.

=> Spika Ndugai:“Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza

=> Spika Ndugai:Tunataka tumuoneshe Prof. Assad kuwa Bunge halichezewi, simuelekezi kazi ila anatakiwa ajiongeze kama ni kujiuzulu au la! maana tushamwambia hatumtaki, anavyoendelea kubaki ofisini ni kumpa tu wakati mgumu Rais

=> Spika Ndugai:Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai:Sisi kama Bunge hatutaki hilo neno dhaifu, kwa sababu Bunge kama Bunge halifanyiwi tathmini na ofisi ya CAG ila wanaofanyiwa tathmini ni watendaji wa Ofisi hiyo hivyo hawakupaswa kudhihakiwa na lugha hiyo inayotajwa kuwa ya kihasibu.

=> Spika Ndugai: “Hata katika maisha ya kawaida, we unamuita mtu jina flani, anakwambia bwana tafadhali jina hili silipendi, lakini unaendelea kumuita na kuahidi utaendelea kulitumia, ni ustaarabu duniani?”

=> Spika Ndugai: “Katika kutekeleza majukumu yake #CAG hakupaswa na hapaswi kulitukana #Bunge kwa lugha zile za rejareja. Bunge huangalia taratibu zake na kuendesha mambo yake kufuatana na kanuni za Bunge…lile Bunge lenyewe hawezi kulikagua”

=> Spika Ndugai: Hatuna tatizo na ripoti ya CAG…tatizo letu ni maneno ambayo Profesa Mussa Juma Assad ameyatoa akiwa Marekani, na alipoita waandishi akarudia tena, maneno yale sie tumeyakataa sio ya kistaarabu.

=> Spika Ndugai: “Sasa kumekuwa na ufafanuzi usiokuwa sawa sawa, kilichowekwa mezani ni ‘Audit Queries’ …kilichowekwa mezani sio ukweli wenyewe kwamba aliyetajwa mule sasa huyo mwizi… ‘Audit queries’ zile zikishawekwa mezani kazi yetu ni kuwaita mezani na kuwasikiliza”

"Nilipokuwa sipo kuna mambo mengi yamezungumzwa, na mengine yameandikwa kuhusu Ripoti ya CAG. Nitakapokuwa Dodoma nitaagiza ripoti ipelekwe kwenye kamati za PAC na LAC"




Zaidi soma.....

Dar es Salaam. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akamwone Rais John Magufuli ili mzozo wake na Bunge uishe.

Kauli ya Spika inakuja wakati tayari Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad bali ofisi ya CAG.

Spika Ndugai aliyekuwa ziarani nchini Sweden wiki iliyopita ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 14, 2019 akieleza kusikitishwa na hatua ya Profesa Assad kurudia neno udhaifu kwa Bunge alipotoa taarifa yake hivi karibuni.

"Zipo njia za kumaliza mambo kama haya, mojawapo aende kwa Rais akajieleze kwamba mimi nimepima nimeona nimekosea hapa na pale. Maana Rais ni sehemu yetu sisi (Bunge) hatuwezi kupitisha sheria bila yeye kupitisha mkono wake," alisema Ndugai.

Ameongeza kuwa hata bajeti inayojadiliwa na Bunge lazima ipitishwe na Rais. Amesema kwa kuwa Bunge limeshapitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad alitakiwa ajiuzulu.

"Kwa kuwa Bunge likishaaamua kuwa halifanyi kazi na mtu, ni uamuzi halali. Katika nchi zote Bunge likishakosa imani na wewe unajiuzulu," amesema.

Ameongeza, "Sasa hatumfundishi kazi Mussa Assad, anampa wakati mgumu Rais tu. Tutafanya kazi na ofisi ya wananchi."

Spika Ndugai amemsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

"Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri na jamaa ana ujasiri. Ila ni ujasiri ule wa mbwa anayemtukana anayemlisha," amesema.

Hata hivyo, Ndugai amesema hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu aliyotumia ya kuliita Bunge dhaifu.

Naona huyu speaker ana-ramble anachoongea hakileti sense. Kama hataki kufanya kazi na CAG mbona ripoti yake bunge inaifanyia kazi, sasa kwanini ajiuzulu? Ushauri wangu ni wafanye kazi na CAG Prof. Assad hadi atakapostaafu kwa sababu sioni impact yoyote CAG Assad akiwepo....Watafanyia kazi tu hiyo report maana CAG akipeleka ripoti IKULU, kutoka kule anapeleka mtu mwingine, sasa kuna shida gani hapo?
Watanzania wengi waliopo nje wanahitaji uraia pacha kwa faida ya nchi yetu....Siyo kweli hayo anayoyasema kuhusu uraia pacha (Dual Citizenship), wameuomba tangu enzi za Kikwete lakini serikali ya Tanzania imekuwa ikiwadharau, wana-diaspora wana faida kubwa hasa kwenye money remittance, ni vyema wakawapa uraia pacha kuliko kuvamia Bureau De Change na kunyang'anya pesa huko. Watanzania wote waliopo nje wanahitaji uraia pacha ili wawe na uhakika na miradi na mali watakayowekeza nchini...Wamechoka kukataliwa na kutishiwa kuambiwa kuwa HAWANA HAKI YA KUMILIKI ARDHI, Wenzetu Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wanaruhusu uraia wa pacha...sisi tunakataa kwa sababu ambazo hazina maana...Waacheni watanzania wafurahie nchi yao, LUKUVI anawaita waliojiripua kumbe hata knowledge ya watu kukaa nje hana. KWANI WATANZANIA WANAOISHI NJE WAKIKUBALIWA URAIA PACHA TUTAPOTEZA NINI? Ndugai acha nia ovu.
 
  1. Profesa aliapa kutimiza majukumu yake kwa kufuata katiba ya nchi siyo kwa kufuata Ndugai au mtu yeyote anataka nini
  2. Profesa akikubali kujiuzulu kwa kushinikizwa maana yake ameshindwa kutimiza kiapo chake.
  3. Profesa lazima atambue kuwa hakutakiwa kujiuzulu kwa sababu kalidharau bunge, bali wanataka ajiuzulu kwa sababu anafanya kazi yake vizuri na wanachukia hilo.
  4. Profesa lazima ajue kuwa ana dhima ya kulinda uhuru wa ofisi ya CAG kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho, Akikubali kuwapa wanachotaka basi ataweka precedence ya kudhoofisha ofisi ya CAG, Profesa asikubali kuweka precendence ya ofisi ya CAG kukanyagwakanyagwa. Asikubali kujiuzulu
  5. Namshauri Profesa awe Makini na Masheikh na Wazee wazito wazto watakaotumwa kumlainisha, asikubali katakata kwa sababu alipoapa kulinda Katiba pengine haohao ndo walimsomea dua, Leo asikubali maneno ya kumlainisha eti aachie, aachie kwa nini?
  6. Profesa lazima ajue, Cheo cha CAG kilitungiwa sheria maalum ya kukilinda kwenye katiba kwa sababu watu wenye busara walijua kuwa ipo siku mgongano kama huu utatokea pindi CAG akifanya kazi yake kwelikweli, Sasa ni Jukumu la CAG kulinda tunu hii ya hadhi ya ofisi yake kwa ajili ya faida ya nchi yetu leo, kesho na keshokutwa.
  7. Nimalizie kwa kumkumbusha CAG aya ya Qur'an inayosema kuwa usiwatii wanaopinga ukweli na wanafiki bali Mtegemee Mwenyezi Mungu peke yake!
  8. CAG akikubali kujiuzulu maana yake ni kwamba anakiri kuwa kalitukana bunge wakati hajalitukana na hivyo anajutia ndo maana akajiuzulu hii inaweza kutafsiriwa kuwa kavunja sheria ya maadili ya umma na inaweza kumletea shida mbele kwa sababu hawa watu wana visasi.
  9. TAFADHALI CAG ULIAPA KULINDA KATIBA, NA UKAOMBA MWENYEZI MUNGU AKUSAIDIE, USIKUBALI KUVUNJA KIAPO CHAKO KWA SABABU YA WATU WENYE HILA, SIMAMIA UKWELI NA USIKUBALI WAZEE WATAKAOTUMWA KWAKO KUKULAINISHA!.
Asikubali kabisa kabisa hata kama Spika anatumiwa na mafisadi na wezi wa Mali za umma.

Bunge kama lilishindwa kumwadhibu mkosaji mwenye makosa ya kijinai ya vyeti feki Leo linataka kumwadhibu mtu mwadilifu anayelinda fedha za walipa Kodi kwa sababu mafisadi wanataka kuivuruga serikali kwa mgongo wa bunge kwa kumtumia Jobman.

Rais atapambana vipi na ufisadi bila kuweka MTU mwadilifu aliyejitoa muhanga kulinda rasilimali za umma kwa uaminifu?

CCM ijitafakari vizuri 2020 ,Ndugai asipewe tena nafasi apumzike amwachie yule kada mwenzake aliyejaribu kumuua kwa kumpiga gongo mpaka akapoteza fahamu.
Kama CCM kingekua ni chama kinachojali utu na uhai wa binadam ile ilikua ni sababu tosha ya kumwengua Ndugai na hata kumnyima uspika.
Ni Tanzania tu watu wanaotumia silaha za marungu kuwazupiga wanasiasa wenzao ndani ya chama kimoja wanapewa nafasi ya kugombea na hata kuongoza muhimili mkubwa unaotegemewa kutunga sheria za haki za binadam na utawala bora.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hii issue bunge lipo at mercy ya CAG,speaker analialia tuu aache kutuita hivyo😃😃 hawana cha kumfanya.
 
Hata mimi nimeshangaa sana yule DHAIFU kuwa upande wa ku.Defence as if yeye ni serikali.

Kweli leo ule udhaifu wake amejipambanua vizuri sana,press ya leo amethibitisha udhaifu wake kabisa.

Siku za nyuma,viongozi kibao walitimuliwa nafasi zao kwa hizo hizo ambazo anaziita "audit queries",lakini leo haona umuhimu wa govt kuwajibika due to shortcoming that raised in CAG report,huyu jamaa ni waajabu sana.

Huyu ******* anaongea as if hajui jinsi CAG anavyofanya kazi zake, hajui kama CAG anawapata nafasi ya kujibu hoja wakaguliwa wote ndani ya muda husika then ndio report inaandikwa according to majibu waliyotoa,lakini huyu ******* anatoa reasoning ya kitoto. Huyu jamaa ni DHAIFU SANA SANA. Kwakweli MAGU ametuletea SPIKA kituko mwaka huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anatumiwa na mafisadi na wezi wa Mali za umma na pesa sa walipa kodi.
Kuna watu wamezoea kupiga sana pesa za umma kwa miradi feki.
Walizoea kuwahonga Walachizi lakini kwa Prof. Assad amegonga mwamba kwa uadilifu wake ,sasa wameamua kumtumia Spika na bunge lake ili wamdhibiti CAG na kuwatisha waadilifu wote ili waamini kuwa uadilifu wao hauna manufaa kwao binafsi.

Mbona yeye amemtukana CAG kwa kumfananisha na mbwa?
Nduu gay hajui hata Lipi lenye manufaa kwa umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom