Amesahau kuwa aliahirisha siku ya msiba wa KANUMBA??????????????????? WACHAWI HAWA CCM
Kwani hawa wabunge wa Zanzibar ni wazamiaji ili wawahi kwenda kupiga mbizi na kuokoa watu au wanataka kwenda kuuza sura kwa wapiga kura wao?
wasingeweza ingewazidi nguvu mawiziri wenyewe wawili tu boti ina watu mamia afu walikuwa mbali na eneo la tukio.eboBajeti ya wizara ya mambo ya ndani na wizara ya Ulinzi zisipite mpaka mawaziri wao waeleze ni kwanini walishindwa kuizuia hiyo boat isizame.
Spika kungolewa?
Baadhi ya wabunge wameanza kuwahamasisha wenzao kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge.
Wabunge hao walifikia hatua hiyo kwenye kikao cha dharura walichokifanya jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa kwa lengo la kufanya maandalizi ya kwenda Zanzibar kuhudhuria msiba wa wenzao waliozama katika ajali meli ya Skagit.
Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahimu Sanya (CUF), alisema Spika Makinda hana utu ndiyo maana aligoma kuahirisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi ya watu kushiriki kwenye jambo hilo.
Huyu Spika hatufai, yaani vifo vikitokea kwa watu wa Bara yeye ndiyo ataona kuna uzito hapa alikufa Amina Chifupa tukaahirisha Bunge, sasa iweje wenzetu wamekufa kule Zanzibar yeye akatae kuahirisha shughuli za Bunge? Jamani tujipange kupiga kura za kutokuwa na imani naye, ameonyesha kushindwa kulihimili Bunge, alisema.
Mbunge mwingine kutoka Zanzibar alisema hawaoni sababu ya kuendelea na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu wapiga kura wao ndio waliofariki dunia.
Tuna raha gani ya kuendelea kujadili hotuba ya bajeti, huyu Spika tumedhihirisha hana uwezo wa kutuongoza, hatufai, waliokufa kule ni binadamu si paka wala wanyama, alisema.
Chanzo:Tanzania daima
Kwa mara ya kwanza jana niliona alivozungukwa na aibu mwili mzima baada ya udikteta ulioambatana na unafiki,alitamani atoweke
...sio wote wenye macho wanaoona...Tanzania Daima haina habari hii- Acha uzushi
Lakini hebu tuwe practical wapendwa, Kikao kimeahirishwa kwa sababu tu ya hiyo ajali (kwamba upo uwezekano ya kuwa baadhi ya wabunge wa zenj na bara wanaweza kuwa na ndugu zao ndani ya hiyo meli) au kwa sababu kuna kitu wabunge wanaweza kufanya kusaidia katika uokozi au shuguli yoyote inayohusina na ajali hiyo. Kwa maoni yangu, huyo mbunge hakukosea na Spika pia hakukosea sana ila anaweza kuwa ameeleweka ndivyo sivyo. Tuwe wavumilivu sana wakati huu tunapoombleza!Mmmh sidhani kama huyo mbunge alikosea sana...maana Spika alidai kwamba kama ajali ingekuwa imetokea karibu na Bunge(which justifies kuwa alikua anaongelea Bara) ndio kungekuwa na mantiki ya kuhairisha kikao cha bunge.
Lakini hebu tuwe practical wapendwa, Kikao kimeahirishwa kwa sababu tu ya hiyo ajali (kwamba upo uwezekano ya kuwa baadhi ya wabunge wa zenj na bara wanaweza kuwa na ndugu zao ndani ya hiyo meli) au kwa sababu kuna kitu wabunge wanaweza kufanya kusaidia katika uokozi au shuguli yoyote inayohusina na ajali hiyo. Kwa maoni yangu, huyo mbunge hakukosea na Spika pia hakukosea sana ila anaweza kuwa ameeleweka ndivyo sivyo. Tuwe wavumilivu sana wakati huu tunapoombleza!
Kaliahirisha Bunge leo. Tumfutie "dhambi" yake ya jana?
Taarifa rasmi ilikua haijatolewa bungeni we ulitaka aairishe bila kua na uhakika na kile kinachozungumzwa?Ukweli ni kwamba alikosea, na isingekuwa busara za Nchimbi kikao cha bunge kingeendelea mpaka lihamba.
Bunge linaendeshwa kwa sheria na wala sio hisia mkuu, tukio lolote la huzuni linalogusa Taifa moja kwa moja huwa kunakuwa na utaratibu wa kuhairisha kikao cha bunge ili kujumuika na wahanga. Hii haijalishi kuwa wabunge wana uhusiano wa moja kwa moja na wahanga au lah! Kilichotokea ni janga la kitaifa.
Unajua Mama Makinda inabidi abadilike, siku zote anaendesha Bunge katika itikadi zile zile za Mwalimu na mwanafunzi.
Inabidi asanuke na kugundua kuwa pale sio shuleni ni bungeni...na sasa hivi yeye ni Spika na sio mwalimu.
Kama hakuwa na taarifa hakutakiwa kupinga hoja kwa utashi bali kwa vifungu vya sheria.Taarifa rasmi ilikua haijatolewa bungeni we ulitaka aairishe bila kua na uhakika na kile kinachozungumzwa?