Spika akalia kuti kavu

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,166
1,247
Spika kung'olewa?

Baadhi ya wabunge wameanza kuwahamasisha wenzao kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge.
Wabunge hao walifikia hatua hiyo kwenye kikao cha dharura walichokifanya jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa kwa lengo la kufanya maandalizi ya kwenda Zanzibar kuhudhuria msiba wa wenzao waliozama katika ajali meli ya Skagit.

Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahimu Sanya (CUF), alisema Spika Makinda hana utu ndiyo maana aligoma kuahirisha shughuli za Bunge ili kutoa nafasi ya watu kushiriki kwenye jambo hilo.

"Huyu Spika hatufai, yaani vifo vikitokea kwa watu wa Bara yeye ndiyo ataona kuna uzito…hapa alikufa Amina Chifupa tukaahirisha Bunge, sasa iweje wenzetu wamekufa kule Zanzibar yeye akatae kuahirisha shughuli za Bunge? Jamani tujipange kupiga kura za kutokuwa na imani naye, ameonyesha kushindwa kulihimili Bunge," alisema.

Mbunge mwingine kutoka Zanzibar alisema hawaoni sababu ya kuendelea na mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa sababu wapiga kura wao ndio waliofariki dunia.

"Tuna raha gani ya kuendelea kujadili hotuba ya bajeti, huyu Spika tumedhihirisha hana uwezo wa kutuongoza, hatufai, waliokufa kule ni binadamu si paka wala wanyama," alisema.

Chanzo:Tanzania daima
 
Mh, hata mi nilimuona jana anavyowaka mara oh bado nafanya mawasiliano, labada hakuwa amepata habari za kuaminika au hakuna kifungu kinachomruhusu kuahirisha bunge kwa matukio kama hayo? manake pia nilimuona waziri Nchimbi ndiye aliyekuja kutoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge.
 
Huyu mama kwa sababu hana utashi wa kutosha alisahau alipoahirisha bunge wakati wa msiba wa chifupa pale aliset precedence inabidi iwe hivyo siku zote................... katika hili spika makinda ameboronga, awataka radhi wabunge na watanzania wote.
 
CCM kila mtu sasa ni afadhali kidogo hakuna aliyebomba kabisa. Ni afadhali ya huyu kuliko yule lakini wote ni hovyo tu.
 
Huyu mama kwa sababu hana utashi wa kutosha alisahau alipoahirisha bunge wakati wa msiba wa chifupa pale aliset precedence inabidi iwe hivyo siku zote................... katika hili spika makinda ameboronga, awataka radhi wabunge na watanzania wote.

Amesahau kuwa aliahirisha siku ya msiba wa KANUMBA??????????????????? WACHAWI HAWA CCM
 
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto?

Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu.

Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu Spika hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...
 
hapo sasa wao naowameona kuwa afai ehh hata kwa kanumba aliahirisha, sasa hawa ni wanyama sio watu hatufai yeye na wote walio chini yake hawafai
 
Hii sasa ndio mbaya. Kunyanyapaa watu sio vizuri.
Mnataka awe na uchungu kwani ameshawai kujifungua au kuwa na mtoto? Kwa kauli yake ya jana inaonyesha jinsi alivyokuwa na roho mbaya, roho iliyokosa utu. Pia, hata akalie ncha ya hilo 'kuti kavu', kwa mfumo wa kimagamba huyu bibi koroboto hawawezi kumng'oa uspika, tuhesaba tumeshalamba garasa, tusubiri 2015...
 
Alichoharibu ni hapo kwenye RED...subiri watakuja kumjibu hapa.....

Mmmh sidhani kama huyo mbunge alikosea sana...maana Spika alidai kwamba kama ajali ingekuwa imetokea karibu na Bunge(which justifies kuwa alikua anaongelea Bara) ndio kungekuwa na mantiki ya kuhairisha kikao cha bunge.
 
Yule Mabumba wa Zanzibar naye alitoka nje? maana naye akikaa kwenye hicho kiti huwa haambilki, pengine sasa ameonja machungu ya uongozi wao wa kibabe.
 
Bajeti ya wizara ya mambo ya ndani na wizara ya Ulinzi zisipite mpaka mawaziri wao waeleze ni kwanini walishindwa kuizuia hiyo boat isizame.
 
Mh, hata mi nilimuona jana anavyowaka mara oh bado nafanya mawasiliano, labada hakuwa amepata habari za kuaminika au hakuna kifungu kinachomruhusu kuahirisha bunge kwa matukio kama hayo? manake pia nilimuona waziri Nchimbi ndiye aliyekuja kutoa hoja ya kuahirishwa kwa bunge.

Correction..... decruca, Waziri hawezi kufanya hivyo alichokifanya nchimbi ni kuondoa hoja ya serekali bungeni....
 
Kwa mara ya kwanza jana niliona alivozungukwa na aibu mwili mzima baada ya udikteta ulioambatana na unafiki,alitamani atoweke
 
Huyu mama kwa Kweli Hii kazi iko juu ya uwezo wake nazani ata Waliomuweka wanajuta
Poleni wazenji msameheni kwa Maana hajui atendalo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom