Binafsi, sioni sababu hata kidogo ya kutumia kodi ya watanzania kugharamia vikao vya bunge kwa sasa. Nitaeleza:
Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, wanaongea yale waliyotumwa na wananchi, lakini chini ya Makinda wabunge wamezibwa midomo na hivyo hoja za wananchi hazijadili. Kwa kutoruhusu wawakilishi wa wananchi kuwasilisha yale waliyotumwa maana yake bunge sasa linageuzwa kuwa rubber- stamp.
Uhuru wa mhimili huu mkubwa, mhimili wenye mamlaka ya kuisamamia serikali sasa haupo tena. Makinda kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe amegeuza huu mhimili kuwa idara ya serikali.
Serikali inaleta hoja mezani ili ijadiliwe, lakini Spika anaonekana kuruhusu mijadala ile inayompendeza yeye (spika) kwa kisingizio cha kanuni! Spika amesahau kabisa kwamba anapomziba mbunge mdomo maana yake amewaziba mdogo pia wananchi waliomtuma mbunge huyo. Kanuni sio msahafu, na haiwezekani tafrisi ya mtu mmoja - spika ndiyo iwe tu sahihi.
Tukumbuke huyu Spika hajasoma sheria, naibu wake hajasoma sheria, katibu wa bunge naye hajasoma sheria. Hivyo team yote ya juu ya bunge ni kama wapita njia in terms of sheria. Na matokeo yake ndiyo haya tunayoona sasa. Hata madai kwamba wabunge hawawezi kujadili hoja ambayo iko mahakami ni tafsiri pototu. Tanzania wanafuata British law, na chini ya sheria zetu unaweza kabisa kujadili hoja ambayo kesi iko mahakamani bila kuathiri mwenendo wa kesi.
Ukitizama mwenendo mzima wa bunge tangu mwezi June hadi sasa, hakuna jambo lolote la maana lililopitishwa zaidi ya ku-rubber stamp hoja za serikali.
Sasa kama Spika yuko pale kuimarisha huo mfumo wa rubber-stamp kwanini watumie kodi ya wananchi kulipa posho wabunge 300+ kwa kazi ambayo inaweza kufanyika kwa siku 3 au 4? Kwanini wasipitishe vifungu vyote kwa wizara zote kwa pamoja ili waokoe fedha za watanzania? Nasema tena, hakuna haja ya kuweza wabunge Dodoma kwa miezi kadhaa, wapitishe vifungu kwa pamoja bila ya mipasho na ngonjera na haraka warudi uraini.