Spidi ile JK wanamkimbizia wapi..!?

Si tumeambiwa yuko mlimani anauza sura? Au ni mwanae manake kuna wakati ananyanyuka na Presidential convoy!!!!!
 
kupanda mlima hadi kileleni ni siku tano (kwedna na kurudi). Kupanda nusu ni siku tatu (kwenda na kurudi)

atafika mbele ya mandara hut ni safari ndefu
Alikuwa zaidi anazindua program....ya wanawake, yeye si mpandaji kwa siku zote tatu za ziara yake K'njaro.
 
Wakuu salamu,
Muda huu umenipita msafara wa JK hapa maeneo ya Tabata dampo. Msafara ulikuwa na magari zaidi ya 30 na difenda za Presidential Protective Unit kama 8 hivi. Wamepita kwa spidi kali pengine kuliko kawaida ya spidi ya Presidential motorcade jambo ambalo limewashangaza wengi hapa.
Gari hizo zimetokea maeneo ya Ubungo na zimeelekea Tazara/Airport.

Kwa wale wenye taarifa mtujuze;
1. Bwana mkubwa anaelekea wapi?
2. Kwa nini msafara ukimbie kwa spidi ile? (spidi ilikuwa si chini ya 160kph).
3. Kwa nini leo amebadili njia na kutumia njia ya Mwenge-Ubungo-Tazara-Airport? (Njia ambayo huwa anatumia mara nyingi akiwa anaenda Airport ni Nyerere Road, leo mbona amezunguka hivi....kulikoni?

Wenye taarifa tafadhali.
Zile gari zimetoka moshi kumuwahi kumchukua airport hapa dar, amerudi jioni hii
 
Huyu jamaa kesha toka moshi?

Nasikia jana alikuwa himo akikagua magodown ya mahindi ya watu binafsi akiwa na mrema, mrema akamwambia hayo magodown ndo yanasafirisha mahindi kwenda kenya. Je kwani ya serikali hayapo akayakague? Kama hayapo basi ayatengeneze ili akapate kuyakagua
 
Taarifa za KIINTELIJENSIA zinasema kuwa, JK hakupanda mlima kabisaaaaaaaaaaaa! Aliwasindikiza tu na aliishia pale getini Marangu. Jana jioni alipanda pipa kurudi bongo daslam! Inawezekana anaelekea airport JKNIA kuelekea Russia kuhudhuria sherehe za kuapishwa rais mchaguliwa wa Russia, Vladimir Putin!
Hivi kuna watu waalikuwa wanaamini kuwa bwamkubwa kapanda mlima hadi kileleni..!? Kweli humu kuna ma-greti sinkers.
 
Mkeshaji,

Unasema msafara umepita kwa speed isiyo ya kawaida kwani standard ya speed kwa msafara wa Prez ni ngapi km/hr?

Na je huo ulikuwa unaenda kilometa ngapi wka saa?
Mkuu ile spidi ya leo mi huwa naionaga kwenye motor racing championship tu.
 
Hapana hakupanda juu zaidi ya Marangu geti kuu

Ni ukweli kwamba Mheshimiwa Rais alikuwa mgeni rasmi jana kuwatakia kila jema wapanda mlima Kilimanjaro kutetea haki za akina mama, na sherehe hii ilifanyika Marangu gate, na hivyo hakupanda mlima. Picha za Mheshimiwa akipunga bendera kuanzisha safari, na akiwahutubia wapandaji hizi hapa chini (Source: michuziblogspot.com).

JK flagging off the Kilimanjaro climbers.jpg

JK flagging off the Kilimanjaro climbers2.jpg
 
Kila nikiulazimisha ubongo wangu kukuelewa inakuwa ngumu sana, yaani swala la madaktari na kupanda mlima priority ya Rais ni kupanda mlima kwa sababu lipo kwenye ratiba ya muda mrefu?
Mbona JK huyu huyu alikatisha ziara yake South Africa kwa ajili ya kuja kuwahi kumzika yule mchawi wa magomeni Mwembe chai?
Mkuu kwani ilikuwa Rais akutane na madaktari?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom