Wakuu salamu,
Muda huu umenipita msafara wa JK hapa maeneo ya Tabata dampo. Msafara ulikuwa na magari zaidi ya 30 na difenda za Presidential Protective Unit kama 8 hivi. Wamepita kwa spidi kali pengine kuliko kawaida ya spidi ya Presidential motorcade jambo ambalo limewashangaza wengi hapa.
Gari hizo zimetokea maeneo ya Ubungo na zimeelekea Tazara/Airport.
Kwa wale wenye taarifa mtujuze;
1. Bwana mkubwa anaelekea wapi?
2. Kwa nini msafara ukimbie kwa spidi ile? (spidi ilikuwa si chini ya 160kph).
3. Kwa nini leo amebadili njia na kutumia njia ya Mwenge-Ubungo-Tazara-Airport? (Njia ambayo huwa anatumia mara nyingi akiwa anaenda Airport ni Nyerere Road, leo mbona amezunguka hivi....kulikoni?
Wenye taarifa tafadhali.