Huk Luk
JF-Expert Member
- May 5, 2022
- 1,258
- 15,778
Huh kuna clip inatembea, huyu huyu Blinken anaeshawishi watu waende frontline waka kaangwe vizuri huku yeye akiwa jukwaani hapo Kiev akicheza na Gitaa.Juzi Antony Blinken alienda Kiev kuonana na Zelensky.
Kwenye mazungumzo Yao, USA wamemwambia wanataka kuona matokea ya huu Msaada wa $61bil.
Wanataka kuona Ukraine inayarudisha nyuma majeshi ya Russia, vinginevyo watamkatia misaada.
View attachment 2990539
F really kweli they care, katika Nchi wanayo tuaminisha kua ipo Vitani dhidi ya "Enemy" mwenye nguvu zaidi yake hivyo misaada ya kina inahitajika. Anafika eneo la mapambano anapanda jukwaani kucheza na Gitaa, kweli?
Kwa raia wa Ukraine wenye akili timam hili jambo wanalichukuliaje? Of course kuna pink ponies wanaona kawaida and enjoyable. Ila kwa Baba, Mama, au mke ambae mtu wake kachukuliwa kwa lazima then kwenda kufia frontlines kwa ajili ya hawa viumbe uchungu alio nao haupimiki.
Kuna wakati hua najarib kuvaa viatu vyao, inaniwazisha sana. Aiseee ni kheri kua na ulemavu wa mwili ila sio ulemavu wa akili. Kwa binadam ambae ana matatizo akilini mwake en yet hajioni kama ana tatizo yule mbuzi zizini ana ubora kuliko yeye.
With the help of map just for illustration, US to Ukraine ni thousands miles (Yellow to Green), Ila watu wanafunga safari kwenda kuhakikisha mtu na jirani yake hawapatani abadani.
Ukrainians sijui nani kawaloga, na how comes serikali inaeza control population of millions astray, mmh? Ina maana hawawezi kupinga endapo wanapotezwa? Kwanini they are heading into total destruction, total collapse calmly utafikiri mikondoo. (Hapa huenda hata kondoo wakawa na nafuu).
Pia kama kweli ni Serikali ya raia wa Ukraine, imewekwa na raia wa Ukraine kwa ajili ya raia wa Ukraine kwanini ifanye kazi kwa maslah ya US nje ya interests za Ukrainians wenyewe?
Tukiangalia wanaokimbia na kujitoa kafara kuvuka mto kuingia Romania, wengine kunusurika wengine kufia majini wakijarib kutoroka kukamatwa kupelekwa front, hii hali inaongea mengi sana kuhusu Raia wa kawaida hapo Ukraine, Wanateseka sio kidogo.
When the rich wage WAR, its the POOR who DIES, it's the poor who SUFFERS. West wana print fedha kupeleka Ukraine, ila raia wa kawaida ndio wanaonja joto la jiwe huko fronts.