Zelensky: Hakuna nchi inayoweza kustahimili vita na Urusi peke yake

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,965
6,625
Kiongozi wa Ukraine anahimiza ulimwengu kuungana dhidi ya Moscow

Hakuna nchi inayoweza kustahimili vita na Urusi peke yake - Zelensky

Vladimir Zelensky wa Ukraine ameitaka jumuiya ya kimataifa kufanya kazi pamoja dhidi ya Urusi, akisisitiza kwamba hakuna taifa linaloweza kunusurika vita na Moscow peke yake.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Asia ya Kati siku ya Jumamosi, Zelensky alisema lengo linapaswa kuwa kuhakikisha kwamba Rais Vladimir Putin "anafikiria juu ya maisha yake na usalama wake," na kwamba "Warusi wanafikiria jinsi wanaweza kuepuka kupoteza uhuru wa nchi yao. - bila kuwatishia - kwa kuonyesha tu jinsi ulimwengu ulivyo na umoja, jinsi ulivyo na nguvu."

Umoja huo unahitajika kwa sababu "hakuna anayeweza kustahimili vita kamili na Warusi peke yake," kiongozi huyo wa Ukraine alisema, kama alivyonukuliwa na gazeti la mtandaoni la Kazakh la Vlast.

"Tulikuwa peke yetu, tulikuwa peke yetu" wakati Urusi ilipoanzisha operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022, Zelensky alidai. "Lakini basi tulikubaliana na washirika wetu juu ya aina fulani ya vikwazo, aina fulani ya silaha na mambo mengine," alisema. alisema, akimaanisha msaada uliotolewa na nchi za Magharibi tangu kuanza kwa mzozo huo.

Hata Beijing "lazima ilinde Ukraine kwa sababu tulishambuliwa," kama "China inasema kwamba uadilifu wa eneo lazima uheshimiwe," mwanasiasa huyo alisema.

My Take:
😷
 
Nilisema humu na nitaendelea kusema kuwa; Russia ni dubwasha lenye nguvu mno kivita siyo nchi ya kuikabili kirahisi katika mapigano ya kivita.
Silaha nyingi alizo deploy dhidi ya Ukraine ni zile za Soviet era, Zelensky alikosea na anaendelea kukosea kuwategemea "walimwengu" kumsaidia.
Marekani, ujerumani, uingereza, polandi, Latvia n.k wamejitahidi kupeleka silaha na wanajeshi uwanja wa vita dhidi ya Russia lakini wameishia kupata hasara

Ifike mahala akubali kukaa meza moja na Hilo dude wayamalize kiujirani. Jiografia ya marekani kuisaidia Ukraine at a full scale haisapoti.

Taifa pekee duniani la kukabiliana na Russia kivita wakatoshana nguvu labda marekani ( of course number matters a lot).

Warusi ni jamii korofi na yenye kujiamini sana.
 
Hata USA hamuwrzi Mrusi ndio sababu akaunda Nato.
 
Kwa hiyo na mmarekani hawezi pigana vita na mrusi? 😂
Hata sasa anapigana nao wote, na bado anaendelea na shughuli zake za kila siku kama vile hayuko kwenye operesheni kubwa.

Russia ni gari kubwa sana, sema tu haina mambo ya propaganda kama USA, hadi wengi wanaichukulia poa.

Fikiria alitibua uchaguzi mkuu wao na hakukuwa na kitu kawafanya.

Ova
 
US hawez enda head to head na Russia bila washirika wakuu.

US hawezi kujirisk kupigana na linchinkama Russia, Ni risk kubwa sana.

Russia angekuwa soft NATO wangekuwa washamvamia na kuondoa Serikali, lakin wanahofu kubwa sana na wako makini sana.

Imagine silaha tu za kumpa Zelensky apige Moscow hawataki na wanaogopa. Why??
 
Awe makini tu Putin asije kumpatia yeye hicho anachoongelea yani kuuweka usalama wa maisha yake mashakani
Huyu ni mjinga na kwa ujinga wake anataka kuishirikisha dunia iingie gharama
Akubaliane na Putin maisha yaendelee aache udwanzi
Kama hawa watu/washirika wa ukraine wangekuwa na akili wangeingia vitani na Russia moja kwa moja
Wameshindwa kuishinda Russia kwasababu
Mfano mimi nina mishale elfu tatu wewe una mishale mia mbili unaomba maswahiba zako wakusaidie mishale ya kupambanna na mimi mmoja anakupa mishale mia mwingine anakupa mia mbili na mwingine anakupa hamsini jumla unakuwa na mishale 550
Ukija kwangu ninayo 3000 utatoboa vipi sasa

Hawa maswahiba zako wanazo stock za kutosha sana lakini hawako tayari kutoa kiasi kikubwa kwaajili yako sasa ushindi utapata vipi hapo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom