Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Vipi kuhusu uwezo wa gari kukata kona maana hilo tairi kubwa haliruhusu kina, maoni yangu ni kwambaanadumu gari halifiki mbali lazima litapata ajali ya either kugonga au kutumbukia korongoni au lisifike lolote likiwa limekwama mahali sababu ya kizuizi ambacho kinakwepeka kama lingekuwa na uwezo wa kukata kona,sijui Hii inarelate Kiasi gani na Tanzania as plate number inavyoonesha
 
Dreamliner wakati hata usafiri wa mabasi ni gharama kwa raia.

Flyover mjini huku serikali inahamia Dom badala ya kujenga mji mpya ambako hakujajengeka.

Kila leo Dar inabomolewa, msishangae miaka 10 ijayo makao makuu ya serikali yakarudi Dar.
angaria rangi ya gari utajua
 
TZ inaongozwa na buldoza ambalo ndio tair hpo aka chuma,nahilo tair la kulia mbele dogo ni mama samia na viongoz wenzake nyuma nahilo gar limepaki maana yake mafisadi wote washashuka humo
 
Mimi nimeielewa hivi..hizo tairi hazifanani ,hii ni hali ya sasa ya hamahama ya wanasiasa kuelekea upande mwingine na hii inaudhohofisha upinzani..upinzani ukidhohofika nchi haiwezi kuendelea kwani kunakuwa hakuna wakosoaji wazuri wa serikali..so nchi haiwezi kwenda mbele,,na ni kama unavyoona hapo kwenye picha ya gari,,gari hilo haliwezi kuenda mbele zaidi ya kudondoka bondeni,sababu tairi hazijabalance au kukaribiana size
hii rangi chama gani!????

mmekalili eeeeeh

 
Tanzania inaendeshwa kwa kuungaunga tu km maskini anavotaka kua na gari anaweza akaanza na ingini ya IST akaishia kupata chasis ya Fuso na Tairi za Trekta....Yani No Policy No Plan bora umiliki Gari ata km halitatembea ila linawaka tu
 
Hii ni kazi ya kifasihi ya hali ya juu.....inanikumbusha kazi ya Kezilahabi iitwayo MZINGILE na ile tamthiliya kali sana ya KAPTULA LA MARX...
GuDumeeeeeee! Njoo uone hukuuuu.
 
Kwa kawaida gari ili itembee vizuri inatakiwa kuwe na uwiano sawa but hapo inaonyesha kuwa tair Moja tu ndio inanguvu
 
wapinzani wa tanzania
taasisi binafsi kabisa za kifedha zinazama.

chama tawala nchini tanzania
taasisi binafsi kabisa za kifedha zinakuja juu baada ya kuzama kwa muda mrefu.

mimi mpiga kura mtarajiwa
aigooo macho yangu hayaoni vizuri
 
Tunaomba msaada wa tafsiri sahihi ya hiki kibwengo (Sir KIPANYA please do the needful, maana najua upo humu). Sijaelewa kabisa hivyo vifito vilivyofungwa kwa kamba vinamaanisha nini
 
Huyu jamaa huwaga simuelewi kabisa!
FB_IMG_15343391894084174.jpg
 
Back
Top Bottom