nimeelewa yafuatayo:
Gari maana yake ni serikali ya TZ.
Gari ina usukani lakini haina dereva maana yake Tanzania haina raisi mathubuti kwa sasa.
neo TANZANIA limeandikwa mbele ya gari maana yake maslahi ya taifa ndilo neno linalonadiwa sana na wanasiasa wa sasa lakini kiuhalisia hakuna anayejeli maslahi ya Tz, wanajali matumbo yao.
Tairi la kushoto ni kubwa kuliko matairi yote maana yake nguvu za utawala wa nchi zimeelemea upande mmoja pasipo kujali mambo mengine, kwa mfano; kuhangaisha wapinzani na wanaoikosoa serikali kwa kuwakamata kamata na kuwafungulia kesi za ajabu ajabu.
Tairi kubwa kuwa mbele upande wa kushoto maana yake jambo inalolishikilia sana serikali la kutesa wanaoikosoa lipo upande usio na nguvu yaani upande wa kushoto, yaani wananchi wengi hawalikubali.
mkao wa picha unaonyesha wananchi wamesimama upande wa huku ilipo tayiri kubwa na ndipo mchukua picha alisimama pia.
tayiri kubwa kuwa mbele maana yake nyingine ni kuwa gari inaenda kwa kasi maana tayiri hiyo inasapoti hivyo ila huenda ikaenda kasi kwa jambo fulani halafu ikapeleka gari shimoni au huenda ikapelekea gari kurudi nyuma ghafla na kuanguka maana uzito emeelemea nyuma hasa upande wa kuume.
setimila ya kushoto inaangalia chini maana yake dereva hataweza kuona kinachokuja nyuma yake badala yake ataendesha gari bila kujali wa nyuma yake, kwa mfano, wastaafu mnawashwa washwa.
tairi la kulia ni la piki piki maana yake upande wa dereva hauko salama kabisa gari yaweza pinduka wakati wowote maana uzito umeelemea huko.
rangi ya njano kwenye plate maana yake utajiri wa tanzania ndo kitu kinachopewa kipaumbele kuliko hata wananchi wenyewe, utasikia wakisema faru john lazima apelekwe hospitalini ulaya kutibiwa, utasikia mbwa atafutwe haraka sana, utasikia .. .................................
barabara ina udongo mwekundu maana yake gari inakanyaga hatari ktk safari yake, kwa mfano kunyima haki za msingi kama za kujieleza ambapo watu wengi wanaanza kuwa na kinyongo na vyombo vya dola ambavyo ni sehemu ya serikali tena vinawazuia kusema ya moyoni.
gari ipo kwenye mteremko maana yake inaseleleka kwa kasi huku haina dereva na lazima tu itapinduka huko mbeleni,
barabara ni fupi maana yake mda si mrefu gari hiyo haitafika mbali lazima itavurugikiwa tu.