Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Special thread: Vikaragosi vya Masoud Kipanya

Iko hv. Magufuli anahangaika kujenga au kusafisha saiti (ku-clear site) lakini kuna mitoto au watu wanacheza juu ya kifusi na wengine wamepanda na wanacheza kwenye kijiko sasa badala ya yeye kuendelea na kazi anabaki kukimbizaa nao.

Kwa ufupi ni kwamba hawaelewi ni nini anachofanya wanadhani ni mchezo tu.

My Note. HILI NI KWELI na Masoud ni jinias kweli.
Nimekuelewa mkuu, tafsiri mrua kabisaa au wewe ndo kipanya mwenyewe vipi!!!?
Halafu wakati anahangaika na hao wanacheza kwa kifusi wengine wanakuja nyuma ya tinga na vikapu wanarundika tena michanga alikorekebisha Hahahahaha hatari sana
 
Mange hapo sasa ni yupi?

Ok, nimeshamuona kumbe yupo hapo juu ya bullldoza na midole yake juu.
 
Aisee nimegundua lingine..angalia gari lenyewe halina dereva yaani dereva ametoka kwenye stering yupo nje akiwa onya watu( kushika fimbo ni lugha ya kuonya) alafu watu wenyewe hawajali lakini walio nyuma ya hilo gari wamebeba ndoo (ni ishara ya kunufaika yaani kuchota mali) na wengine hawana habari wapo nyuma lkn wamekaa kama mazuzu hahaha hii picha inahitaji akili sanaaa
You are jinias hahahahhh
 
Bulldozer hasikilizwi tena !!
Katoka kwenye hilo dude kuwaambia watu wampishe ... Ndo kwaaanzaaa wanaruka sarakasi .... wengine wameamua wapande kabisa kwenye bulldozer kuonyesha hawamwogop hawa ndo balaa
Sio hivyo tuu jamaa ana foka foka .. Ni kama washamzoea hivi !! Hii ndo balaa
Waliopo kwenye bulldozer wanafanana rang na dereva hivyo inaonesha ni watu wa kundi moja sio waliotoka chini wakadandia
 
Dereva anasafisha kifusi huku akiwa na watu ambao wangemsaidia kusafisha kifusi(kipanya amewatofautisha na watu wengine wa chini kwa rangi hapa kila mmoja anaweza kuja na theory yake
Mimi nilichofikiria
Yawezekana mmoja akawa anawakilisha viongozi wa dini na mwengine anawakilisha watendaji ndani ya serekali)
Huku dereva akijua alionao kwenye bulldozer watamsaidia ndio kwanza (viongozi wa dini) wanamgeuka na kuwa wapinzani(angalia ishara ya vidole)
Na huku dereva akimuachia jukumu la kuchunga watu wanyuma huyu mtendaji ndio kwanza ametulia akisubiri maagizo na watu wanajichotea kilaini

Huku mbele dereva amechanganyikiwa na makelele mpaka ameachia usukani bulldozer linaenda lenyewe madhara yake litaenda bila ya direction
 
Iko hv. Magufuli anahangaika kujenga au kusafisha saiti (ku-clear site) lakini kuna mitoto au watu wanacheza juu ya kifusi na wengine wamepanda na wanacheza kwenye kijiko sasa badala ya yeye kuendelea na kazi anabaki kukimbizaa nao.

Kwa ufupi ni kwamba hawaelewi ni nini anachofanya wanadhani ni mchezo tu.

My Note. HILI NI KWELI na Masoud ni jinias kweli.
Kuanzia leo naanza kufatilia comment zako!! Maana umetafsiri vizur
 
Mi nimeona Kifusi na Tingatinga!View attachment 735969
Nimeelewa hivi.
Magufuli ana kazi ya kusawazisha hicho kifusi. Shida ni kwamba juu ya kifusi kuna watu ambao hataki waumie pindi anapoendelea kufanya kazi yake. Ameamua kushuka ili awaambie watoke yeye afanye kazi yake. Badala ya hao watu kuondoka eneo hilo, wao ndo kwanza wanaruka sarakasi.

Tafsiri ya hilo ni kwamba hatumcheleweshi magufuli. Bali tunajichelewesha wenyewe.

Huku nyuma ni baadhi ya watu walianza kunufaika na kazi yake ya kusawazisha
 
Huyo aliyekaa kwenye Hilo bulldozer huku akiwa amenyanyua mikono anashangilia lazima atakuwa ni Bashite tuu!
Kweli uoni ni macho, kila mtu ana yake! Kuna aliyekaa na kunyanyua mikono hapo kweli?
 
Kwa kelele zenu mmesababisha nitoke kwenye usukani, mmepanda kwenye kifusi ninachotaka kukifukua, haitoshi mmepanda hadi kwenye karandika kunikebehi, na wengine mnaiba hadi mafuta. Dawa yenu nikuwashukia huko huko niwatandike RUNGU
 
Kwa kelele zenu mmesababisha nitoke kwenye usukani, mmepanda kwenye kifusi ninachotaka kukifukua, haitoshi mmepanda hadi kwenye karandika kunikebehi, na wengine mnaiba hadi mafuta. Dawa yenu nikuwashukia huko huko niwatandike RUNGU
 
Hii nilivyoelewa mm ni kwamba wananchi wanzidi kusukumwa mbaaali na hilo li tingatinga na huyo operator aliye juu ya hilo tingatinga na anatoa maelekezo na kuwafukuza wazidi wasogee huko
Hapana ni kinyume chake wananchi wanaanza kufaidi matunda huku majizi yakilala mbele
 
The Bulldozer hawamsikilizi tena. Hawamwogopi, anapiga nduru wampishe ndo kwanza wanapiga sarakasi.

Wengine wamepanda kabisa tingatinga, ila wachache wanachota mafuta.

Sijui mwisho wake.
Ndivyo inavyokuwa hata ktk Familia baba ukiwa Mali Sana hufikia hatua watoto hukudharau wewe utapiga kelele wao hawakusikilizi tena wao wafuata yao
 
Back
Top Bottom