Hahahah, ila kweli watunzi wa muvi za kibongo hawajishughulishi sana kutaka kuendana na mazingira!
Kama hii muvi tuliyotoka kuicheki, eti watu wamemteka mtu karibu na ulinzi mkuu halafu wanamrudisha na kumtupa karibu na ulinzi huo huo mkuu nchini.
Halafu mtekwaji anapiga simu home wamfuate,anakaa anasubiri ndugu zake wamfuate,ndugu wanafika,wanamchukua wanaenda naye haooooo...nyumbani.....muda wooooote huo hakuna hata mlinzi wa kibanda aliyeshituka achilia mbali walinzi wa eneo kuu!!!!.....
Wanafamilia nao,badala ya kwenda polisi wanaenda nyumbani halafu wanawaita polisi.....polisi nao kweli wanaenda nyumbani....tehe tehe tehe.....
Ila naamini wangeandika wale wa hollowod,angalau angetupwa mpakani (labda mbeya)huko kwa sababu tulishasikia aliyemteka ni mgeni na dsm yote tuliambiwa askari hawalali usiku na mchana wanamsaka mtekaji!