Special thread: Kampeni ya kumsaka Roma nchi nzima kila sehemu

Special thread: Kampeni ya kumsaka Roma nchi nzima kila sehemu

Kama Simu Yake Inaita Kwanini Polisi Wasiitafute Sehemu Ilipo?

Kama Kuna Watu Wanaofanya Kazi Kwenye Mashirika ya Simu Wenye Uwezo Wa Kuitazama Simu Inaita Kutoka Sehemu Gani Wanaweza Kusaidia
Hili jambo limekaliwa kimya na mamlaka sabau wanajua wanachokifanya, sisi hatuna haja ya kujiuliza hayo maawali sananu tayati yana majibu. Rais alijihusisha moja kwa moja ishu ya Ney ni kielelezo tosha, sasa usimtafute mchawi sababu anajulikana, kilichopo ni kumkalia kooni mchawi amrudishe ROMA akiwa HAI.
 
*SINDANO*[emoji116][emoji116]



KILA KONA NI VILIO.......

Na Thadei Ole Mushi.

Mwaka jana 2016 Raisi Magufuli alipoteua wakuu wa Mikoa, Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajabu alikuwa maarufu Gafla.

Huyu ni yule mkuu wa mkoa aliyelia hadharani baada ya kuachwa kwenye uteuzi nafikiri mnakumbuka alivyokuwa analia kwa kusema nimekosa mimi,nimekosa mimi nimekosa sana huku akijifananisha na Yona wa kwenye biblia ili Raisi amuonee huruma.

Kwa taarifa tu huyu jamaa ni Dr wa Kilimo analia kwenye nchi yenye Rutuba na maji kila mahali huku yeye akiwa na elimu ya kilimo.

Nimeaamka Leo nasikia Shy Rose naye anaulilia ubunge wa Afrika mashariki. Kwake yeye ubunge ndio kazi yake tu hakuna mtu mwingine anayeweza kuifanya zaidi yake.

Hapa ndipo Tanzania ilipofikia kuna baadhi ya Familia zimeshajitweza kuwa wao wanatokea kundi la viongozi .. ndio maana sioni ajabu kwa kina Godlisten Malisa kulia kukatwa majina yao huku kina Masha wakichukuliwa kwenda kugombea ubunge wa A. Mashariki.

Najua Malisa atakuwa kajiokoteza hadi akatoa laki 5 akachukua form huku akiamini anafaa kulisemea taifa lake kwenye Jumuiya ya A. Mashariki.... sitaki kurudia kilichomtokea ila ndio hivyo yeye hajatokea kwenye kundi la familia za kuliongoza taifa hili.

Naaamka asubuhi nakuta asilimia 50 ya walioteuliwa wote na CCM kugombea ubunge wa A. Masharikia ni watoto wa Viongozi kwa asilimia 100. Hii ni aibu kwetu CCM. Majina yao ni haya:-

Zainabu Rashid kawawa, Dr Ngwaru Jumanne Maghembe, Adam Omari Kimbisa, Charles Makongoro .

Hawa toka wanazaliwa wanakula grade A ya Keki ya Taifa hili na wazazi wao wamefanikiwa kuwarithisha madaraka ili na wajukuu zao waendeleee kula mema ya nchi.

Hata hao wengine 4 waliobaki bado watakuwa na utengamano na viongozi hii ndio ccm na hii ndio Tanzania hivyo Malisa kuwa mpole.

Itabidi uwe na akili za ujuha kuendelea kuwasifia na kusema CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi.....

Naamka nakutana na post ya Mbunge Sixtus Mapunda akifurahia mwanawe kupewa jukumu la kumkaribisha waziri mkuu wa Ethiopia ... Anafurahia kwa kuwa ndio anaanza kumuandaa kuja kuongoza baadaye nampongeza kwa hili ndio hivyo ni kuandaana tu.

Naamka nakutana na SMS za vijana waliomaliza ualimu miaka miwili iliyopita wakiniulizia kama yanayosemwa ni ya ukweli kuwa mwaka huu wataajiriwa waalimu wa Sayansi tu.

Mpaka sasa sijawajibu kwa kuwa najua nikiwajibu ukweli nitakuwa nimeuponda mioyo yao sana. Wengine ambao wameshaujua ukweli imebidi wanikumbushie zile salamu zangu nilizowapa kipindi wanahitimu.... Niliwatumia salamu hizi.

"SALAMU ZANGU KWA WAHITIMU MSIMU HUU WA GRADUATION

Asilimia 90 ya wakazi wa Mkoa wa Daresalam hawana kazi na hawaingizi chochote kwenye pato la Taifa. Hii ni kwa mujibu wa Dr Mpango waati wa uwasilishaji wa bajeti 2016/2017.

Asilimia 71 ya watanzania wote hufanya kazi zisizochangia chochote kwenye pato la taifa, kwa maana hiyo ni ajira zisizo rasmi leo ipo kesho haipo.Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mh Jenista Mhagama mapema mwaka huu alipokuwa akizindua mojawapo ya tafiti toka kituo cha takwimu Tanzania.

Tarehe 13/06/2014 Vijana zaidi ya elfu 10,000 walijitokeza kuomba ajira wizara ya mambo ya ndani nafasi 70 tu na hawakuzipata.

Tarehe 12/12/2014 vijana zaidi ya 10,000 walijitokeza kuomba nafasi 50 za kazi TRA.

Kila mwaka vyuo vikuu na vyuo vingine vya kati hutoa wahitimu zaidi ya 90 elfu mtaani na wanaoajiriwa hawazidi 20 elfu kwenye sekta rasmi.

Asilimia 20 tu ardhi ya Tanzania ndio ambayo inatumika kwa kilimo nchini.

Eneo kubwa lenye rutuba zaidi ya asilimia 46 ya eneo lote la Afrika mashariki Lipo Tanzania.

Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi ya kilimo, na 5% tu ndiyo inayolimwa.

Asilimia zaidi ya 50 ya wakazi wa jumuiya ya Arika mashariki inategemea chakula toka Tanzania.

Tuna mvua za kutosha kwa mwaka mzima, tumezungukwa na maji kila pembe ya nchi hii.

Kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012 vijana ni asilimia 35 ya watanzania wote. Nyie wahitimu mpo kwenye hili kundi la vijana, kundi hili ndilo linalopaswa kuzalisha na kulisha makundi mengine yaliyobakia (asilima 44 watoto na asilimia 21 ni wazee)

Vijana hawa asilimia 90 hawajui nini maana ya kilimo na hawajaandaliwa kwa ajili ya kutumia fursa hii. Haishangazi mhitimu wa SUA degree ya kilimo kwenda kukabana koo na aliyehitimu darsa la saba kwenye kijiwe cha boda boda huku wakigombea abiria.

Haitanishangaza mhitimu wa engineering tena wa maswala ya kilimo akiwa mrudifishaji CD huku akisakwa na wasanii kwa kuharibu kazi zao.

Usiniulize swali au nimewaza nini karibu uraiani, karibu mhitimu najua umekuja na vifaa vyako vya kazi (ipad, laptop,smartphone, na una external hard disc iliyojaa move na series za kutosha.

Vifaa hivi vitakusaidia sana ku chat na kuitukana au kuilaumu serikali.Vijana wamemezwa na siasa hata post hii haitapata wachangiaji, subiri umtaje Magufuli, mbowe au Lowassa utajua kila aina ya tusi la nchi hii."

KINACHOTULIZA.

Kinachotuliza ni kitu kimoja tu ni aina ya elimu tunayoipata. Haituandai kuja kujitegemea.

Tanzania na Eritrea ndio nchi pakee Afrika zenye falsafa ya Education for self reliance. Ikiwa na maana kuwa elimu tuipatayo ilenge kumjengea mtu uwezo wa kujitegemea. Leo hii Tanzania na Eritrea hawatofautiani sana kiuchumi kasi ya ukuaji wa uchumi wa Eritrea ni mkubwa kuliko wetu pamoja na matatizo waliyo nayo.

Lazma tukubali kuwa Elimu yetu haifuati falsafa ya elimu iliyopo na hatujui kuwa tupo wapi.Ni jambo la aibu kama elimu yetu haina dira wanafunzi wamekuwa wakijisomea tu bila kujua kesho yake atakuwa nani. Dira ya elimu katika nchi yoyote duniani ni Falsafa ya nchi husika. Tuna viashiria vingi sana vinavyotuonyesha kuwa tulishahama kwenye falsafa yetu ya elimu ya kujitegemea aliyoiasisi Mwl Nyerere.

1/. Kitu pekee kinachoweza kutafsiri Elimu ya kujitegema kwa mazingira tuliyonayo Tanzania ni Kilimo chetu. Mpaka sasa Sekta ya kilimo inachangia asilimia 24.5% tu kwenye pato la taifa. Pamoja na ukubwa wa ardhi tuliyonayo, Maji kila kona katika nchi yetu bado kilimo kipo taabani.

2/. Sera ya elimu ya 2014 nayo ni kiashiria cha kwamba hatuifutai tena falsafa yetu. Sera hii mpya inataka mtoto aanze shule akiwa na miaka 3 (elimu ya awali) na kama akimudu stadi za elimu ya awali basi aanzishwe darasa la kwanza. Kwa maana hiyo kuna wanafunzi wataanza elimu ya msingi akiwa na miaka 4. Mtoto atakayeanza katika umri huo tunategemea atamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 11. Katika umri huu mwanafunzi kama atafeli darasa la saba anaweza kufanya nini?? Kama waliomaliza wakiwa na miaka 13-15 walishindwa kujitegemea hawa watafanya nini??

3. Tunayofundishwa hayatafsiri jinsi ya kutumia rasilimali zinazotuzunguka. Kwa kuwa elimu hii haitafsiri kilichotuzunga tunakosa Ubunifu wa kutengeneza Zana za kuweza kufaidi rasilimali hizo (Technology) huwezi kutengeza zana ya kurina asali kama hujawahi kujifunza kuhusu nyuki nk.

4. Vyuo vyetu vikuu vimeendelea kutoa course zile zile za mkoloni. Aidha wamekuwa wakikopi course za nchi nyingine na kuzileta hapa kwetu.Vijana hawaajiriki kwa kuwa wanafundishwa jambo moja tu wawapo chuoni. Kwenye nchi yenye matatizo ya Ajira kama hii lazima tuwe na maltiple courses. Mfano mtu anayesomea Ualimu basi afundishwe na Kilimo, Mtu anayesomea Udaktari afundishwe pia na udaktari wa wanyama, Mtu anayesomea Uhandisi wa barabara afundishwe na uhandisi wa maswala ya Kilimo nk. Mtu anasomea ualimu tu tena wa Somo Moja akikosa anakuwa miaka yote aliyosoma ni bure.

5.Shule Zetu za ufundi zimetupwa wakati tunahitaji kutafsiri Tanzania ya Viwanda. Nilifikiri ni wakati sasa wa Serikali kufanya maamuzi ya kufundisha fani Mbalimbali za ufundi kwenye shule zote za Serikali itasaidia kuwabadili Mind set hawa vijana.

Wacha nisubiri Stephen M. Wasira anataka kurudi bungeni 2025 kama alivyoahidi atagombea ndio kazi pekee anayoijua na aliyozaliwa kwa ajili yake.

Ole Mushi
 
Where a uuuuu??????????? Roma Come back , come back, your family is missing you
 
Una mihemko hio hio je na yeye jalada lake likifungwa mtasingiziamtasingizia wenye mamlaka wamefunga jalada?
Inaonekana una mihemko ya kibashite!
Suala la Benn lilpigiwa sana kelele, wenye mamlaka wakakaa kimya hatimae wakasema wanafunga jalada!...
Ulitaka atafutwe kwa style gani??
...anyway je ulitaka basi roma wakae kimya?
 
Simu itakua inaitia kutoka wapi/ hata kama ni msituni si itajulikana tu leteni mawazo, Basata and Tanzania missing him very much naupenda mwimbo wa Marehemu Alyaah unaitwa Missing you

Mkuu Sijakuelewa Kabisa
 
[HASHTAG]#freeroma[/HASHTAG] [HASHTAG]#freemoni[/HASHTAG]
 
Jamani hivi haiwezekani kuitrack sim yake kama ipo hewani, wanadai sms whatsapp zinasomwa which means sim ipo on na data on wataalam watusaidie kulocate
Hayo yote yatafanyikaje wakt hakuna political will?
 
Wakuu Chapisheni Tshirt tuzinunue.. Zidizainiwe vizuri, ziwe na picha za Roma na Saanane, na maandishi,ziuzwe mtaani kama njugu.

Wasanii tunaomba mtoe nyimbo nyingi kuwalilia hawa vijana.

Serikali ikipiga marufuku tunajua mchawi Ni nani!
 
Inasikitisha sana kuona kuwa kwa baadhi ya watu hawaoni kama kunatatizo kwa watu kupotea bila ya kupata Maelezo making kutoka ktk vyombo vya dola, halafu watu wengine kulifanyia mzaha tatizo hili!...., kwako wewe kutafuta hela ni muhimu kuliko utu?....something must be wrong in your brain!
Mkuu huyo si binadam na Inshallah km anafanya mzaha basi Mungu atamshushia la kumshushia ataijua dunia, kuna muda unaweza muona mtu anapata shida ya maradhi au jambo lolote kumbe Mungu anamuadhibu kwa jambo au kauli aliyowahi kutoa na akadharau kuona ni kawaida tu. Huyu ni MSHENZI. waswahili wanajua mtu mshenzi ni mtu wa aina gani. SHENZI KABISA.
 
Back
Top Bottom