Special thread: Kampeni ya kumsaka Roma nchi nzima kila sehemu

Special thread: Kampeni ya kumsaka Roma nchi nzima kila sehemu

Ndio maana polisi wakiuwawa na majambazi watu hufurahia kwani yako kwa ajili ya kulinda interests za CCM shenz. Mkiua kila mtu mtatawala nini sasa
 
Inakuaje mtu anapotea kiholela kivile na serikali iko kimya? kuna haja ya kuwa na jeshi la polisi kweli au turudishe sungusungu za kina mtemi mirambo. Naunga hoja ya kumsaka,tuanze na kukaa na balozi wa nyumba kumi wasadie katika msako.
 
Kama Simu Yake Inaita Kwanini Polisi Wasiitafute Sehemu Ilipo?

Kama Kuna Watu Wanaofanya Kazi Kwenye Mashirika ya Simu Wenye Uwezo Wa Kuitazama Simu Inaita Kutoka Sehemu Gani Wanaweza Kusaidia
Kama kuna mkono Wa serikali,usitegemee watatoa support yoyote
Ndio maana wana ujasiri Wa kuiacha simu hewani Hadi WhatsApp sinaonekana zinasomwa
 
Daah nimeskiliza songi la mshikaji Viva Roma Viva.... nimejikuta nalia tu. Poa lakini ipo siku tutaelewana
 
Mke wake kuzunguka vituo vyote vya police
Lakini RPC Wa kinondoni anasema hawajapata taarifa zozote za kutekwa kwa Roma
It only happens in Tanzania
 
Inasikitisha sana vijana wanapotea polisi ambao ndio tunategemea waseme walipo au waliowateka kulingana na taaluma yao inavyowataka wanashindwa kutoa majibu ya kuridhisha...Ben Saanane nae ilikuwa hivi hivi ila kimya hadi sasa.
 
si bora huo muda wa kwenda kutafuta mtu aliyeamua kujipoteza mwenyewe uutumie Walau kwenye shughuli za kilimo,tena na masika hii?
 
Back
Top Bottom