lonewolf ranger
JF-Expert Member
- Feb 22, 2013
- 476
- 149
- Thread starter
-
- #81
Mkuu, hapa bongo secret service unaweza kuifananisha na TISS kitengo kinachomlinda JK. Ila tofauti kati ya hao SS na hawa TISS wetu ni kubwa mno. (1) Secret Service ni wanajeshi from US Forces, wanakua either in active combat duties or not. Yani ni lazima uwe umeshapitia uaskari. (2) TISS wa bongo wengi wao ni watoto wa mjomba au shangazi... "KAMLETE". Ndio maana JK alikuwa na kashfa ya kujaza ndugu zake huko. (3) SS ni taasisi inayojitegemea, ikiwa na kazi ya KUMLINDA RAIS ili aweze kutekeleza majukumu yake kikatiba (4) TISS wao kazi yao ni kama yule mbwa wako pale nyumbani, ukimwambia bweka... anabweka. wao hawako kusimamia katiba, wao ndio matapeli hapa mjini, wezi, majambazi na kila aina ya uchafu unaoujua wewe.
Nimekuelewa ndugu MD25 , maana hiyo tanzani inazalisha makondo ambao ni HALF BAWA ambao sio makomando kamili, basi hii ni hatari maana hata teknolojia yetu kiusalama ipo chini.
Mkuu C.T.U unaweza kutoa maelezo zaidi juu ya kazi za hawa AMY RANGER je ni kama askari wa miguu bongo au ni makomadoo?
Nimekukubali sana CTU,nimesoma na nimefurahishwa na maelezo yako,ningependa kujua hiyo briefcase wanayoilinda inakuwa na nini na umuhimu wake.Naomba unieleweshe ndugu CTU.
ok kaka CTU nimekusoma,ila nina swali kidogo,ina maana ni lazima hiyo brifkes atembee nayo kokote anakokwenda rais?
Zipo hata Lugalo ipo....all though mimi nilishatumikia special force inaitwa ANTI TERRORISM UNIT FORCE-TAZARA Au kwa jina lingine kiliitwa KMT-Kikosi maalumu Tazara hiki kikosi kilikuwa ni kwaajili ya kuzuia ugaidi uliokuwa ukiendeshwa na makaburu wa afrika kusini wakipinga nchi za kusini mwa afrika kutumia reli ya tazara!!wakuu hivi tz hakuna special force kama green beret,army rangers & navy seals.
MD25 acha kudanganya wenzako,nimesoma maelezo yako na inaonyesha unaongea kitu usicho kijua.Kuwa Comando Half bawa haina maana ni makomamdo nusu,lahasha bali ni kwamba wamemaliza mafunzo yote ila tu wanasubiria kuruka na miavuli(parachuty)ni hilo tu basi!na wakat mwngine mtu anapenda kuvaa half cuz ile ndio basic na ndio phase ngumu kuliko nzote!
Kwenye red siyo sawa usije ukadhani wanaovaa bawa kama hili ni makomandooSpecial forces Tanzania zipo. Tatizo watanzania wengi ni wavivu kutafuta Facts.Kama ungekuwa umetembelea banda la JWTZ kwenye maonyesho ya sabasaba 2012,kilikuwepo kitengo kinachoelezea special forces ya JWTZ wanapatikanaje,mazoezi yao kazi zao na mambo mbalimbali wanayofanya. Nilipata kuongea nao. Afisa mmoja alisema wao kiujuzi na mafunzo wapo sawa karibia dunia nzima. Hii ina maana komandoo wa TZ ana ujuzi sawa na komandoo wa US,China,France,Russia etc. Hii ni kwa sababu makomandoo karibia wote wanafundishwa mbinu za SEAL's. Komandoo lazima afundishwe upambanaji toka angani,nchi kavu ikiwamo msituni na majini.Wengi wa makomandoo sare zao huwa zina alama ya bawa la ndege kifuani kushoto. Alisema ki uwezo makomandoo wanne tu wanauwezo wa kushambulia na kuharibu kijiji kizima kinacholindwa na jeshi.Alisema mafunzo mengi ya komandoo wa TZ waliyapata Russia,China,Israel,Cuba na Canada na miaka ya karibuni wengine wameyapata US.Alifafanua kiujuzi makomandoo karibu wote wanafanana ila wanazidiana technics ndogondogo na sare watakazovaa. Aidha alisema wakati wa mafunzo huwa kuna kadhaa ambao huwa wanakufa.Alitufafanulia mengi zaidi ya haya lakini mwisho alikataa kabisa kutueleza kwa sasa TZ wapo wangapi na kambi zao zipo wapi. Mwezi wa saba tembelea banda la JWTZ pale sabasaba -Dar utapata mengi zaidi ya haya ikiwemo ulinzi wetu wa anga na majini unafanyikaje kwa kutumia mitambo ya kisasa!. Utaelezwa historia nzima ya Jeshi letu la JWTZ na pia utaona Mama Maria Nyerere alipokuwa akichukua mafunzo ya mgambo,usije ukamdharau unapomuona sasa!
Mkuu ile brifcase inaitwa THE FOOTBALL ni case ambayo inatunza code zote za ku launch nyuklia ambazo ziko chini ya serikali ya marekani
Codes hata raisi mwenyewe hazijui na anazijua pale tu akitaka ku launch nyuklia hiyo
Halafu wakati wa ku launch anatakiwa awasiliane na mkuu wa kitengo cha nyuklia president na mtu mwingine mkubwa katika serikali ya marekani kama sio vice president ni secretary of defence sina uhakika sana hapa ndio wanaohusika ku launch
Pili sheria nyingine ya ku lauch hii kitu kama code inasema T hutakiwi kusema Tunatakiwa useme Tango or Tomato
Like TZC
TANGO, ZULU, CANADA
Na code yake au pasword ni jicho la raisi na huyo jamaa mwingine ambaye ni secretary of defence au vice president sina uhakika hapa
ikitokea raisi katekwa hawamuokoi yeye kwanza wana i secure FootBall kwanza kwani wamarekani wanaamini hata raisi akifa sio janga kubwa kuliko adui kumiliki football yao wanaweza waka launch nyuklia ku target all major cities yeyote duniani na kusababisha uhasama baina ya wamarekani na taifa lingine kitu ambacho kinawezankusababisha ww3
Au magaidi wakaamua kuipiga marekani yenyewe to all major cities za u.s kwa kutumia nyuklia zao wenyewe
Football inalindwa kuliko hata raisi na huo ndio ukweli kwani ile ndio roho ya taifa la marekani, nguvu yao iko pale ubabe wao wote uko pale...
Ndani ya hiyo briefcase ni just a laptop ambayo iko designed kwa ajili hiyo tu so itamuomba aingize eye varification password, then anaendelea na mambo mengine
I recomend uangalie movie ya salt ya angeline jolie kidogo wametoa idea kuhusu football
Au 24 nafikiri ya jack buer
Mkuu naomba nikurekebishe kidogo, hii kitu inaitwa nuclear football, au the football kama ulivyosema au president emergence satchel au the black box au the button.
Hii ni briefcase iliyona vifaa vinavyomwezesha raisi ku launch atomic/nuclear bomb pale atakapokuwa mbali na nuclear launching station.
Yani hii ni kama remote, anaitumia tu pale akiwa mbali na fixed command station. Mfano wa fixed command station ni white house situation room. Hiki ni chumba maalum ndani ya ikulu ya marekani kinachohusika na kulaunch na kumonitor nuclear weapons.
Kama alivyosema C.T.U hii the football rais uwa anaenda nayo kila mahali kwani ni kama remote yake itakayomwezesha kuendelea kuwa na uwezo wa kulaunch nuclear hata akiwa mbali na white house.
Katika kitabu cha Breaking Cover kilichoandikwa na Bill Gulley ambaye alikuwa afisa usalama ndani ya white house anasema the football ina vitu vinne ndani yake.
1. Kuna Black book njia za kuchukua ikiwa USA itashambuliwa kwa Nuclear.
2. Halafu kuna kitabu kikionyesha list ya sehemu zote ndani ya USA zilipo nuclear missiles
3. Karatasi 8 mpaka 10 za manila zikiwa zimeungwa pamoja zikielezea njia za kumwezesha rais wa USA kutumia emergence broadcast system. Hii ni njia inayomwezesha rais wa marekani kuwasiliana na raia endapo kutakuwa na hatari ya vita ama jambo kubwa linalohatarisha nchi.
4. Halafu kuna card yenye codes za kulaunch hizo nuclear missiles.
Hiyo briefcase yenyewe ni mtambo tosha wa kufanya hiyo shughuli ukiwa na antena kwa ajili ya mawasiliano na fixed command center.